Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Hivi kosa ndio hilo la kuiomba EWURA ipandishe bei ili kuweza kujiendesha?au kuna mengine?

Leo 1.1.2017 Prof. Muhongo amehojiwa na Radio One na kueleza sababu za kusitisha mpango wa EWURA wa kupandisha bei ya Umeme kwa 8.5% kama ifuatavyo: -
1. Kwenye mikutano ya 'public hearing' nchini kote wadau walipinga myongeza ya bei;
2. hadi jana 31.12.2017 EWURA, kinyume na matakwa ya sheria, haikuwa imepeleka ripoti ya uamuzi wake kwa waziri mwenye dhamana, kujadiliwa na kupitishwa/kuthibitishwa kabla ya kutangazwa kwa pendekezo la bei mpya;
3. Ufumbuzi wa matatizo ya kifedha (madeni) wa TANESCO hauwezi utatuliwa kwa kupandisha bei ya Umeme. TANESCO inatakiwa kuwa na mkakati wa ku-improve efficiency kwenye management yake badala ya kuongeza bei ya Umeme; na
4. Wakuu wa TANESCO hawawpaswi kulipana bonus kila mwisho wa mwaka kiasi cha kufikia Tzs. 60m/- kwa mtu mmoja wakati shirika linashindwa kujiendesha isipokuwa kwa kupandisha bei ya Umeme. Hii inamaanisha kuwa wananchi wakamuliwe ili ipatikane pesa ya mabosi wa TANESCO kulipana bonus! Prof. Muhongo amesema ameagiza hata hiyo bonus isilipwe au irudishwe kwa waliokwisha kulipwa.
 
Rais Magufuli leo ametengua rasmi uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini(TANESCO), Eng. Felchesmi Mramba.

Aidha Rais amemteua Dkt. Tito Esau Mwinuka kukaimu nafasi hiyo. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Mwinuka alikuwa mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM).



Atoke tu, ingawa maswahiba wamenuna .
 
Dah jamaa kaanza mwaka vibaya, kaweka rekodi ya kutumbuliwa siku ya mwaka mpya. Kwanza ilikuwaje atake kupandisha bei ya umeme wakati uzalishaji wa gesi ndio unaongezeka na umeme uzalishaji unaongezeka
wakuu unajua nawaonea huruma sana watanzania wajinga wasiojua haya mambo Tanesco, Baada ya Muongo kuingia aliondoa bonus ya wafanyakazi wa tanesco kinyume cha sheria. Lakini kwasababu wafanyakazi wa tanesco wanajitambua walipiga kelele waziri akabadilisha msimamo wake. Hapa katikati kuna makampuni yamezima mitambo yake kushinikiza tanesco kuwalipa fedha zao, Tanesco wameshindwa kuwalipa wazalishaji. Leo kwa lugha za kusema unawatetea masikini, unaua shirika la umeme. Ngojeni tusubiri, wawekezaji wanakataa kuwekeza kwenye sectoor hizi kwasababu ya tanesco kuchelewa kulipa leo unakuja unajifanya unawatetea wananchi while mmnaenda kinyume ya mikataba .......................let us wait
 
Kuna mtu humu alimuomba Mh Rais atengue uteuzi wa DG Tanesco duuh leo kamngo'a mtu
 
Atumbue na bosi wa Ewura sasa asiishie kwa wa Tanesco kwanini na wao Ewura wapitishe hiyo bei?
 
Yule jamaa wa EWURA aliekubaliana na ombi la Mramba la kupandisha bei ya Umeme anafanya nini ofisini mpaka leo??
Mramba ana makosa yake nae, lakini na yule jamaa nae angetimuliwa tu. Maana alichofanya yule M-Ewura ni sawasawa na Mwele wa NIMR, anapandisha bei bila kuwasiliana na Waziri husika
JIPU KUU ni TANESCO
 
Bado huyu wa EWURA

Huyu anatakiwa atumbuliwe kabisa waache kula pesa za mafisadi na kuja kusingizia professional...........

Sasa hivi kuna gesi inazalishwap umeme,Tanesco wamefunga Luku karibu kwa watumia 75% sasa hasara inatoka wapi?.........

Wakati mtu akitaka kuunganishiwa umeme ananunua nguzo,vifaa vyote kama mita ananunua sasa hizo garama zinatoka wapi?......

Mchawi ni Tanesco wenyewe waliokubali kuingiza siasa kwenye professional yao kusaini mikataba mibovu kama kuwalipa watu Milioni 400 kwa siku...........

Huyu mkurugenzi huwezi sema hana maslahi wakati umeme ukipanda na tozo yao kama EWURA inapanda pia....

Hawa ndio walisababisha mafuta ya taa yapande bila sababu eti uchakachuaji...

Uchakachaji unathibitiwa kwa kupandishwa mafuta ya taa?.......

Halafu kichekesho pesa wanayokusanya yote kwenye mafuta,umeme maji ni pesa ya kugawana tu kula kwenye vikao,posho na kuandaa press kwa ajili ya kutoa matamko......

Huyu anatumwa na wezi na wanyonyaji wenye kampuni za kufua umeme tuwe wa kweli hapa Rais kuchukua hatua wala siwezi shangaa............

Haya ndio majipu........
well said,,,,
 
Wewe ni mwongo. Dr. Tito anatoka Nyand za Juu Kusini, O-level alisoma Bihawana (Dodoma), A-level alisoma Azania, halafu UD. Sawa huo uhaya wake wewe ulikutana nao wapi?

Ngoja aje kukujibu
 
Sikubaliani na wewe,JPM alivyokuja Arusha kipindi cha kampeni umeme ulikaa kwa siku mbili bila ya kukatika. Ilikua ni mara ya kwanza tokea mwezi wa 6 2015.
Acha uongo wewe....hukumbuki JPM aliwaambia nini watu wa Tanesko na wizara ya nishati kuhusu kukatika umeme hovyo hovyo.

Magufuli kambeba sana huyu mkurugenzi
 
Wewe ni mwongo. Dr. Tito anatoka Nyand za Juu Kusini, O-level alisoma Bihawana (Dodoma), A-level alisoma Azania, halafu UD. Sawa huo uhaya wake wewe ulikutana nao wapi?

Ngoja aje kukujibu
 
Yule mpuuzi wa Ewura bado anafanya nn ofisini?
Leo watu hawapo job... Hadi kesho it's holiday... Kisheria mfanyakazi hatakiwi kuwa distabunce.... Hii ni aina yake ya huu uongozi....

Movie ya Friday Chris Tucker alimshangaa kwa kumuuliza Claig ice cube... How come you got fire on your day off! Anhhg!
 
Mimi naomba mnisadie... hivi alivyotumbuliwa anaondoka Tanesco au anaendelea kuwa mfanyakazi wa Tanesco ila tu anakuwa siyo Mkurugenzi mkuu tena?
Yule alikuwa ni DG hivyo anaondoka japo na virago vyake!
 
Back
Top Bottom