Voice of Tanzania
JF-Expert Member
- Sep 23, 2018
- 2,036
- 3,107
Khaaa udsm hyo na huyo ndo mzalisha vilaza na machawa wa Sasa na wajao
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Muacheni kabudi mbali kwenye hili. Amekaa kimya kama maji mtungini! Mshauri wa mikataba! Amepigwa na kitu kizito baada ya sheria aliyotunga mwenyewe ya umiliki wa raslimali zetu! kubadilishwa. Mngojee kama atatoa hata pumzi kwenye hili!Na Jaji Masaju ni mshauri wa nini? Kama Kabudi ni mshauri wa kisheria ?
Ficha ujinga wakati mwingine
Mkuu Isanga msaada wa iyo linki ya video. Ama ndio ile mrangi alitupiako?Daah nilikua namwonea imani sana Prof wa Tanzania huyo maana niliona kaingia ngoma za watu na kutoka hawezi aisee sitamani kuiangalia tena ile video...
Nimeicheki asee. Dah jamaa alikuwa anatetemeka balaa mikono inasheki. Yani hat msukuma na kibajaji wanaconfident kumshinda.Daah nilikua namwonea imani sana Prof wa Tanzania huyo maana niliona kaingia ngoma za watu na kutoka hawezi aisee sitamani kuiangalia tena ile video...
Aisee ccm mnawakati mgumu sana sema mnatumia nguvu kubaki madarakani.Yani jamaa mdoga anavomuendesha mzee kilaza mruma alafu anaulizwa ndio unavowafundisha hapo UDSM.
Inaleta picha gani kwamba maprofa vilaza na phd za mchongo walizonazo hapa tz.
Aisee ccm mnawakati mgumu sana sema mnatumia nguvu kubaki madarakani.
Hakuna kesi tulizoshinda.View attachment 2698364
View attachment 2698365
Tulia weweeKuna nini huko? Mbona kelele nyingi?
Inaumiza sana na ni hatari hata Kwa usalama wa nchi...Tunaonekana hatuna tunachokiweza so hata kuingiliwa na kudanganywa itakuwa rahisi. Hivi nchi iliruhusuje watu kama hao kwenda huko bila kuwa scrutinized? Afadhali angekuwa mmoja tu ndiyo Yuko hivyo, karibu wote pale ilikuwa ni kama walichaguliwa wabovu kwenda huko....Daah hii kitu imetudhalilisha sana watanzania.Issue sio matokeo tu, ukifatilia vyeti vyao ni vipanga kweli. Issue ni exposure! Huku private mahojiano/ negotiations kama hayo ni kila siku virtual meetings au physical.
Mfano kuna lugha za kisheria, kuna lugha za kibiashara, kuna lugha za kiuchumi n.k discussion kama ile lazima mtu awe na element of law na business.
Pia nimeshangaa hata body expression hazikuwa nzuri, ni rahisi kuonekana unadanganya, hujui, hujitambui n.k kuna muda professor alikuwa anatoboa karatasi kwa pen , mara afunue file unnecessarily n.k
Hivi tunaendaje kwenye case hizi bila hata rehearsal walau? Mambo ya nchi tunauliza maswali ambayo huoni yatasaidia nini!
Very embarrassing! Hili swala watu wanacheka lakini sio Issue ya kutaniana bali ni Issue ya kuibua mjadala uwezo wa watu wetu. Hii case nani anasimamia? Hawa watu wameandaliwa vipi? Hata kama ni case ya kushinda utashinda vipi namna hii?
Binafsi nimejisikia vibaya sana, ningekuwa na uwezo ningeifuta ile video maana inatuvua nguo tu.
Hii nchi itaishia kuwa ya vilaza, physics ya A-level imekuwa nyepesi namna hiyo?Nimepitia yale maswali ni mepesi sana
Kila swali marks kumi na unafanya maswali 10 hiyo physics
Profesa Mruma amepata pigo kubwa sana kwa umri wake; waliomtuma huko Duniani wamedhamiria adhalilishwe na lengo limetimia . Anaulizwa kwa fedheha " haya ndiyo unawafundisha wanafunzi wako wa UDSM?
Muuliza swali ni mtoto wake wa kumzaa. Kwanini tumeruhusu wasiojiweza watusimamie?
---
Winshear Gold Corp. Vs. United Republic of Tanzania (ICSID Case No. ARB/20/25).
Kesi hii ipo chini ya Rais Gabrielle Kaufmann Hohrer kutoka Uswizi.
Mashahidi wetu huko ni Prof. Mruma na Mwanasheria wa Serikali bwana Igenge.
---
Video 1: Profesa Mruma akihojiwa
View attachment 2698386
Video 2: Mkurugenzi wa Huduma za Sheria(Wizara ya Madini) Edwin Igenge akihojiwa na Robert Denison
View attachment 2698385
---
WASIFU WA PROFESA MRUMA
Dkt. Mruma ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye kwa sasa ni Profesa wa Jiolojia. Profesa Mruma kwa sasa anahudumu kama Kamishna wa Tume ya Madini nchini Tanzania.
Mwaka 2017 Hayati Rais Magufuli alimteua Prof. Abdulkarim Mruma kuwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Kuhifadhi Mafuta (TIPER)
Profesa Mruma alijizolea umaarufu 24 Mei, 2017 baada ya kuongoza Kamati maalum iliyondwa na Rais Magufuli kuchunguza mchanga ulio katika makontena yenye mchanga wa madini (makinikia) yaliyopo katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania
-
Dkt. Abdulkarim Hamisi Mruma Ph.D. M.Sc. B.Sc. ni Mkurugenzi wa Kujitegemea wa Tanzania Royalty Exploration Corporationration. Dkt Mruma ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako kwa sasa ni Profesa wa Jiolojia.
Masomo yake ya Uzamili yalijumuisha tafiti katika vyuo vikuu na taasisi za Serikali nchini Ujerumani, Ubelgiji, Zimbabwe na Ufini.
Ameandika ripoti za kiufundi kuhusu mada mbalimbali za kijiolojia na kuchangia katika majarida kadhaa ya kiufundi na yasiyo ya kiufundi juu ya anuwai ya masomo ya Jiolojia.
Orodha ya machapisho hayo ni pamoja na Jarida la UNESCO la Sayansi ya Ardhi ya Afrika na Jarida la Tanzania la Sayansi ya Dunia.
Mbali na majukumu yake ya kitaaluma, Dk. Mruma ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania nafasi ambayo ameitumikia tangu Oktoba 2004.
Pia anahudumu kama Mjumbe wa Bodi ya Chuo cha Sayansi za Ardhi cha Williamson Diamonds Limited cha Chuo Kikuu cha Dodoma na Shirika la Madini la Taifa la Tanzania mshirika wa ubia wa Kampuni ya Uboreshaji wa Mradi wa Buckreef Gold Mine.