Mahakama ya Rufaani yabatilisha hukumu ya kifo mauaji ya 'Super Sami', Kibatala asema haki imetendeka

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Mahakama ya Rufani nchini Tanzania imewaachia huru waliokuwa wamehukumiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa tuhuma za kumuua mfanyabiashara mashuhuri wa Mwanza, Samwel Mwang’onda, maarufu kama 'Super Sami'.

Desemba 2024, jopo la majaji wa Mahakama ya Rufani lilitengua hukumu hiyo ya awali ya Mahakama Kuu baada ya kubaini kuwepo kwa mapungufu makubwa ya kisheria na ukosefu wa ushahidi wa kutosha wa kuwatia hatiani pasipo kuacha shaka yoyote.

Mchakato huo wa kisheria ulioendeshwa na mawakili wa utetezi wakiongozwa na Wakili Peter Kibatala, ulihitimishwa kwa amri ya kuachiliwa huru mara moja kwa warufani hao. Akizungumzia maamuzi hayo, Wakili Kibatala alieleza kuridhishwa kwake na uamuzi huo akisisitiza kuwa haki imetendeka na kwamba Mahakama ya Rufani imethibitisha kuwa kimbilio la mwisho la haki pale ushahidi wa upande wa mashtaka unapokuwa na shaka.

Haya
 
Back
Top Bottom