Mahakama ya ICSID: Professional bullying anayofanyiwa Profesa Mruma inafedhehesha jamii ya Wanazuoni

Mtu aliyempeleka huyu bwana kutuwakilisha kwenye hii kesi must be criminally prosecuted. Ni lazima kulikuwa na conspiracy kuwa ile kesi nchi ishindwe ili watu wapate mgao wao!! How come huyo jamaa anashindwa hata kuzungumza? You cannot win when you send zombies like this man to represent you!
Alfu rais Samia alishwai kusema hili kuwa Kuna umakusudi maalumu wkt wa kuingia mikataba
 
Yeye kama Rais anajua hilo anachukua hatua gani; yeye kila wakati kulia lia tu badala ya kuchukua hatua!! Nchi ndio inamomonyoka hivyo na yeye badala ya kuchukua hatua anaishia kulaumu!
The lady is not up to par!
 
Profesa Mruma amepata pigo kubwa sana kwa umri wake; waliomtuma huko Duniani wamedhamiria adhalilishwe na lengo limetimia . Anaulizwa kwa fedheha " haya ndiyo unawafundisha wanafunzi wako wa UDSM?

Muuliza swali ni mtoto wake wa kumzaa. Kwanini tumeruhusu wasiojiweza watusimamie?

View attachment 2697730
Huwa tunawalaumu wacheza mpira wetu kwavile tuna nafasi yakuwatazama nakuona mapungufu yao...laiti tungekua na nafasi hiyo kuwatazama watumishi wa umma and the entire chain of command yetu tungelia machozi.

Hilo ni profesa linakupa hadi sup chuoni!

Rubbish!
 
Halafu unawakuta wanajitutumua kiswahili kiwe lugha ya kufundishia utadhani kwenye hiyo mikataba ya kimataifa watakutana na kiswahili! Inakera na kuhuzunisha sana, thamani ya elimu yetu ni changamoto.
Wajinga tu hao, ukiona mtu anasimama na kusema tupuuzie lugha ya mataifa na ndio lugha inayotumika kwenye biashara nyingi ujue huyo ni mjinga tu. Na wanaodanganywa hivyo ni maskini na watoto wao.
 
Kama wengi mnavyofahamu, Tanzania imekuwa ikishtakiwa na makampuni ya madini kwenye mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya kibiashara, ICSID kwa kosa la kufuta leseni za makampuni ya kigeni yaliyokuwa yameingia nchini kwa kufuata sheria zote, kisha yakafanya utafiti, na baadaye kupewa Retention Licenses, halafu kwa ubabe, Serikali ikazifuta leseni hizo.

Kampuni zilizokuwa zimefanyiwa uhuni huo ni takribani 6, mpaka sasa kampuni 3 zimefikisha malalamiko yake kwenye mahakama ya ICSID. Shauri la kwanza lilikuwa ni la kampuni ya Indiana, limekwisha, kama ilivyotegemewa, Tanzania tumeshindwa, na tumeamriwa kuilipa fidia kampuni ya Indiana ya Australia AUD 127m (zaidi ya shilingi bilioni 210). Montero ya Canada inadai fidia ya CAD 90m (zaidi ya shilingi bilioni 170), na Winshear ya Canada inataka fidia ya CAD 124m (zaidi ya shilingi bilioni 230).

Kesi ya pili inaendelea sasa, ikiwa kwenye hatua ya mwisho, na hakuna dalili yoyote ya Tanzania kushinda. Kesi ya 3, kati ya Montero v. Tanzania nayo inaendelea.

Kesi ya pili ni:

Winshear Gold Corp. V. United Republic of Tanzania (ICSID Case No. ARB/20/25).
Kesi hii ipo chini ya Rais Gabrielle Kaufmann Hohrer kutoka Uswizi.

Mashahidi wetu huko ni Prof. Mruma na Mwanasheria wa Serikali bwana Igenge.

Nimesikiliza mahojiano kati ya Wakili wa Winshear bwana Fordin na Prof. Mruma na mwanasheria Igenge, kwa kweli ni aibu tupu. Mapungufu yapo kuanzia kuonekana mtu unasema uwongo, kushindwa kuelewa maswali yanayoulizwa, kutoa majibu ya kujichanganya, kushindwa kuelewa hata sheria zetu, mpaka kushindwa kuongea Kiingereza vizuri. Igenge muda mwingine akabakia kusema tu yes, lakini akimaanisha no. Ni aibu tupu.

Nadhani hawa mashahidi walichokuwa wanaangalia zaidi ni kupata tu posho zao lakini siyo kufanya chochote cha maana. Fikiria mtu kama Igenge, eti ni mwanasheria, halafu hazielewi hata sheria zetu. Yaani mawakili wa Winshear ambao siyo Watanzania, inaonekana wanazijua vizuri zaidi sheria zetu kuliko wanasheria wetu.

