DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imepanga Agosti 12, 2025 kutoa uamuzi wa maombi ya mapitio yaliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu.
Uamuzi huo umetolewa leo Jumatano, Julai 16, 2025 na Jaji Elizabeth Mkwizu, baada ya kusikiliza maombi yamleta maombi (Lissu) na majibu ya Serikali.
Lissu amefungua shauri la maombi ya mapitio ya mahakamani, akipinga uamuzi wa Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam kutoa ulinzi kwa baadhi ya mashahidi wa Jamhuri katika kesi ya kuchapisha taarifa za uwongo mtandaoni katika Mahakama ya Kisutu inayomkabili Lissu.
Jaji Mkwizu amesema siku hiyo pia atatoa uamuzi kuhusiana na malalamiko ya Lissu aliyoyatoa mahakamami hapo akilalamikia askari Magereza wanavyomdhibiti kwa kumnyima fursa ya kuwasiliana na mawakili wake na kumzuia kupewa nyaraka kutoka kwa mawakili wake.