Magufuli na Lissu kukutana Kigoma kwa mara ya kwanza leo

Amepaniki joni
 
Ratiba za kampeni ziko wazi. Hivyo Jiwe hawezi kuingilia utaratibu wa Chadema
Naona Mzee mzima pumzi ina karibia kukata. Kaamua kuingiza wapiga kampeni toka nje ya nchi.
Shikamoo Lissu, Shikamoo Chadema. Ccm mna semaje? Upinzani upo au umekufa?
 
Tundu Lisu itabidi apishe shughuli ya kitaifa kwanza.

Yeye aendelee ni mkutano wake kesho maana hawezi kuingilia shughuli mahsusi ya mkuu wa nchi ambaye tayari yuko Kigoma!

Afadhali umejikaza kuwa mkweli na kukiri kwamba Tundu Lisu ni namba nyingne kwamba popote anapokuwa CCM mnakosa watu.
 
Pamoja na yote, hivi inakuwaje katikati ya kampeni za uchaguzi mkuu huyu bwana anafanya mambo haya?

Hivi mtu akitafsiri shughuli hizi kuwa ni kuzidiwa kwa mgombea Urais wa CCM John Magufuli na hivyo anaamua kutafuta usaidizi wa waziwazi toka nje ya nchi kwa vitendo kama hivi, atakuwa anakosea?

Je, hii mialiko ya marais toka nje isingeweza kusubiri uchaguzi upite? Na je, sheria na kanuni za uchaguzi zinasemaje? NEC mnasemaje? Huyu mtu anatenda sawasawa na kanuni na maadili yenu?
 
Kuna mambo yanapatikana Tanzania pekee...
 
Magufuli mtu wa maajabu sana. Usikute akatumbukia ghafla mkutano wa Lissu na kutangaza kuunga mkono juhudi za Lissu na kujitoa ugombea ili Lissu aje amkumbuke kwenye ufalme wake.
Heri nusu shari kuliko shari kamili.
 
Rais wetu ameshamaliza mkutano wa hadhara na Jenerali Ndayishimiye,jioni mgombea wetu atakua njiani kuelekea Tabora
 
Kigoma ni mji mkubwa hivyo sioni sababu ya wao kusuguana. Ufunguzi wa mahakama ya kanda inafanyika eneo la Bangwe mbali kabisa na Mwanga Community Center ambapo Lissu atafanyia mkutano wake. Lakini pia si kwamba Lissu wakati anafanya mkutano atakuwa peke yake kuna vyama vingine vitakuwa vikifanya mikutano maeneo mengine kama Gungu, Katubuka, Masanga, Kibirizi, Mlole, Kagera , Katonga na kwingineko
 
Mkuu tumeshaambiwa Namba moja anafanya mikutano 10 kwa siku na TL anafanya 1 - 4 kwa hiyo toa shaka.
 
Baada ya kukabwa kisawasawa, Mzee Baba anatafuta pa kuanzishia visa. Tunae mwaka huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…