Mahakama ya ICSID: Professional bullying anayofanyiwa Profesa Mruma inafedhehesha jamii ya Wanazuoni

Mahakama ya ICSID: Professional bullying anayofanyiwa Profesa Mruma inafedhehesha jamii ya Wanazuoni

Wawekezaji wajiandae, wajue wakija kufanya Biashara nchini kwa Hila ama zao wenyewe ama kwa Hila za baadhi ya watanzania wenzetu tuliowaamini wajue watafilisiwa siku zijazo. Na hao baadhi waliowaingiza mkengeni watawabeba!
 
Daah nilikua namwonea imani sana Prof wa Tanzania huyo maana niliona kaingia ngoma za watu na kutoka hawezi aisee sitamani kuiangalia tena ile video...
 
Na Jaji Masaju ni mshauri wa nini? Kama Kabudi ni mshauri wa kisheria ?

Ficha ujinga wakati mwingine
Muacheni kabudi mbali kwenye hili. Amekaa kimya kama maji mtungini! Mshauri wa mikataba! Amepigwa na kitu kizito baada ya sheria aliyotunga mwenyewe ya umiliki wa raslimali zetu! kubadilishwa. Mngojee kama atatoa hata pumzi kwenye hili!
 
Daah nilikua namwonea imani sana Prof wa Tanzania huyo maana niliona kaingia ngoma za watu na kutoka hawezi aisee sitamani kuiangalia tena ile video...
Nimeicheki asee. Dah jamaa alikuwa anatetemeka balaa mikono inasheki. Yani hat msukuma na kibajaji wanaconfident kumshinda.
 
Professor hata Kiingereza ni issue, lawyers siku zote ni washenzi na hapo wameshamsoma hawezi hata kujieleza kwa ufasaha kwa kiingereza, ni mashambulizi, next time watafute mkalimani au waajiri wanasheria wazungu kwenye timu yao ya utetezi, kesi tumeshindwa kabla haijaisha
 
Ila alivyokuwa anajibu Mruma ni aibu tupu! kama 'zero brain' vile!
Au nae alikuwa "amechukua chake" kama waliopitisha huu mkataba walivyochukua chao!!
 
Yani jamaa mdoga anavomuendesha mzee kilaza mruma alafu anaulizwa ndio unavowafundisha hapo UDSM.
Inaleta picha gani kwamba maprofa vilaza na phd za mchongo walizonazo hapa tz.

Aisee ccm mnawakati mgumu sana sema mnatumia nguvu kubaki madarakani.
Hakuna kesi tulizoshinda.View attachment 2698364
View attachment 2698365
Aisee ccm mnawakati mgumu sana sema mnatumia nguvu kubaki madarakani.
Hakuna kesi tulizoshinda.[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
My name is Pro Mruma actually i was not resiponsibo tu buringi them here, i was noti filingi welooooo tudeiiiii
🤣🤣🤣
 
Issue sio matokeo tu, ukifatilia vyeti vyao ni vipanga kweli. Issue ni exposure! Huku private mahojiano/ negotiations kama hayo ni kila siku virtual meetings au physical.

Mfano kuna lugha za kisheria, kuna lugha za kibiashara, kuna lugha za kiuchumi n.k discussion kama ile lazima mtu awe na element of law na business.

Pia nimeshangaa hata body expression hazikuwa nzuri, ni rahisi kuonekana unadanganya, hujui, hujitambui n.k kuna muda professor alikuwa anatoboa karatasi kwa pen , mara afunue file unnecessarily n.k

Hivi tunaendaje kwenye case hizi bila hata rehearsal walau? Mambo ya nchi tunauliza maswali ambayo huoni yatasaidia nini!

Very embarrassing! Hili swala watu wanacheka lakini sio Issue ya kutaniana bali ni Issue ya kuibua mjadala uwezo wa watu wetu. Hii case nani anasimamia? Hawa watu wameandaliwa vipi? Hata kama ni case ya kushinda utashinda vipi namna hii?

