Mahakama ya ICSID: Professional bullying anayofanyiwa Profesa Mruma inafedhehesha jamii ya Wanazuoni

Mahakama ya ICSID: Professional bullying anayofanyiwa Profesa Mruma inafedhehesha jamii ya Wanazuoni

Kuna wasomi wa MADRASA
wameuza Loliondo uarabuni
Wakauza gesi
Richmond
Bandari ndio wanamalizia
Mkuu wengi hata madrassa hawakumaliza wali attend kaswida tuuuu ndo watetetee maslahi ya nchi
 
Profesa Mruma amepata pigo kubwa sana kwa umri wake; waliomtuma huko Duniani wamedhamiria adhalilishwe na lengo limetimia . Anaulizwa kwa fedheha " haya ndiyo unawafundisha wanafunzi wako wa UDSM?

Muuliza swali ni mtoto wake wa kumzaa. Kwanini tumeruhusu wasiojiweza watusimamie?

View attachment 2697730
Aibu yetu yaani !
 
Hivi Mruma ni mtaalamu wa Sheria ama yule ni Geologist?

Why serikali inawatuma watu wa miamba wakalitetee taifa kwenye maswala ya Kisheria?

Muda mwingine unaweza kufikiria kuna baadhi ya watu wanataka Tanzania ishindwe, idaiwe Mabillion kisha nao wapate mgao.
Alienda Kama Shahidi
 
Hivi Mruma ni mtaalamu wa Sheria ama yule ni Geologist?

Why serikali inawatuma watu wa miamba wakalitetee taifa kwenye maswala ya Kisheria?

Muda mwingine unaweza kufikiria kuna baadhi ya watu wanataka Tanzania ishindwe, idaiwe Mabillion kisha nao wapate mgao.
Kwa upuuzi wa mikataba kama ya bandari, na iwe tu. Maana haliepukiki kabisa.
 
Tatizo kubwa la nchi hii watu hawana Professional Intergrity.
Wasomi wengi wanaendeshwa na Wanasiasa.

Kwenye la kuvunja mikataba wa kulaumiwa anajulikana wala sio Prof. Mruma
Uko sahihi Mkuu. Mruma hawezi kubadili rangi pale ilipofikia, maana pale vinasomwa vifungu. Vifungu vyenyewe vibovu, anajenga hoja yake wapi. Msingi mbovu nyumba haiwezi kuwa imara
 
Halafu alitakiwa apewe rehearsal na mwanasheria kabla ya kwenda pale, sijui kama hicho kitu kilifanyika.
Hao huwa wana kiburi sana, yaani akiitwa Prof hapa Tz ni ngumu sana kukubali msaada kutoka kwa wanasheria wa kawaida, si ajabu alishauriwa hivyo ila akapuuza.
 
Kiingereza cha kuandika wa level ya PHD ataandika vizuri tu tatizo kuongea sasa na ukute anaongeleshwa na mtu ambaye english ndo lugha yake aisee atatamani ardhi ipasuke afichwe kingine kumbuka hao mawakili walioenda huko si ajabu kukuta hawana uzoefu wa kuwakilisha washtakiwa kwenye mashauri magumu na kwenye mahakama za kimataifa usije fikiri wakili aliyezoea mahakama za kisutu eti ataweza shindana na maadvocate ambao leo yupo mahakamani new york kesho yupo paris mtondogoo yupo london keshokutwa yupo durban wiki ijayo yupo sao paulo wiki ijayo yupo abu dhabi
Hao mawakili wa kwenye hii kesi kama ndio mchujo ulifanyika na wakaonekana ndio wenye uwezo wa kuitetea nchi kwenye ngazi ya kimataifa, basi naomba kukiri kwamba tuna hali mbaya kama taifa!
Lakini bado hatujachelewa, tunaweza kuanza upya kuandaa watu mahiri, tuondoe ukiritimba wa kupeana kazi kwa connection.
 
Kuna wasomi wa MADRASA
wameuza Loliondo uarabuni
Wakauza gesi
Richmond
Bandari ndio wanamalizia
Kuna mpuuzi mmoja tu hapo toka Iran mwizi mwizi mwizi tu aliondoka karudi mmemkaribisha.
Huyo ndo kimeo.
 
Kwa nini kesi za humu nchini hazirushwi live? Waanze kuzirusha live hata za humu nchini tuwe tunaona mbivu na mbichi.
 
Issue sio matokeo tu, ukifatilia vyeti vyao ni vipanga kweli. Issue ni exposure! Huku private mahojiano/ negotiations kama hayo ni kila siku virtual meetings au physical.

Mfano kuna lugha za kisheria, kuna lugha za kibiashara, kuna lugha za kiuchumi n.k discussion kama ile lazima mtu awe na element of law na business.

Pia nimeshangaa hata body expression hazikuwa nzuri, ni rahisi kuonekana unadanganya, hujui, hujitambui n.k kuna muda professor alikuwa anatoboa karatasi kwa pen , mara afunue file unnecessarily n.k

Hivi tunaendaje kwenye case hizi bila hata rehearsal walau? Mambo ya nchi tunauliza maswali ambayo huoni yatasaidia nini!

Very embarrassing! Hili swala watu wanacheka lakini sio Issue ya kutaniana bali ni Issue ya kuibua mjadala uwezo wa watu wetu. Hii case nani anasimamia? Hawa watu wameandaliwa vipi? Hata kama ni case ya kushinda utashinda vipi namna hii?

Binafsi nimejisikia vibaya sana, ningekuwa na uwezo ningeifuta ile video maana inatuvua nguo tu.
Hazifutiki..

Mimi pia nimeshangaa kumbe hawa ICDS wana YouTube channel Yao na hearing ya kesi hii yote imepositiwa huko..

Kuna video za kesi hii part 1 hadi 7 na zote ni za masaa kati ya 2 hadi 3½ ..

Ama kweli sasa dunia hii ni ya uwazi mno. Bila shaka hata Tanzania tunahitaji kesi zote zisikilizwe Kwa uwazi wa namna hii...
 
Back
Top Bottom