Magufuli hakika ulijitolea maisha yako kwa ajili ya Watanzania

Magufuli hakika ulijitolea maisha yako kwa ajili ya Watanzania

Kwa nini alijengea nazo Airport Chato ambako hakuna biashara ya ndege? Kwa nini alinunulia nazo korosho ambazo hakujua atazipeleka wapi? Kwa nini alilipia nazo wakina Halima Mdee na wenzake? Kwa nini alilipia nazo chaguzi za marudio kwa wabunge waliounga juhudi mkono ??
1. Kwani Chato ipo Kenya au Tanzania?
2. Hizo korosho alizonunua zinatoka Nchi ya Kigeni au Tanzania?
3. Hao wakina Halima Mdee na Wenzake ni raia wakigeni au Watanzania?
 
Vyeti mpo humu mitandaoni mmejaa mlitumbuliwa 13000 na Magufuli mnahasira nae
Hongera sana kama kumtukuza Magufuri na kumsifu ndiyo usomi wacha niitwe cheti feki milele na wasiojitambua.Nakubali kuitwa majina yoyote yale na Sukuma gang lakini moyo wangu uko salama maana yule dhalimu hayupo tena duniani ameenda kukutana na wale wote aliowaua sababu tu hawakukubaliana na uongozi wake.
 
1. Kwani Chato ipo Kenya au Tanzania?
2. Hizo korosho alizonunua zinatoka Nchi ya Kigeni au Tanzania?
3. Hao wakina Halima Mdee na Wenzake ni raia wakigeni au Watanzania?
Unatetea ujinga wewe.Kama wasomi wa Tanzania ndiyo ninyi basi Tanzania haiwezi kuendelea kamwe.
 
nilicheka juzi kuna mjinga mmoja anasema enzi za JK na Mwinyi kulikuwa hakuna mauaji 😃 😃 😃 😃

nikamkumbusha kifo cha mwandishi Mwangosi(RIP) na kutekwa na kuteswa kwa DR Ulimboka enzi za JK

nkamkumbusha tena mauaji ya Mapadri Zanzibar na uchomaji wa makanisa enzi za Mwinyi

mwisho nikamsihi asiwe msahaulifu ana asiwe mtu wa mrengo anapokuwa anadadavua mambo.
Kanisa gani na mauuaji ya mapadri gani yalitokea wakati wa Aliy Hassan Mwinyi au Hussei Ali Mwinyi?
Ukishindwa kujibu rudi kwenu Oort Clouds nje ya sayari ya Uranus in outer space.
Nchi hii imejaa vilaza wanaojifanya wanajua kila kitu
Merde
 
Naimbie ni Raisi gani ambaye alikuwa madarakani akaacha kupaendeleza kwao.

Tazama sasa Zanzibar inavyochanua unafikiri kwa nini?
Awamu zote zilitawala kwa weledi maana nchi ya Tanzania kwa ujumla wake ilikuwa mali yao hivyo waliweza kuendeleza kila mahali bila kujali kuwa walizaliwa wapi,ila alipokuja huyo wa awamu ya Tano miradi mingi alipeleka Chato kwao alikozaliwa.
 
Huyo mfu wako aliongoza nchi kwa maslahi yake, familia yake na wapambe wake usitukumbushe habari za huyo katili muuaji. Huna hata haya we ngedere eti alijitoa kwa ajili ya watu, labda alijitoa kwa ajili ya mamako. Yule mhutu mbaguzi? Aligawa nchi, alimsaidia nani, alifukuza wafanyakazi kwa chuki na roho mbaya tu, km ni vyeti, PhD yake ni feki na ukweli wake ukaondoa roho ya Ben Saanane. Wafanyakazi wa nchi hii waliishi kwa vitisho hawakujaribu kunyanyua midomo yao kudai hazi zao za kupandishwa madaraja wala mishahara maana ukijaribu jibu lilikuwa acha kazi km unaona hailipi, watu waliishi km wako jehanamu usitutoneshe vidonda we poyoyo.

Hakuna ajira miaka 6, mpaka leo watanzania wamejaa mitaani na vyeti vyao watu wanawakebehi, wanawatukana kisa Magufuli, yule shetani anatakiwa afe mara 7 bado hajafa na aitumikie adhabu ya kaburi inavyomstahili.
Punguza miemko, kuwa na stara.

Usiandike kama unaropoka, lugha za kejeli za nini hapa!

Kama hauwezi kuzuia hisia zako basi haina haja ya kubishana.

Ulitaka Magufuli akulambe miguu, na akuletee chakula mezani kwako.
Aliyoweza kufanya kwa uwezo wake na kwa watu kama nyinyi ambao ni selfish na wachumia tumbo wakubwa inatosha.

Halafu tatizo la ajira sio Tanzania tu, tatizo la Ajira lipo Duniani kote. Kama hujui ndio ujue sasa, uko tuendako Artificial Intelligence AI ita-mreplace mwanadamu kwa sehemu kubwa sana. Kitakacho matter ni wewe una Skills gani na sio wewe umesomea nini?

Ishi kwa mabadiliko ya Dunia yanavyokwenda husiishi kwa kukariri vinginevyo utakwenda na maji.​
 
Aliyoyasema na matendo yake vitu viwili tofauti, utajiri wa kutajirisha kwao hiyo ni falsafa mfu.

Hiyo ni imani tu. ukuaji wa nchi hii katika maeneo tofauti tofauti haupishani sana.
Sikilizeni hii ili muongeze uwezo wenu wa kung'amua mambo.

 
Nionyeshe rafiki zako nikuambie tabia yako. Kwa mtu aliyewateua watu kama Sabaya na Makonda kisha kuwalinda inaonyesha tabia yake ni ipi. Nachomsifia Magufuli licha ya mauaji na ukatili dhidi ya raia wake, wizi kama tunavyozidi kufunuliwa kupitia waandishi nguli kwenye kitabu cha I am the state. Upigwaji wa 1.5trillion ulioficguliwa na CAG profesa Assad aliposema akamtimua bado kuna majuha wanamuona mzalendo, hicho ndicho kipaji cha Magufuli
 
1. Kwani Chato ipo Kenya au Tanzania?
2. Hizo korosho alizonunua zinatoka Nchi ya Kigeni au Tanzania?
3. Hao wakina Halima Mdee na Wenzake ni raia wakigeni au Watanzania?
Alifuata taratibu za serikali kwa kwenda kujenga uwanja wa ndege wa Chato kijijini kwake bila ridhaa na kibali cha bunge?
Kipaumbele cha nchi kwa kutumia rasilimali za taifa ni kujenga uwanja wa ndege wa Chato nyumbani kwake?
Kwa kuvunja sheria na kanuni na katiba kwa kuwaingiza watu bungeni kinyume cha sheria mradi ni watanzania kwako ni sawa?
Kiungo gani unachotumia kufikiria?
 
Ukiwa mwenye akili fupi kama wewe, utaona amekufa. Lakini kwa wenye akili kubwa wanaendelea kumuona na kuishi naye. Ndiyo maana mpaka leo hii JPM haachwi kutajwa kila mahali.
Inategemea anatajwa kwa yepi, huyu ataendelea kutajwa kwa uovu na mauaji dhidi ya aliotofautiana nao.
Kuhusu wenye akili hata ukienda Mirembe wagonjwa huwaona wauguzi ndio vichaa
 
Back
Top Bottom