Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Karoge tu mkuu
Dah wewe miezi miwili tu umechoka
Kuna watu wana miaka miwili Sasa Bado hawapata
We mweleze mganga tu unataka pesa zako kutoka mahakamani basi mengine atajua yyTukamroge nani sasa?
We mweleze mganga tu unataka pesa zako kutoka mahakamani basi mengine atajua yy
Kesi yako iko mahakama ya Wilaya au ilianzia mahakama ya Mwanzo? Unaweza kufika kwa hakimu Mfawidhi hapo mahakama ya Wilaya na ukamweleza malalamiko yako. Pia unaweza kufika mahakam ya Rufaa kitengo cha mirathi unawambia concern yako. Wao wanaweza kukuelekeza namna ya kufikisha malalamiko yakoHilo linajulikana.
Ndio maana nimeleta humu ili na wengine wajue mahakama zilivyo sehemu za ovyo
Very sad, wengi wao wanaotoa ushauri hapa wanashauri utoe rushwa!
Kwa mtindo huu tusahau kutokomeza rushwa!Watu hawajui hata haki zao.
Mtu anakupa ushauri kabisa katoe rushwa
We endelea kusikiliza hao waganga wa instagram ila usiniulize mganga mzur utampata wapi maana sifanyi promo za waganga mimiUmetisha mkuu.mganga mwenyewe tapeli nae anataka malipo
Hapo ndio utajua hujui kwa Tanzania eneo la mahakama rushwa imehalalishwa. Mfano karani anakuambia eti mheshimiwa hajanywa chai!! Hakuna msaada popote Nakushauri wape hela ya chai na maandazi tu wamalize shauri lakoKutoa rushwa ni kuondoa tatizo ama kuongeza tatizo.
Kiukweli wafanyakazi wa mahakama wanaifanya mahakama ionekane ni sehemu ya ovyo sana. Usumbufu mwingi sana
Mkuu, Naomba kukuuliza kama nakala ya hukumu ya mirathi mlishapewa?
Kama malipo yote ya marehemu yalishaingizwa kwenye account ya mahakama, Na kama ni kweli wategemezi mlifata taratibu zote ikiwemo kujaza vendor form, Basi tatizo lipo kwa Muhasibu wa mahakama.
Kinachokosekana ni uwazi wa kupewa taarifa, Mimi ni Muhasibu wa mahakama pia Kuna taratibu za kiofisi ambazo lazima ziwe kwa maandishi,mfano pesa zikishaingizwa Judiciary Mirathi Account lazima ziwe approved kutoka makao makuu then mh hakimu aidhinishe malipo ndo mlipwe sio kitu Cha siku moja ni process kidogo.
Ninachokiona ni ww kuwa na jazba au kutokupewa taarifa kamili na hao wahusika. Kwa situation uliyofikia haikupaswa uwe mtu wa hasira jitahidi kumfanya uyo Muhasibu kuwa rafiki ili akupe taarifa sahihi kwa wakati. Jishushe ongea nao kirafiki uone kama hawatokuhudumia vizuri.
Kama imeshindikana unaweza pia kuwasilisha malalamiko yako kwa msajili wa mahakama au hakimu husika kwa hatua zaidi. Kumbuka malalamiko yawe kwa njia ya maandishi sio mdomo.
Mahakama ya Tanzania kwa sasa imejitahidi kufanya maboresho hasa wakati huu ambao huduma zote zitahamia kwenye mfumo wa tehama.
Ni vyema ukawepo hapo mahakamani siku ya kilele Cha wiki ya sheria jumanne ya tar 2 February ili utoe kero yako hapo hapo na utasikilizwa.
Ndo Mana nasema usiwe na jazba, Muhasibu hawezi kulipa kama anatoa pesa mfukoni mwake, Kuna taratibu za malipo.Nimekuelewa sana. Ukisoma vizuri uzi wangu nimeilalamikia idara ya uhasibu kwa majibu yao mepesi kama ya kusema mtu amepata msiba .
Nakala ya hukumu ipo, kila kitu kipo.
Hakuna sehemu nilipomlalamikia hakimu.
Nimelalamikia idara ya kulipa pesa tu.
Na hata ukisoma wachangiaji wengine na wao wamelalamika kwamba ni tabia ya wahasibu kutolipa mpaka wapewe pesa za rushwa.. wanaita push money.
Yaani mtu hapewi haki yake mpaka push money.
Why utumie zaidi ya miezi mitatu ama sita kumlipa mtu aliyekamilisha kila kitu kwa wakati. Mbona mahakimu hawana shida siku hizi
Ndo Mana nasema usiwe na jazba, Muhasibu hawezi kulipa kama anatoa pesa mfukoni mwake, Kuna taratibu za malipo.
Unachotakiwa ni kujenga ukaribu nae ili awe anakupa taarifa sahihi za hatua alizofikia.
Sio kwamba anahitaji rushwa, Hapana isipokuwa mazingira na taratibu za kazi wakati mwingine inaonekana kama muhusika anahitaji rushwa wakati si kweli.
Kama vipi tengenezeni mazingira ya kuwalipua,maana hapo wanachotaka ni rushwa tu hakuna jipya.Mahakama ya wilaya ya temeke ina wafanyakazi wa ajabu sana.
Tumekamilisha taratibu zote za mirathi za mzee wetu.
Bank alizokuwa anatumia marehemu, mifuko ya hifadhi ya jamii psssf na mobile money zote zimetuma pesa kwenda kwenye account ya mahakama toka october 2021
Barua ya mchanganuo wa mgao wa mirathi imepelekwa toka November mwanzoni. Na taratibu zote za zikafanyika kama kujaza vendor form na nyaraka za kibenk za warithi wa marehemu.
Ila mpaka leo mahakama haijawalipa hao warithi.
Msimamizi wa mirathi akienda kufatilia anaambiwa subiri. Kuna wafanyakazi wa idara ya uhasibu wamepatwa na msiba wa wazazi wao. Ukaguzi bado hawajaumaliza.
Siku nyingine wakienda wanaambiwa December kuna sikukuu nyingi sasa walipaji hawakuwa kazini.
Akienda kuulizia tena anaambiwa mlipaji ameenda likizo fupi.
Miezi zaidi ya miwili ni longo longo tu
Kweli mfanyakazi akipata msiba na ofisi yake mahakamani inasimama kufanya kazi zake mpaka arudi ?
Kama vipi tengenezeni mazingira ya kuwalipua,maana hapo wanachotaka ni rushwa tu hakuna jipya.
Msimamiz wa mirathi ametoa 2 weeks za ziada Wasipolipa tunampanga jamaa yetu wa takukuru yeye atatulekeza cha kufanya ili liwe fundisho
sheikh mkono mtupu haulambwi.
Hao ni mbuzi wanaofata maelekezo ya kula kwa kamba.
Itisha press conference mbele ya ofisi yao uzungumzie hilo swala.. kesho yake asubuhi utalipwa mpunga wako…