Pacha, Cyprian Musiba akishindwa kulipa hio hela yatapelekwa maombi mahakamani ya;
1) kukamata mali zote za Gazeti na za kwake binafsi ziuzwe ili alipwe Fatma Karume.
2) Kufungiwa account zake na za Gazetti zote za bank, pesa zilizomo kulipwa kwa Fatma Karume.
Deni lisipowezekana kulipwa kabisa kutokana na mali kutofikia kiasi anacho daiwa, basi maombi ya kumfunga yanaweza kufanywa mahakamani (Civil Jail Term, sio Criminal Jail) na kama maombi yatakubaliwa na mahakama basi itapigwa hesabu ya deni na kifungo atakachotakiwa kufungwa kwa gharama za Fatma Karume (Yani Fatma Karume atakua akimhudumia lishe yake Cyprian Musiba kwa kipindi chote atakachofungwa).
In short, Cyprian Musiba safari hii anaweza akatolewa marinda.