Mahakama ya Kisutu imewatia hatiani Viongozi wa CHADEMA na kuwahukumu kulipa faini ya Tsh. Milioni 350 au kwenda jela, Wapelekwa Segerea

Mahakama ya Kisutu imewatia hatiani Viongozi wa CHADEMA na kuwahukumu kulipa faini ya Tsh. Milioni 350 au kwenda jela, Wapelekwa Segerea

Kwamba wanasiasa hawapaswi kushtakiwa wala kuadhibiwa wakikosea. Haki itendeka Kama hawana hatia waachiwe na kama kweli walitenda makosa hayo waadhibiwe kama Watanzania wengine wanavyoadhibiwa wakikosea!
Unajua hawa CHADEMA ni mazuzu! Eti kwa vile ni kiongozi wa chama cha upinzani ukikosea usiguswe! Uliona wapi? Acha wawashikishe adabu!
 
vile watu wapo attention kufatilia hii hukumu unaweza kuachia "Cha Yusuph" humu kikanuka jukwaa zima na hakuna atakayekusemesha, wote watachukulia normal, macho, pua, mdomo, na masikio yote leo kisutu
 
Wakati Hakimu Mkazi Mfawidhi, Thomas Simba wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akisoma hukumu ya viongozi 12 wa Cahdema na mmoja wa CCM (Mashinji) wanaokabiliwa na mashktaka ya uchochezi, Jeshi la Polisi limetumia nguvu kuwafurusha wafuasi wa Chadema waliokuwa wamekusanyika mahakamani hapo kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo.

Polisi waliagiza wafuasi wote wa Chadema kuondoka kwenye viunga vya mahakama hiyo, lakini waliendelea kukaa wakidai hawajavunja sheria yoyote kwenda kusikiliza hukumu ya viongozi wao. Hata hivyo polisi walitoa amri ya kutawanyika kwa hiari vinginevyo watatumia nguvu. Wafuasi hao walikataa kutawanyika na kuimba kwa hisia "Mkitaka mtuue, mtuue"
_
Baadae polisi wenye silaha za moto, wakisindikizwa na mbwa waliwavamia wafuasi hao kwa kipigo na kuwatawanya wakati hukumu ikiendelea kusomwa ndani ya mahamkama hiyo.!
Polis kwa kuvunja sheria tushawazoea...wapinzani wapole mno
 
Mahakama ya Kisutu leo Machi10, inatarajia kutoa hukumu kwa Viongozi wa CHADEMA wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi Mahakamani hapo, Viongozi hao ni pamoja na Mwenyekiti CHADEMA, Freeman Mbowe, pia John Mnyika, Halima Mdee, Ester Bulaya, Ester Matiko, Heche, Msigwa na Mashinji.

Katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, vigogo hao wanakabiliwa na mashtaka 13, wakituhumiwa kwa uchochezi, katika kesi iliyoanza kusilikizwa Machi 7, 2018.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya Februari Mosi na 16, mwaka 2018, wakiwa Kinondoni jijini Dar es Salaam, kwa pamoja walikula njama na wengine ambao hawapo mahakamani kwa kutenda kosa la jinai na kuendelea na mkusanyiko isivyo halali na kusababisha chuki na uchochezi wa uasi.

UPDATE

4:30 Asubuhi : Hukumu yaahirishwa mpaka saa 7:30 mchana

Awali kesi hiyo ilipangwa kusomwa saa 4:30 wakati washtakiwa wakiwa ndani ya ukumbi, walifahamishwa kupitia kwa Wakili wao Peter Kibatala kuwa muda umesogezwa hadi saa 7:30 mchana.

7:30 Mchana : Hukumu ya kesi imeanza

Hukumu hiyo inasomwa kwenye Mahakama ya wazi na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba. Ulinzi umeimarishwa ndani na nje ya Mahakama.

Idadi kubwa ya wananchi na wafuasi wa chama hicho wamezuiwa kuingia mahakamani, kutakiwa kutoka nje. Baadhi yao wamesikika wakiimba nyimbo za kulituhumu Jeshi la Polisi kuwa CCM.

