Mahakama Kuu yatengua hukumu ya kuvuliwa Uwakili dhidi ya Fatuma Karume

Mahakama Kuu yatengua hukumu ya kuvuliwa Uwakili dhidi ya Fatuma Karume

Kiukweli kabisa sasa imethibitika kabisa kuwa mahakama zetu hutoa hukumu kwa maelekezo ya serikali.

Mahakama zetu hazina uhuru wo wote hivyo ni vema mahakama zikapigania haki yake kama ambavyo katiba inataka!

Mahakama ziko Kenya, hapa kuna wapigania tumbo kwenye majengo ya mahakama.
 
Unajua katiba ni nini na ina kazi gani wewe? Kweli akili ni nywele....
Leo nilikuwa nasikiliza BBC World Service, walikuwa wanaongelea kuhusu protesters wa Thailand, Hong Kong na Myanmar wanaotaka mabadiliko ya kikatiba.

Kuna sehemu mtu akasema, hawa protesters wanakosa support ya watu wengi, kwa sababu wanajikita kudai mambo ya katiba ambayo watu wa kawaida hawaoni umuhimu wake.

Wangeongelea mambo kama ya bei za vitu kupanda, wangeweza kueleweka na kupata support kirahisi na watu wengi zaidi.

Sasa, naona issue ile ile inajirudia hapa JF kuhusu mambo ya Tanzania.
 
iyo katiba itakusaidia nini kwa sasa

nchi inahitaji mambo mengi zaidi ya katiba mpya

Miaka karibia 40 hakuna hiyo katiba mpya, ni maendeleo gani ya maana yamefanyika? Je katiba inazuia vipi maendeleo? Bendera fuata upepo mna kazi kweli kweli.
 
Hii ndio taarifa mpya iliyotufikia muda huu kutoka Mahakamani .

Taarifa inaeleza kwamba Mahakama kuu imeona kwamba Fatuma Karume alihukumiwa bila kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya Kamati ya maadili ya Mawakili , hivyo imetengua hukumu yake na kuitaka Kamati hiyo kumaliza jambo hilo kwa haki

Ikumbukwe kwamba Mlalamikaji kwenye hili Sakata la Wakili Msomi Fatuma Karume lililojaa chuki , Wivu na uzandiki alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali , Je unadhani bado anafaa kukalia ofisi hiyo ?

View attachment 1825533
IMG-20210621-WA0189.jpg
 
Bado anafaaa, maelekezo toka juu hata wewe ungefanya hivyo hivyo. Mnaambiwa badilisheni katiba hamsikii,siku atakuja mwendawazimu kweli
 
Ikiwa kama kiongozi anaweza kuamua nani ahukumiwe na nani aachwe basi bila shaka hatutanyamaza , ni mpaka itengenezwe Katiba mpya itakayoonda Rais kuwa mungu
Ndio kwanza ujuwe leo hii ipo tangu awamu ya kwanza watu huekwa ndani au kuachiwa huru kwa matakwa ya rais
 
Back
Top Bottom