Dalton Elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 968
- 1,978
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kuwa Mahakama Kuu ya Tanzania, inatarajiwa kutoa hukumu katika Kesi ya Kikatiba inayohusu haki ya mawakili kukutana kwa faragha na mteja wao, Tundu Antipas Lissu, akiwa gerezani bila kusikilizwa au kuingiliwa na maafisa wa magereza.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia, hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa saa 3:00 asubuhi katika mahakama ndogo maskala ya Dar es laam
Kesi hiyo inajikita katika masuala ya kikatiba na kisheria, yakiwemo haki ya kupata ushauri wa kisheria bila kuingiliwa na kulindwa kwa usiri wa mawasiliano kati ya wakili na mteja wake.
Chanzo: Chadema official