Mahakama ya Kisutu imewatia hatiani Viongozi wa CHADEMA na kuwahukumu kulipa faini ya Tsh. Milioni 350 au kwenda jela, Wapelekwa Segerea

Mahakama ya Kisutu imewatia hatiani Viongozi wa CHADEMA na kuwahukumu kulipa faini ya Tsh. Milioni 350 au kwenda jela, Wapelekwa Segerea

Watagombea vizuri tu!Sina muda wa kukuelezea ila elewa aina ya hukumu iliyotoka haiwazuii!
 
Hii faini inalipika lakini italipwaje leo na muda wa kazi umekwisha?

Ndo kusema watakwenda jela hadi kesho?

Na ni nini athari za hukumu hii kisiasa kwa wote waliokutwa na hatia iwe wamelipa faini au kufungwa jela?
 
Mchumia Rungu,
Wanaifurahia kwa kuwa makosa yalikuwa makubwa. Hakimu angeweza kusema wafungwe jela na kulipa faini...Sasa hakimu ametoa option. Hi ni hukumu nzuri kwa maoni yangu kama layman wa sheria
Naongelea uonezi unaofanywa dhidi ya upinzani na viongozi hawaamui wafuasi tufanyeje kwa uonezi huo.

Habari ya makosa makubwa unaitoa wapi kama unafahamu chimbuko la kesi hii? Nakerwa kwa ujumla na utawala wa sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Viongozi wakihukumiwa, wanachama na wafuasi wanachanga. Je, wafuasi na wanachama wakihukumiwa viongozi wanachanga? Chezeeni biashara ya siasa. Zile za Lissu zilifikia kiasi gani?
Kama sio ujinga ni nini? Unauliuzia fedha zisizo kuhusu?
 
Masaa 11 replies 930+ what a msg to the authorities

Jr[emoji769]
 
Inamaana kuwa mtu usipotendewa haki ambayo ni halali yako hutakiwi kulalamika wala kudai haki yako, ukithubutu adhabu yako ni kufungwa jela.
 
IMG-20200310-WA0032.jpg
 
Naongelea uonezi unaofanywa dhidi ya upinzani na viongozi hawaamui wafuasi tufanyeje kwa uonezi huo.

Habari ya makosa makubwa unaitoa wapi kama unafahamu chimbuko la kesi hii? Nakerwa kwa ujumla na utawala wa sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Halafu eti kesho au keshokutwa utasikia kamuita Mh Mbowe Ikulu. Najua hawezi kumkatalia lkn ni aibu kubwa mno kwa hapa tulikofikia kama nchi moja.

Ukiwa Kiongozi Mkuu wa Nchi ukashindwa kuwaleta watu pamoja basi huna sifa ya kuendelea kuwa Kiongozi.

Hukumu ya leo imeichafua nchi yetu Kitaifa na Kimataifa. Mkurugenzi pamoja na Polisi wafanye yao mchana kweupee halafu uje uwahukumu waliokuwa wakidhulumiwa HAKI zao.

Kina Lissu wakiweka ukweli hadharani wankimbilia kusema wanaichafua nchi. Hivi kwa hukumu ya leo ni uchafu kiasi gani wameitia nchi yetu??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Viongozi wakihukumiwa, wanachama na wafuasi wanachanga. Je, wafuasi na wanachama wakihukumiwa viongozi wanachanga? Chezeeni biashara ya siasa. Zile za Lissu zilifikia kiasi gani?
Kiongozi analindwa kwa nguvu zote sababu anabeba dhamana ya nchi au kundi analoongoza. Kiongozi mzuri anakuwa ametoa nafsi yake kwa maslahi ya wanaoongozwa au nchi. Ndio maana kote duniani na katika historia, watu wametoa maisha yao kumlinda kiongozi wao.

Tundu Lissu amehatarisha maisha yake kwa kujitokeza kukosoa serikali ya kidhalimu na kikandamizaji kuwahi kutokea katika historia ya nchi yetu. Ndio maana watanzania kwa maelfu walijitokeza kumchangia. Uongozi bora ni janga, usilete mzaha hapa
 
Halaiser,
Haki imetendeka mkuu! Wachangie pesa wameshatoa account na simu ya kuchangia acha kelele wako Segerea wanaumia waonee huruma mkuu!!
 
Nimeleta uzi huu ili nipate michango ya wajuzi wa mambo ,
Hii ni baada ya hukumu ya viongozi wa chadema kutiwa hatiani leo hii hapa mahakama ya kisutu.
Najua watalipa faini ili kuepuka kifungo,je jinai itakuwa imefutika?ikizingatiwa tuna uchaguzi mkuu mwaka huu wa 2020 October,,
Kwa anayejua lolote achangie maoni
Jinai haifutiki kwakuwa faini nayo ni adhabu kama ilivyo kifungo, so they are criminals mpaka hapo Mahakama za juu zitakaposema vinginevyo.
 
Kiongozi analindwa kwa nguvu zote sababu anabeba dhamana ya nchi au kundi analoongoza. Kiongozi mzuri anakuwa ametoa nafsi yake kwa maslahi ya wanaoongozwa au nchi. Ndio maana kote duniani na katika historia, watu wametoa maisha yao kumlinda kiongozi wao.
Tundu Lissu amehatarisha maisha yake kwa kujitokeza kukosoa serikali ya kidhalimu na kikandamizaji kuwahi kutokea katika historia ya nchi yetu. Ndio maana watanzania kwa maelfu walijitokeza kumchangia. Uongozi bora ni janga, usilete mzaha hapa
Wakati alikuwa analialia kila siku hana pesa mpaka wazungu ndiyo wanamfadhiri nyinyi maneno tuui!
 
Back
Top Bottom