View attachment 1383035

Video: Taswira ya hali ilivyo ndani na nje ya viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
Tujulisheni kinachoendelea
 
Polis kwa kuvunja sheria tushawazoea...wapinzani wapole mno
[emoji16][emoji16][emoji16]
tapatalk_jpeg_1582962299761.jpeg
 
waliopo nje wanapoteza muda kwanza ukiwatizama ni aina ya watu waajabu ajabu hv ambao kimsingi hata uhakika wa kumiliki nyumba ni mdogo mno...Kamata wote weka segerea, mtu unashndwa kufanya kazi za msingi upate kipate unaenda kubishana na POLISI, hakuna wake wala waume na watoto wa hao viongozi hapo mahakamani nyie ndio mnajifanya wafia chama....
 
Ni wazi macho ma masikio ya watanzania yapo kisutu kwa sasa. kitakchoamriwa ama kitatoa taswira chanya ama hasi kwa taifa letu ngazi za kimataifa.
Huku kujidanganya hukuuuuuuu......
Kwa taarifa yako hizi habari zinaishia Hapo Mdaula kama siyo Chalinze zaidi zaidi tunazijua hapa hapa JF ambapo Wapiga kura hawazidi Milioni 1. Kama tunataka dolla Twendeni Vijijin tuache hizi ndoto za Mtandaoni tunapotezeana muda.
 
Mahakama ya Kisutu leo Machi10, inatarajia kutoa hukumu kwa Viongozi wa CHADEMA wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi Mahakamani hapo, Viongozi hao ni pamoja na Mwenyekiti CHADEMA, Freeman Mbowe, pia John Mnyika, Halima Mdee, Ester Bulaya, Ester Matiko, Heche, Msigwa na Mashinji.

Katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, vigogo hao wanakabiliwa na mashtaka 13, wakituhumiwa kwa uchochezi, katika kesi iliyoanza kusilikizwa Machi 7, 2018.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya Februari Mosi na 16, mwaka 2018, wakiwa Kinondoni jijini Dar es Salaam, kwa pamoja walikula njama na wengine ambao hawapo mahakamani kwa kutenda kosa la jinai na kuendelea na mkusanyiko isivyo halali na kusababisha chuki na uchochezi wa uasi.

UPDATE

4:30 Asubuhi : Hukumu yaahirishwa mpaka saa 7:30 mchana

Awali kesi hiyo ilipangwa kusomwa saa 4:30 wakati washtakiwa wakiwa ndani ya ukumbi, walifahamishwa kupitia kwa Wakili wao Peter Kibatala kuwa muda umesogezwa hadi saa 7:30 mchana.

7:30 Mchana : Hukumu ya kesi imeanza

Hukumu hiyo inasomwa kwenye Mahakama ya wazi na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba. Ulinzi umeimarishwa ndani na nje ya Mahakama.

Idadi kubwa ya wananchi na wafuasi wa chama hicho wamezuiwa kuingia mahakamani, kutakiwa kutoka nje. Waliamua kukaa chini karibu na mlango mkuu wa kuingia kwenye jengo la Mahakama mpaka Polisi walipowafukuza kwa vitisho. Baadhi yao wamesikika wakiimba nyimbo za kulituhumu Jeshi la Polisi kuwa CCM.

View attachment 1383035

Video: Taswira ya hali ilivyo ndani na nje ya viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
Uzi ume stuck huu. tupatie updates mkuu
 
hakuna mwenye kosa ni kuwaonea tu,,,,... persecution
Umefatilia mwenendo wa kesi, umesikiliza mashahidi, umesikiliza utetezi, au umeamua kujitia ujuaji.Nyie ni wanademockrasia acheni kuishinikiza Mahakama iamue mnavyotaka. Subirini Hukumu na maamuzi yatakayotoka yaheshimiwe na asiyeridhika utaratibu wa kisheria ufuatwe!
 
Back
Top Bottom