Magufuli ni Rais muoga haijawahi tokea katika nchi hii

Adui akishafahamu udhaifu wako ulipo basi watakutesa kama mtoto mdogo na usijue cha kufanya...

Kwa hili la magufuli, wapinzani washagundua ya kwamba magufuli hataki kusemwa vibaya, so na wao wanatumia udhaifu wake huu kumsema zaidi na hili magufuli asipikuwa makini na vile ni mtu wa hasira sana anaweza fanya tukio baya ambalo litamuondosha madarakani kwa nguvu...

Na watu wenye tabia kama zake hawafai kupewa nchi maana atatengeneza makundi mengi katika utawala wake na hadi tunavyoongea ni kwamba kuna watu ndani ya chama chake wanatamani apoteze maisha kabisa maana washamchoka sema tu ndio hivyo ni nani wa kumfunga paka kengele...
 
Ulianza vizuri sana mwaka wa kwanza na nusu ya uongozi wako, you were the model of good African leadership and everyone was in love with you
Alianza vizuri na bado anaendelea vizuri tu kwan unadhan kwanini kama muswada sio wa haki mbona umepitishwa na bunge, wewe ni nani ulione bunge halina akili kuukubali na kuupitishwa muswada huo?? na by the way everyoneis still in love with him ( am talking about people who are not delusional)
 
Ukishapita muswaada wa Miaka 7 utafuata muswaada wa kutokuwa na ukomo kutawala milele, ili yatimie aliyonena itatawala milele
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unafananisha maendeleo ya vitu ambayo ni direct proportional na ukuaji wa uchumi na maendeleo ya tabia ya watu?

Watu hua hawabadiliki kwa generation moja au mbili,sayansi inasema walao miaka 1000!

Sasa kutoka Nyerere mpaka Magufuli kuna miaka 1000?

Hoja yako ya ulinzi ni ya kipumbavu maana Waziri Mkuu wa Sweden au Switzerland anaenda kazini kwa mguu na hana ulinzi wa aina yoyote!Halafu Sweden na TZ ipi imeendelea?

Yaani nchi zimekua na kuvuka stage ya ya u-savage na kwenda ustaarabu!

Tabia ya fujo,ulinzi,majeshi,kuuana,kuumizana,etc ni tabia bado za savage animals.

Sasa wakati dunia inatoka huko kwenda kwenye ustaarabu,wewe na jamaa zako mnaona ndio wakati wenyewe hasa wa mafujo na maulinzi ya kipumbavu,etc!
 
Majority ya wabunge wa chama tawala bungeni ndio inafanya wabunge wote waonekane wa hovyo. Unakumbuka suala la kikokotoo? Ndivyo ilivyotokea kwa muswada wa mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa. Wabunge wa CCM wakishaitwa kwenye caucus hawana usemi kbs kwa mwenyekiti wao
 

Sawa mm ni mpumbavu ila wewe mwenye hekima umeshindwa kujielewa n kutofautisha kati ya jamii moja hafi nyingine. Ulinzi na ujuzi wa sweden utaulinganisha na wa Tz? Ustaarab wao na maendeleo yao yanafanana na ya Tz? Ndo maana nimekuambia acha kukariri maisha.
 
Mkuu hongera sana kwa mada nzuri na ukweli mchungu kwa misukule,Tanzania hatuna rais tuna viroja .Vitendo vinavyofanyika Tanzania ni vya ajabu sana awamu hii ,Hata waliomuweka madarakani mkapa ,kikwete ,mwinyi wanajuta .
 
sio kweli, kwahyo unataka kusema wabunge wa CCM hawana uwezo wa kuona kwamba hicho kitu wanachokubali kupitisha kitakua na effect kwao hapo mbeleni? kiasi kwamba wakubali tu kisa wameambiwa na mwenyekiti wao? am sure hata wapinzani wapo walioafiki vizur sana na ndio mana umepita bila wasiwasi
 
Wao CCM wanaamini kwamba wataongoza milele. Hawaamini kwamba akili za wananchi inaadilika kutokana na kizazi, wanayoyaona yanafaa leo huenda yasifae miaka 10 ijayo. Hilo wao hawalioni ndio sababu wanapitisha takataka nyingi sana bungeni kwa sababu ya wingi wao. Haimannishi kwamba natete kila wanachopinga wapinzani, nao kuna mahali wanakosea sana tu. Wengi wape, lakini wachache wasikilizwe. Kumbuka ya mchakato wa katiba, nani walipinga katiba ya tume ya Warioba?
 

Kama kweli ile idara nyeti inatumia kodi za watanzania kusaka wakosoaji tena wanaokosoa kistaarabu na kwa kusema kweli, basi ujue kuna tatizo na inatakiwa ijitathimini kwa kina. Kama waliomfuata Zitto na kumtisha kumuua wanatoka huko pia, ni wazi kuwa kuna shida na weledi na utendaji umepwaya sana.

Idara ile haiko kwa ajili ya maslahi ya mtu au kikundi cha watu bali kwa maslahi mapana ya taifa bila kujali dini, rangi, itikadi wala kabila.
 
Pamoja na kutubu kwako hadharani lakini Nasikitika kukuambia kwamba hauko makini kabisa ! Mtu yeyote aliyekuwa ana akili hata ya kuvukia barabara tu alitakiwa awe amemfahamu Magufuli tangu alipokuwa Waziri , Matendo yake ya nyumbani na ofisini , ikiwemo hata hotuba zake jimboni kwake akiwa mbunge ilikuwa ushahidi kwamba akiwa Rais atafanyaje
 
Hamna anaesema apende upinzani.... lakini inabidi awavumilie maana walikuwepo, watakuwepo na walizidi kuwepo
 
Mkuu this regime imeng'oa ubongo wako now wamekupandikizia kitu kingine kabisa kichawani pole sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu bwana hajawahi kuwa kiongozi mzuri hata mara moja. Tatizo kubwa la watanzania wanadanganyika na vitu vidogo sana vya hadaa.

Tangu akiwa waziri wa ualiendesha mambo yake kwa hadaa nyingi. Hivi mlikuwa hamshtuki akienda kumkaripia mkandarasi, vyombo vya habari vilikuwa vikisema, 'amefanya ziara ya kushtukiza na kumkaripia mkandarasi', lakini cha ajabu ni kuwa safari ni ya kushtukiza lakini vyombo vya habari vyote vipo!

Kiongozi anayewanunua wanahabari ili wote wawepo wakati anafanya tukio lolote lile, mwogope sana. Madikteta wote duniani huwa hawataki wasikie mtu mwingine yeyote anasikika kwenye vyombo vya habari, isipokuwa yeye tu. Alifanya hivyo Mobutu, Idd Amin, Nguema, Pinochet, Samuel Die na wengine wote.

Msisikilize mtu anachobena, bali yasimeni matendo na tabia zake. Hapa tunafiga bomu. Siku likilipuka hakuna cha CCM wala CHADEMA au mwingine yeyote, wote tutaangamia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu anajithibitisha kupitia muswada huo - wakati Kingunge, Sumaye na Lowassa wakipitisha baadhi ya miongozo na sheria kadhaa kuhusu demokrasia nchini hawakujuwa kwamba mbeleni watakwaa kizingiti - tunaenda uchaguzi wa 2020 wabunge hao hao kitambo watajiona walivyokuwa wanazi

Amani ya nchi hii isichezewe - viongozi ondoeni hofu ya kupoteza nafasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…