Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Jaji Tiganga ameeleza kuwa migogoro inayowasilishwa mahakamani inahusisha masuala ya kisiasa, kiuchumi pamoja na kijamii, na kusisitiza kuwa upatikanaji wa haki unatoa nafasi kwa wananchi kujikita katika shughuli za kiuchumi na hivyo kuchochea maendeleo binafsi na ya taifa kwa ujumla.
Aidha, kwa upande wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2024 walibakiwa na mashauri 73, huku mwaka 2025 yakifunguliwa mashauri 168 na mashauri 202 yakisikilizwa na kumalizika, na kubaki mashauri 39.
Jaji Tiganga amebainisha kuwa mafanikio hayo si ya Mahakama pekee bali ni matokeo ya ushirikiano wa wadau mbalimbali wa sekta ya sheria wakiwemo Mawakili wa Serikali, Mawakili wa Kujitegemea, Jeshi la Polisi, Magereza, TAKUKURU pamoja na wadau wengine wanaowezesha usikilizaji na umalizaji wa mashauri kwa wakati.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha TLS Chapter ya Mbeya Philip Mwakilima anasema TLS iko tayari kushirikiana na Serikali na wadau wote kutafuta suluhu endelevu la changamoto hizi na kuhakikisha kwamba haki si tu inatendeka bali ionekana ikitendeka wakati wote na katika mazingira yote.
Anaongeza kuwa Katika kuadhimisha siku hii, ni muhimu pia kutaja changamoto ambazo sisi kama wadau wa haki tunaona zinahitaji nguvu ya pamoja ili kuleta ustawi wa maendeleo kitaifa:
1. Uhitaji wa maboresho ya Sheria ya Mawakili (Advocate Act) ili kuboresha usimamizi wa Taaluma, Nidhamu na Uadilifu katika sekta na kuongeza usawa, uwajibikaji na uadilifu wakati wa ushughulikiwaji wa Masuala yanayohusu nidhamu za Mawakili pamoja na kulinda Haki na Usalama wa Mawakili wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria.
2. Ucheleweshaji wa mashauri unaosababisha hasara kwa wananchi na wafanyabiashara.
3. Upungufu wa rasilimali, ikiwemo majengo, TEHAMA, na watumishi, hasa katika maeneo ya vijijini.
4. Changamoto ya kifedha kwa upande wa TLS katika utekelezaji wa Majukumu yake ya utoaji wa msaada wa Sheria kwa ukamilifu katika ngazi zote. Chama chetu bado kina changamoto ya kifedha. TLS pia imeandaa mpango mkakati ilikuendana na maono ya Taifa ya 2050 na ni rai ya TLS kwamba wakati tukitambua na kushukuru kwa mchango wa Serikali katika Kuiwezesha kutoa msaada wa kisheria kwa wahitaji tunaomba kwamba Serikali ione umuhimu sasa wa kuwa na mpango maalum naendelevu utakao wezesha TLS kutekeleza majukumu yake kwa Ukamilifu katika kuifikia jamii hasa katika masuala ya msaada wa sheria.
5. Kutokuoana kwa mifumo kati ya Mabaraza ya Ardhi na Nyumba na Mahakama jambo ambalo lina athiri ufanisi katika kuendesha mashauri hasa katika ngazi ya rufaa.
6. Changamoto za kujikita kwenye maswala ya kiufundi katika utoaji wa haki mathalani katika mahakama ya Rufani ambako makosa kama vile kutompelekea notisi ya rufaa mdaawa wa upande mwingine inaweza kupelekea kesi kufutwa.
7. Kusuasua kwa utekelezaji wa mapendekezo ya Mheshimiwa Rais Kuhusu haki jinai ambayo yanapelekea haki za watu wengi kuathiri wa. Mathalani kwa sasa makosa mengi hayana dhamana na wala muda maalumu wa upelelezi hivyo kuumiza watu.
8. Kutofautiana kwa mifumo ya utoaji haki kati ya Zanzibar na Tanzania Bara, mathalani kwa Zanzibar kama kosa halina dhamana mshitakiwa atapewa dhamana ikiwa itafika miezi sita bila kesi kuanza kusikilizwa. Hii inaleta ufanisi na kuziba mianya ya kutumia vibaya mfumo wa haki jinai. Lakini kwa Tanzania Bara makosa yasiyo na dhamana yanatumika vibaya kwa kuwa hakuna ukomo wa lini kesi lazima ianze kusikilizwa, naisipo sikilizwa nini kifanyike.
9. Sheria kuruhusu watumishi wa umma wenye taaluma ya sheria kupata uwakili bila kupitia Shule ya Sheria kwa vitendo. Licha ya Umuhimu wa Kifungu hiki, kukiwa na mazingira maalum na Mahususi hali hii pia inaleta taswira ya Ubaguzi kwa sababu inapendelea watumishi wa Umma tu; nazaidi tayari tuna Law School of Tanzania ambayo ilianzishwa kwa lengo la kuboresha taaluma ya sheria hivyo ni vyema kuhakikisha suala la Mawakili linabaki chini ya Law School of Tanzania na kama ni exemption basi utaratibu uhakikiwe na kuridhiwa na Law School of Tanzania.
10. Kutokuwepo kwa Corona au kuteuliwa kwa Corona wa kutosha ili kurahisisha mahitaji ya uchunguzi pale inapohitajika.