Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Naunga mkono Mramba kutumbuliwa...

kosa lake ni kukosa ubunifu, yaan kila wakijisikia tu ni kuongeza Bei ya umeme kwa wananchi? hamna ubunifu mwingine tofauti na kuongeza gharama kwa wananchi?

Kwa nini wasipunguze zile offer za Units kwa wafanyakazi wao? au wazifute kabisa hizo offer...! haiwezekani wafanyakazi takribani zaidi ya mia 500 tuwalipie gharama za umeme afu wao wanapikia majiko ya Umeme kila siku, sisi tunajibana na mkaa au gas wao tuwalipie!! haiwezekani...
 
Hapo sasa ndipo siasa inapokuwa tamu ukigusa umeme umeme umemgusa kila mtanzania kila siku mwasema mmegundua gesi huku umeme mwataka kupandisha mimi ningekuwa rais ningefuta hii kitu eura
 
Nilitegemea Prof Muhongo atumbuliwe kwanza kisha wafuate wa chini yake.


Naona jamaa katolewa kafara
 
Duniani kote charges za umeme ni political issue na kuangalia muelekeo wa nchi ktk ku promote uzalishaji yaani viwanda nk pamoja na mazingira yaani utumiaji wa umeme na gas badala ya kuni . Sasa tanesco kabla y kupeleka huko ewura jamaa angeanzia na wizara ya nishati na madini
 
Kwa nini Tanesco isipunguze matumizi yao?

Kwa nini walikubali kuongeza mkataba na wahuni wa IPTL? ambao wanatunyonya sana?

Kwa nini wasipunguze matumizi ya mafuta katika kuzalisha umeme?
 
Rais ameshangazwa na kitendo cha watendaji waliopandisha bei ya umeme bila hata ya kushauriana na yeye, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu au Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo.

''Ninamshukuru sana Waziri wa Nishati na Madini kwa maamuzi ya kusitisha hayo. Kwa hiyo umeme hakuna kupanda bei, Amesema.
Kwani kanuni na sheria ya EWURA inawataka washauriane kwanza na Rais,Makamu na Waziri Mkuu kabla ya kufanya uamuzi wa kupandisha bei?
 
Tanesco hawapandishi bei ya umeme moja kwa moja kinachofanyika wao hupeleka mapendekezo then mamlaka zinazohusika huangalia kama kuna ulazima au laa. Hivyo kwrnye hili watu wa kwanza ni EWURA
 
Back
Top Bottom