Binafsi nimejisikia vibaya sana, ningekuwa na uwezo ningeifuta ile video maana inatuvua nguo tu.
Inaumiza sana na ni hatari hata Kwa usalama wa nchi...Tunaonekana hatuna tunachokiweza so hata kuingiliwa na kudanganywa itakuwa rahisi. Hivi nchi iliruhusuje watu kama hao kwenda huko bila kuwa scrutinized? Afadhali angekuwa mmoja tu ndiyo Yuko hivyo, karibu wote pale ilikuwa ni kama walichaguliwa wabovu kwenda huko....Daah hii kitu imetudhalilisha sana watanzania.
 
Profesa Mruma amepata pigo kubwa sana kwa umri wake; waliomtuma huko Duniani wamedhamiria adhalilishwe na lengo limetimia . Anaulizwa kwa fedheha " haya ndiyo unawafundisha wanafunzi wako wa UDSM?

Muuliza swali ni mtoto wake wa kumzaa. Kwanini tumeruhusu wasiojiweza watusimamie?

---
Winshear Gold Corp. Vs. United Republic of Tanzania (ICSID Case No. ARB/20/25).
Kesi hii ipo chini ya Rais Gabrielle Kaufmann Hohrer kutoka Uswizi.

Mashahidi wetu huko ni Prof. Mruma na Mwanasheria wa Serikali bwana Igenge.


---
Video 1: Profesa Mruma akihojiwa
View attachment 2698386

Video 2: Mkurugenzi wa Huduma za Sheria(Wizara ya Madini) Edwin Igenge akihojiwa na Robert Denison
View attachment 2698385

---
WASIFU WA PROFESA MRUMA

Dkt. Mruma ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye kwa sasa ni Profesa wa Jiolojia. Profesa Mruma kwa sasa anahudumu kama Kamishna wa Tume ya Madini nchini Tanzania.

Mwaka 2017 Hayati Rais Magufuli alimteua Prof. Abdulkarim Mruma kuwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Kuhifadhi Mafuta (TIPER)

Profesa Mruma alijizolea umaarufu 24 Mei, 2017 baada ya kuongoza Kamati maalum iliyondwa na Rais Magufuli kuchunguza mchanga ulio katika makontena yenye mchanga wa madini (makinikia) yaliyopo katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania

-
Dkt. Abdulkarim Hamisi Mruma Ph.D. M.Sc. B.Sc. ni Mkurugenzi wa Kujitegemea wa Tanzania Royalty Exploration Corporationration. Dkt Mruma ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako kwa sasa ni Profesa wa Jiolojia.

Masomo yake ya Uzamili yalijumuisha tafiti katika vyuo vikuu na taasisi za Serikali nchini Ujerumani, Ubelgiji, Zimbabwe na Ufini.

Ameandika ripoti za kiufundi kuhusu mada mbalimbali za kijiolojia na kuchangia katika majarida kadhaa ya kiufundi na yasiyo ya kiufundi juu ya anuwai ya masomo ya Jiolojia.

Orodha ya machapisho hayo ni pamoja na Jarida la UNESCO la Sayansi ya Ardhi ya Afrika na Jarida la Tanzania la Sayansi ya Dunia.

Mbali na majukumu yake ya kitaaluma, Dk. Mruma ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania nafasi ambayo ameitumikia tangu Oktoba 2004.

Pia anahudumu kama Mjumbe wa Bodi ya Chuo cha Sayansi za Ardhi cha Williamson Diamonds Limited cha Chuo Kikuu cha Dodoma na Shirika la Madini la Taifa la Tanzania mshirika wa ubia wa Kampuni ya Uboreshaji wa Mradi wa Buckreef Gold Mine.

Hiyo nafasi ilikuwa ya Professor Kabudi au hata mwanasheria mwingine Nguli.
sasa Sijui ilikuwaje akaenda Geologist?
Kimsingi mtaalam sio kazi yake kujibu masuala ya Kisera. Ningekuwa ni mimi wala singekubali kuhojiwa.....
 
Kwa, kuwa sote ni Watanzania Serikali wakati mwingine iombe hata backup kwa Kibatala au Tundu lisu
 
Back
Top Bottom