Mahakama Kuu: Kutangaza Washindi wa Uchaguzi waliopita bila kupingwa ni Kinyume cha Katiba

Mahakama Kuu: Kutangaza Washindi wa Uchaguzi waliopita bila kupingwa ni Kinyume cha Katiba

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imeamuru kuwa hakuna wagombea Ubunge,Udiwani na wenyeviti wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji kupita bila kupingwa na kutangazwa kwenye uchaguzi.

Uamuzi huo wa Mahakama umetolewa leo Machi 29, 2023 ambapo imetamkwa kuwa vifungu vinavyotoa utaratibu huo ni batili na kuwa vinakwenda kinyume na Katiba.

Kesi hiyo namba 19/2021 ilifunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Joran Lwehabura Bashange.
 
Asipojitokeza mshindani uchaguzi unaahirishwa mpaka apatikane?

Wale wapinzani wenye ushawishi watakuwa wanafanyiwa zengwe halafu anapitishwa mchovu mmoja wa kuzugia tu.
 
Mahakama ya Rufaa ilituangusha kutengeua hukumu iliyotolewa na Mahakama kuu kwamba Wakurugenzi kwa maana ya DEDs hawaruhusiwi kusimamia uchaguzi. Ulikuwa uamuzi wa kisheria lakini wa kipuuzi
 
Hao nao wivu tu unawasumbuwa kisa tu uchaguzi unakalibia ndio wanaanza kujisemelesha ili iweje kwanza! Hapo jaji kajichanganya

Kwahiyo kama mshindani wangu kajitowa katikati ya kinyanganyilo mimi sipaswi kutangazwa kama mshindi😞 huu utakuwa uonevu sasa
 
Kesi hii ilifunguliwa na Joran Bashange dhidi ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Hukumu ya Majaji watatu, Mgetta, Masoud na Kakolaki imekubaliana na hoja ya Bashange, hivyo imetamka kuwa kutangaza washindi wanaopita bila kupingwa ni kinyume cha katiba.

IMG_6508.jpeg
IMG_6509.jpeg
IMG_6510.jpeg
 
Ingetamka kabisa kwamba wote waliopita bila kupingwa na waliopitishwa tu kama kuzolewa na kijiko wote wamefutiwa ushindi.

Hiyo ni Kenya tu,hapa ndoto
 
Mifupa mingi JF leo.😁

....ila hili ni muhimu....bila kujali...
CHADEMA wapo kimya leo
 
Haya maamuzi ya mahakama kwa sasa ni story za kumbembelezea mtoto anywe uji. Cha aja uchaguzi ujao yatatokea haya haya, na hiyohiyo mahakama ndio itatumika na watawala kufunga watu watakapoinga huo uhuni.
 
Mahakama Kuu Tanzania imeamuru hakuna wagombea Ubunge,Udiwani wala Wenyeviti wa S/Mitaa/Vijiji/Vitongoji kupita bila kupingwa. Imetamka vifungu hivyo ni BATILI vinakwenda kinyume na Katiba.

---

View attachment 2570208View attachment 2570211View attachment 2570217
MAGUFULI ANAVUNJA KATIBA KWA MARA YA NNE Halafu kuna WAJINGA wanamsifia
1 Kumfukuza CAG
2.Kuzuia Mikutano ya vyama
3.Wabunge fake 19 namna walivyopata ubunge kumtoa mtuhumiwa Gerezani usiku ili aapishwe kuwa mbunge na kuwaacha bungeni huku wakiwa hawana Udhamini wa Chama kinyume na KATIBA
4.Hili la kupita bila kupingwa
 
2025 ccm wajipange kila mmoja kupigania ugali wake. Yale mambo ya kubebwa kama ya kina mwana Fa na kupita bila kupingwa hayatokuwapo.

Mkataba ni mama awe rais wapinzani washughulike na wabunge
 
Ni alikipigania yule mshamba wa chato kisa hakukijua kiingereza.

Ni ujuha kuendekeza lugha za wengine Tena kwenye mambo ya kiserikali Kama haya,lugha ya watu ambao tunasherekea kuwaondoa kila 9 disemba
 
Back
Top Bottom