Mahakama ya ICSID: Professional bullying anayofanyiwa Profesa Mruma inafedhehesha jamii ya Wanazuoni

 
Hii ndiyo cream of the crop ya MaCCM. Mjitu hata body language yao imekaa kijizijizi. Ni kama vibaka wamekamatwa wameambiwa watubu wanaanza vigugumizi.
 
Mimi nashangaa sana Mwanasheria kuwa goigoi kwenye lugha ya Kiingereza, hii inawezekanaje?

Hivi kweli mtu unasoma hadi level ya kuwa na PhD halafu unashindwa kumudu lugha uliyotumia kujifunzia? Uliandika vipi hayo maandiko?
Aibu sana hii
 
Unamchukuaje academician kwenda kwenye negotiations za kibiashara? Jakaya alikuwa analeta watu kutoka private sector tena Nje ya Nchi mkamuina hazimtoshi,haya Sasa hao ndio wasomi wa Jiwe
 
Wako vizuri kwenye academics ila sio kwenye mambo ya biashara nk

Ndio maana watu wanatakiwa kuheshimu sana private sector,ukimuona mtu kajiajiri mpe respect refer yule Mkuu wa Mkoa aliyetumbuliwa na kuanza kulia eti ataishije na alikuwa ni Dokta.
 
Watu kama hawa wanaabisha na kufedhehesha Taifa zima.

Watu wa mataifa mengine watajiuliza, kama profesa yupo hivi, Doctor yupoje, mwenye masters yupoje, mwenye bachelor yupoje, na hao wasio na degree hata moja, watakuwa watu wa namna gani!!
IQ havitegemei Ulivyofaulu sana darasani mana Kuna IQ za aina nyingi tuu..

Pia huyo ni mtoto wa maskini zao la jamii yetu,hata wewe hapo matoto Yako Yako hivyo hivyo unless wanasoma Nje ya Nchi
 
Huyo Mruma na Kabudi ndo walikuja na ripoti ya uongo kwamba tunaidai Barrick Trilioni 495. Kama aliweza kusema uongo kiasi kile acha awe bullied tu kwasababu uadilifu wake unatia shaka. Hawa wazee wana mchango mkubwa kwenye umaskini wa nchi hii.
 
Yeye kama Rais anajua hilo anachukua hatua gani; yeye kila wakati kulia lia tu badala ya kuchukua hatua!! Nchi ndio inamomonyoka hivyo na yeye badala ya kuchukua hatua anaishia kulaumu!
The lady is not up to par!
Rais anategemea watu kama unatumbua huyu unaweka yule Bado wanafanya hivyo si Bora kupiga mnada tuu hii Nchi 😂😂

Kwa sababu shida kubwa ya Nchi hii ni kukosa maadili na sheria za kulindana Kwa hao wa Juu ndio maana upuuzi haiwezi kuisha.

Rais Alitaka kidogo tuu aondoe magari Kwa watu wa Juu Kila mtu akopeshwe ikaleta upinzani na likaisha hivyo.
 
IQ havitegemei Ulivyofaulu sana darasani mana Kuna IQ za aina nyingi tuu..

Pia huyo ni mtoto wa maskini zao la jamii yetu,hata wewe hapo matoto Yako Yako hivyo hivyo unless wanasoma Nje ya Nchi
Nayajua mapungufu ya elimu ya Tanzania. Watoto wangu wote, elimu ya chini wamesoma Tanzania, lakini kwa elimu ya chuo kikuu, wote wameenda nje, mmoja amemaliza, mwingine anamaliza mwaka huu, mwingine mwakani, na mwingine natarajia ataenda Cape University January mwakani.

Sitaki wapatwe na aibu ya kujiumauma vidole huko mbeleni. Natimiza wajibu wangu kama mzazi, mengine nawaachia wao.
 

Hakuna cha bullying hapo, hizo ni mbinu za wanasheria utetereke. Lakini Profesa Mruma kajibu na kujieleza vzuri kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…