Mahakama Kuu Zanzibar yaamuru Cryprian Musiba kumlipa Fatma Karume Tzs 7.5 bilioni

Hivi kwenye muungano suala hili limekaaje? Mtu wa bara unaweza kunyooshwa na mahakama ya visiwani kumbe? Kwahiyo, nikimzingua Mzanzibar, anaenda kunishitaki kule kwao nanyooshwa huko. Sasa tutafute wengine kama huyo jamaa wakanyooshwe huko maana hapa bara ni kama wanafumbiwa macho.
 
CCM watamlipia hiyo faini kwani ndiyo walikuwa wanamtuma kutukana watu
 
Hiyo ni Mahakama kuu ya Tanzania...iko moja nchi nzima bara na visiwani ila ina divisheni na registry nchini kote. Hivyo Mahakama kuu inayoketi Zanzibar ina hadhi sawa na Mahakama kuu inayoketi Bara.
 
Kwani kuna passport ta Zanzibar inayojulikana duniani au kuna nchi ya Zanzibar inayojulikana duniani ukijiuliza hayo maswali mchezo kwisha ndio maana masheikh wa uhamsho walishitakiwa bara na kufungwa bara
 
Hebu tulia wewe Layman. Mambo haya yamekuzidi uwezo! Kilangila.
 
MATAGA pitisheni bakuli kwenye magroupe yenu ya wasap πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
Fundisho kubwa maishani...asiyesikia basintena kweli alaaniwe amtegemeaye binadamu.....
 
Hebu tulia wewe Layman. Mambo haya yamekuzidi uwezo! Kilangila.
Zero brain. Kilangila.
 
Hamjambo? Mnaomjua Cyprian Musiba mwambieni Mahakama Kuu ya Zanzibar, ndio pale VUGA, yametoa HUKUMU leo. Yamesema ni yeye na GAZETI lake wameandika UONGO dhidi yangu
Nafahamu Fatma Kiswahili huwa hajui kuongea, na kuandika pia kumbe hawezi. Mambo ya ajabu sana, wakili wa Waswahili hajui Kiswahili.
 
Keep my words
.
Hamna kitu hapo. Hiyo hukumu ili iwe na meno dawa ivuke bahari na isomwe Bara..
Itasajiliwa na kuwa enforced ndugu...Zanzibar ni Tanzania...na hii pia yaweza kuwa ni test case precedent kama bara wanatambua hukumu za huko... Jibu ni rahisi tu - ndio... mfano uko kwa wale masheik wa uamsho walioshitakiwa Zanzibar na kuhamishiwa bara... sasa msiba ajipange, either appeal hiyo hukumu au vinginevyo amwangukie Fatma kwa style ya msigwa na kinana- hiyo ndio pona yake.
 
Lkn kumbuka Zanzibar ni nchi.Katiba yake inajifunga yenyewe..
Uamsho nguvu nyingi ilitumika kuliko sheria..
Mf=Bara wafungwa uwamishwa magereza tofauti lkn hawapekwi Zanzibar. Na hivyo kwa upande Zanzibar.
Hata kosa na hukumu bara na visiwani tofauti..
 
Wa uamsho kesi yao ilihamishiwa Nara sababu ugaidi Ni kesi ya kimataifa na kimataifa inayotambuliwa Ni jamhuri ya muungano wa Tanzania Sio Zanzibar.Mahakama za muungano ndizo zenye ubavu huo ndio wakaletwa Tanzania bara

Hii ya Musiba hukumu ile Haina nguvu Tanzania bara sababu imeamriwa na mahakama ya Nchi ya Zanzibar Nchi huru kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar
 
Kwani Masheikh wa Zanzibar kesi yao ilikuwa Mahakama za wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…