young solicitor
JF-Expert Member
- Dec 26, 2015
- 1,123
- 713
I'll try to put this as simple as i canHii ndio taarifa mpya iliyotufikia muda huu kutoka Mahakamani .
Taarifa inaeleza kwamba Mahakama kuu imeona kwamba Fatuma Karume alihukumiwa bila kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya Kamati ya maadili ya Mawakili , hivyo imetengua hukumu yake na kuitaka Kamati hiyo kumaliza jambo hilo kwa haki
Ikumbukwe kwamba Mlalamikaji kwenye hili Sakata la Wakili Msomi Fatuma Karume lililojaa chuki , Wivu na uzandiki alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali , Je unadhani bado anafaa kukalia ofisi hiyo ?
View attachment 1825533
Mfumo wa nidhamu kwa mawakili umegawanyika mara tatu
1. Advocate committee (kamati ya maadili ya mawakili)
2. Jaji wa mahakama kuu
3. Jaji mkuu
Sasa kilichotokea jaji wa mahakama kuu Hon. Feleshi JK alimsimamisha wakili karume na kuamuru msajili apeleke shauri lake mbele ya kamati ya maadili ya mawakili kwa hatua zaidi.
Kilichotokea Mwanasheria mkuu akapeleka malalamiko yaleyale pamoja na mengine mbele ya kamati ya maadili ya mawakili.
Sasa mahakama kuu leo imesema haikuwa sawa kwa mwanasheria mkuu kupeleka malalamiko upya wakati kuna amri ya mahakama kuu kumuagiza msajili apeleke malalamiko mbele ya mahakama kuu.
Hivyo basi amri ya Jaji Feleshi kumsimamisha Wakili karume bado inaendelea. Mpaka kamati ya mawakili itakapo kutana tena.
Ms Karume amesema atamuandikia msajili barua kuomba kurenew leseni yake ya uwakili kwani katazo la mda (interim order) la kumsimamisha limeisha (hii ni kwa mtazamo wake)
Disclaimer: huwenda tafsiri yangu ya hukumu imekaa kisheria mno tusaodoane kuelekezana