Njama mlizompangia eti ashindwe uchaguzi ili afungwe gerezani kwa kesi hizo za uchochezi, akishafungwa Kamati Ya Maadili Ya Mawakili imfutie uwanachama wake (Permanent Removal) kwa kigezo amefanya kosa la jinai.
Ila kitu ambacho hamjafikiria, mungu mkubwa atakapo wadhalilisha na kumpa ushindi wa Urais. Halafu anakutana na Kinga Ya Kikatiba (Immune) ya kutoshtakiwa pamoja na kesi zote dhidi yake kufutwa kwa kinga hio. Mungu mkubwa sana.
Fatma Karume anaapishwa kuwa Waziri Wa Sheria, anaanza kufanya kazi na Wakili Mkuu Wa Serikali (Hapa atakuwa Kibatala) kuwashughulikia mafisadi wote wa CCM kimahakama. Mpaka wale walio dhulumu wananchi Kagera zile eka 25,000 za ardhi na kujimilikisha na wale waliotumia madaraka yao vibaya kwa kutumia silaha za moto kuvamia ofisi za watu na kuwabambikizia kesi wafanyabiashara/raia/waandishi wa habari na kutoa roho za watu bila hatia.
Kweli mungu mwema sana.