USHAURI KWA SERIKALI:
Kama hatuna mashahidi kwa sababu utetezi wa kimaandishi tulioutoa ni wa uwongo, au tunaona hatuna utetezi, si afadhali tuwaite hao wanatushtaki, tukubaliane kuwalipa hiyo fidia wanayotudai kuliko kuendelea kuongeza hasara kwa kuwalipa watu kwenda huko Marekani wakati tunajua hawana msaada wowote, na wala hawawezi kubadilisha chochote?

Yaani tuwalipe hawa walioenda kutalii Marekani, halafu tuwalipe tena wanaotudai, hasara mara mbili, na wala hatujifunzi chochote.

Viongozi wa Serikali ni watu wa ajabu ajabu sana. Ni watu wanaopenda kutumia zaidi nguvu kuliko akili. Hawawezi hata kuelewa kwa nini tembo pamoja na ukubwa wote, na nguvu zote, lakini anaishi mwituni, na mwanadamu ana uwezo wa kumwua wakati wowote. Binadamu asiyetumia akili lakini anajivunia mabavu, hana utofauti na mnyama. Anaweza kufanywa chochote na wanaotumia akili. Usiyetumia akili, wakati ukifika utanyolewa na wanaotumia akili.

Nchi hii ni masikini sana katika kutumia akili, ndiyo maana kidogo tunachokipata kinachukuliwa na wenye akili. Sasa zile tozo za kwenye miamala ya akina mama nitilie zinaenda kuwalipa matajiri wa Indiana Resources, Winshear Corp na wengineo wanaotushtaki.

Kama una muda na bando la kutosha sikiliza mashahidi wetu Prof. Mruma na Igenge wanavyonyolewa bila maji na mawakili wazungu.

Hii si mahakama ni kundi fulani la wazungu lililokaa kukandamiza waafrika

Alafu Kuna watu wanataka tuendelee Kwa kutumia wawekezaji wakati wanazidi kutuumiza Kwa Sheria zao kandamizi.

Sh
 
Kwanza hii clip Watanzania wenyewe hamuielewi...

Lakini wote mnakosoa..

🤣🤣🤣😅
 
Kuandkia ni tofauti na kuongea.
Mwanasheria ni mtu anayepikwa kwa mafunzo mbalimbali, huko vyuoni wanaandika tu hawapewi kazi za kuwasilisha mbele ya darasa/wenzao? Hadi unafika ngazi ya PhD inamaana hujawahi kufanya presentation? Umetetea vipi maandiko yako?
 
Kama wengi mnavyofahamu, Tanzania imekuwa ikishtakiwa na makampuni ya madini kwenye mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya kibiashara, ICSID kwa kosa la kufuta leseni za makampuni ya kigeni yaliyokuwa yameingia nchini kwa kufuata sheria zote, kisha yakafanya utafiti, na baadaye kupewa Retention Licenses, halafu kwa ubabe, Serikali ikazifuta leseni hizo.

Kampuni zilizokuwa zimefanyiwa uhuni huo ni takribani 6, mpaka sasa kampuni 3 zimefikisha malalamiko yake kwenye mahakama ya ICSID. Shauri la kwanza lilikuwa ni la kampuni ya Indiana, limekwisha, kama ilivyotegemewa, Tanzania tumeshindwa, na tumeamriwa kuilipa fidia kampuni ya Indiana ya Australia AUD 127m (zaidi ya shilingi bilioni 210). Montero ya Canada inadai fidia ya CAD 90m (zaidi ya shilingi bilioni 170), na Winshear ya Canada inataka fidia ya CAD 124m (zaidi ya shilingi bilioni 230).

Kesi ya pili inaendelea sasa, ikiwa kwenye hatua ya mwisho, na hakuna dalili yoyote ya Tanzania kushinda. Kesi ya 3, kati ya Montero v. Tanzania nayo inaendelea.

Kesi ya pili ni:

Winshear Gold Corp. V. United Republic of Tanzania (ICSID Case No. ARB/20/25).
Kesi hii ipo chini ya Rais Gabrielle Kaufmann Hohrer kutoka Uswizi.

Mashahidi wetu huko ni Prof. Mruma na Mwanasheria wa Serikali bwana Igenge.

Nimesikiliza mahojiano kati ya Wakili wa Winshear bwana Fordin na Prof. Mruma na mwanasheria Igenge, kwa kweli ni aibu tupu. Mapungufu yapo kuanzia kuonekana mtu unasema uwongo, kushindwa kuelewa maswali yanayoulizwa, kutoa majibu ya kujichanganya, kushindwa kuelewa hata sheria zetu, mpaka kushindwa kuongea Kiingereza vizuri. Igenge muda mwingine akabakia kusema tu yes, lakini akimaanisha no. Ni aibu tupu.

