Mahakama ya Mafisadi imekufa kifo cha kawaida?

Hahahaha rejea sababu zilizofamya ikajengwa. Hakuna kesi ya maana hata moja ukiacha ya Yule Mkurugenzi sijui wa Halmashauri gani

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa hiyo hao watuhumiwa wanaopelekwa mahakamani kwa basi na pick up za magereza ni maigizo? Hao majaji na makarani wanakuja kufanyaje? Kila siku mabenchi ya mahakama yanajaa. Maana yake ni kwamba Mahakama inafanya kazi
 

Siyo kila kesi inaripotiwa kwenye media. Waandishi nao wanaangalia habari ya kuuza magazeti. Kama ulitarajia kusikia taarifa za kesi zote mahakamani, basi unajidanganya
 
Walioifungua. Wenyewe NI mafisad unategemea nini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mahakama ya Mafisadi ipo, na jengo lake lipo nyuma ya ofisi za TCRA, na ndani ya geti la Law School. Kila siku watuhumiwa wanaletwa hapa na majaji wanakuja. Acheni kusambaza uongo eti hii mahakama haifanyi kazi
Unaweza kututajia mafisadi wazito hata wawili tu waliofikishwa kwenye mahakama hiyo ? usije ukasema Ndama mtoto wa ng'ombe tu
 
Aliyelengwa na walengwa wake wamekubali terms na conditions. Na kwa sasa wamerejea.
Mabilioni yaliyopotea yatarejea kwa kufunga mikanda zaidi


Shida imebaki kwa walalahoi. Wagombanapo mafahali wawili nyasi ndio huumia.
 
S
Hakuna Rais yoyote duniani anayejiita au kuitwa Rais Doctor flani.... acheni ushamba na kumkweza jiwe bila sababu. Hata Obama ni Doctor lakini aliitwa president Obama. Mnaboa...
Serkali yote imejaa Maprofesa na Madaktari dunia nzima haina nchi nyingine yenye wasoml kama Tz lakini ujuzi wao mashaka tupu. Process ndio mwalimu was Daktari na shahada zote tatu zinafundishwa kwa Kingereza, inakuwaje wasomi hawa lugha hiyo inawapiga chenga?
 
Kifo cha mende
 
Hahaha mnasahau sana, Dr.Harrison Mwakyembe alikuwa mpinzani wa Lowasa tangu bunge la Sitta, kumbukeni Lowasa akuwa waziri mkuu Dr.Mwakyembe aliishupalia hoja ya Richmond ikamng'oa Lowasa kwenye uwaziri mkuu, sasa akiwa mpinzani wa Lowassa alimshawishi Magufuli afungue mahakama ya mafisadi kama ilivyo mahakama ya Biashara. Magufuli akampa wizara ya sheria na katiba na mwakwembe akaiasisi mahakama hii. Sasa hawana wa kumshitaki kwasababu mafisadi yako ccm, na Dr.Slaa anayafahamu lakini naye yuko ccm. Unadhani watamshitaki nani wamuache nani?! Kashifa zote ziko kwao, Green, meremeta, EPA, Tegeta escrow, sukita, na hata Richmond.
Mwakyembe hata yeye akiulizwa leo mantiki ya uanzishwaji wa mahakama hiyo na uhaba wa washitakiwa anaweza kuomba ifutwe. Kwasababu alimtargert Lowassa tu, sasa yuko kwao jiulize mahakama inamaana gani ikiwa hashitakiwi na hakushitakiwa wamebaki kuokoteza watuhumiwa na wanashindwa kuwatia hatihani.
Wampe mwakyembe u-DPP au akabidhiwe TAKUKURU tuone atawatoa wapi mafisadi kama alivyoshadidia kuanzishwa kwa mahakama hiyo?!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haa umenikumbusha mahakama ya Sokwe na Nyani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…