Nadhani hawa mashahidi walichokuwa wanaangalia zaidi ni kupata tu posho zao lakini siyo kufanya chochote cha maana. Fikiria mtu kama Igenge, eti ni mwanasheria, halafu hazielewi hata sheria zetu. Yaani mawakili wa Winshear ambao siyo Watanzania, inaonekana wanazijua vizuri zaidi sheria zetu kuliko wanasheria wetu.

USHAURI KWA SERIKALI:
Kama hatuna mashahidi kwa sababu utetezi wa kimaandishi tulioutoa ni wa uwongo, au tunaona hatuna utetezi, si afadhali tuwaite hao wanatushtaki, tukubaliane kuwalipa hiyo fidia wanayotudai kuliko kuendelea kuongeza hasara kwa kuwalipa watu kwenda huko Marekani wakati tunajua hawana msaada wowote, na wala hawawezi kubadilisha chochote?

Yaani tuwalipe hawa walioenda kutalii Marekani, halafu tuwalipe tena wanaotudai, hasara mara mbili, na wala hatujifunzi chochote.

Viongozi wa Serikali ni watu wa ajabu ajabu sana. Ni watu wanaopenda kutumia zaidi nguvu kuliko akili. Hawawezi hata kuelewa kwa nini tembo pamoja na ukubwa wote, na nguvu zote, lakini anaishi mwituni, na mwanadamu ana uwezo wa kumwua wakati wowote. Binadamu asiyetumia akili lakini anajivunia mabavu, hana utofauti na mnyama. Anaweza kufanywa chochote na wanaotumia akili. Usiyetumia akili, wakati ukifika utanyolewa na wanaotumia akili.

Nchi hii ni masikini sana katika kutumia akili, ndiyo maana kidogo tunachokipata kinachukuliwa na wenye akili. Sasa zile tozo za kwenye miamala ya akina mama nitilie zinaenda kuwalipa matajiri wa Indiana Resources, Winshear Corp na wengineo wanaotushtaki.

Kama una muda na bando la kutosha sikiliza mashahidi wetu Prof. Mruma na Igenge wanavyonyolewa bila maji na mawakili wazungu.

Harafu mbona hayuko huru Ni kama hajiamini hapo Ni sehemu ambapo unatakiwa uongee Kwa maslai ya nchi na Kwa kukaza shingo.
 
Igenge kwa lugha yetu adhimu ya kipare maana yake ni sehemu ya sehem za siri za mwanamke ambayo ni kisimi almaarufu choke! So usitegemee kitu kingine zaidi ya msisimko kutoka kwa "igenge". Mtoa post umepata msisimko wa aibu kutoka kwa igenge
 
Mtu aliyempeleka huyu bwana kutuwakilisha kwenye hii kesi must be criminally prosecuted. Ni lazima kulikuwa na conspiracy kuwa ile kesi nchi ishindwe ili watu wapate mgao wao!! How come huyo jamaa anashindwa hata kuzungumza? You cannot win when you send zombies like this man to represent you!
Unamtukana Prof ni Zombie?
 
Ukiwakuta wamevimba kwenye V8 utasema watu wa maana kumbe mamburura Tu..hawa wasomi wetu wanatutambia Sisi Tu wa uswahilini
Ni afadhali hata wangejitambulisha kuwa professionally ni walimu wa chekechea kuliko kusema eti mmoja ni profesa mwingine ni mwanasheria mwenye masters degree.
 
Ameyataka mwenyewe mtu wa geology ametoka wapi na wanasheriaa sipati picha Yule aliye kuwa mwanasheria wa jiwe bwana adeledurus kilangi jamaa alikuwa mweupe mno

Hyo Kaz angepewa Andrew chenge tungeshinda hyo kesi
Mkuu hata Andrew Chenge tusinge shinda....
Yaani mwekezaji amepata leseni kwa kufuata masharti na muongozo wa sheria zetu za mwaka 2010, sasa Jiwe mwaka 2017 akabadili sheria za madini....
Wale wooote walioingia na masharti ya 2010 akawatimulia mbali... Sasa wamekwenda mahakamani.. Utashindaje kesi hiyo?

Maana hapo kuna mtu kaonewa
 
Nimesikitika sana binafsi na hii ni dhahiri hakukuwa na maandalizi! Hata wanasheria wetu lugha imewafanya waonekane hawajui watendalo.
Ccm walizoea kesi za kubambikia wananchi wanyonge tu na kutumia mitutu ya polisi. Nje ya hapo mnaona hakuna uwezo wowote wa kujinasua kwenye jambo lolote
 
Back
Top Bottom