Mahakama ya Temeke wanasumbua kulipa pesa za Mirathi bila hoja za msingi

Polee MKUU.. endelea kuvumilia.. umepanga kuifanyia nini? Mgao wako wa MIRATHI
 
Mkuu umeongea kwa ukweli kabisa ILA tuangalie upande wa pili wa coin ,hayo uliyoyashauri hapo juu yanawezekana?ni kweli wadai wakifuata ushauri huu watafanikiwa?maana end of the day watarudishwa kule kule wanakusumbuliwa;wakuu humu ndani tuwe na WILL ili kuepusha kuacha mess tunapokua tumekufa,why warithi wasipate mafao yao STRAIGHT kutoka kwenye mifuko ?why fedha hii inapelekwa pale Temeke?tafadhali naomba ushauri may be i mis something here.
 
Ni kweli Kuna haja ya watu kuwa na utaratibu wa kuandaa Will. Tatizo unajua sio Will pekee Ila shida huwa inakuja kwa hao warithi au wasimamizi wa Mirathi na ndipo mahakam huamua kusimama kama msimamizi baada ya kuona kuna mtafaruku kwenye kugawa hiyo mali ya marehemu ikiwemo pesa.

Endapo itatokea mtafaruku kwenye shauri la kuomba Mirathi Mahakama Ina uwezo wa kutafuta msimamizi yenyewe na ikampa majukumu ya kusimamia mgawanyo wa mali na kupeleka mrejesho wa namna mgao ulivyofanyika.

Pia Mahakama inaweza kuamua kugawa hizo mali yenyewe kama itaona ni sawa kufanya hivyo ili kuondoa migongano baina ya warithi na mara nyingi ni Kama hakuna mali nyingi au ni ishu inahusisha mgao tu was pesa jambo ambalo Mahakama inaweza kusimamia mgawanyo huo kwa wepesi na haraka.

Pia Mahakama inaweza kumteua RITA kusimamia mgawanyo wa mali ya Mirathi au kurithi pia kama pesa au mali haijulikani nani ni mrithi maana kuna watu wengine wanafariki na wanaacha mali bila kuacha Will na anakuwa ameishi hana ndugu Wala mtoto. Hii hutokea sana kwa wahamiaji.

Sasa kujibu swali lako la kwa nini pesa imeamuriwa ipelekwa Mahakamani wakagawiwe pale nadhani nitakuwa nimekujibu kulingana na maelezo yangu hapo juu.

Japo sina facts zilizopelekea Mahakama kuamua kutoa order ya pesa zipelekwe na kugawiwa Mahakamani, kutokana na mazingira ambayo sheria imetamka basi ni wazi kwamba kuna uwezekano hao ndugu wamekuwa wakivutana kuhusu mgao wa pesa na Mahakama inaweza kuwa imeona kwamba kuna wajanja wanataka wawazidi wenzao either sababu ni pesa basi wawape kidogo au wasiwape kabisa na kutoa visingizio kama vile pesa haijatoka nk.

Tatizo kwetu waafrika sio tu kuacha Will,, wengine Will unakuwepo na bado wanataka kumdhulumu mrithi halali, tamaa huwa inasumbua. Unakuta mtu ameamua kumrithiisha mali mtu fulani mali ambayo labda Ina thamani kubwa hapo ndipo shida huanza, jamii inatakiwa kubadilika.

Unakuta mume au mke kafariki lakini anatokea baba mdogo huko anaanza kutaka kumdhulumu mjane au mgane. Hii ipo sana kwenye jamii au unakuta msimamizi wa Mirathi huwa anahisi ndio kama amepewa mali yeye wakati yeye anasimamia mgawanyo tu na anaweza asiwe sehemu ya warithi Ila nao huwa wanaanza kuwa na tamaa.
 
Wanataka hela hao mzee,hii ni bongolala
 
 

Kuwe na will ama kusiwe na will Hela yoyote ya mirathi lazima ipelekwe account ya mahakama. Iwe mirathi ina amani ama ina ugomvi. Huo ni utaratibu wa lazima.

Hakuna mirathi ambayo hela ya marehemu haipiti mahakamani hata kama marehem ana mtoto mmoja tu
 
 
Mkuu hilo linawezekanaje? PSSSF huwa wanaweka pesa moja kwa moja kwenye akaunti za wanufaika kuendana na mgawanyo wa mali kama unavyokuwa kwenye form namba VI inayopatikana mahakamani. HAKUNA namna yoyote inawezekana PSSSF wakatuma pesa kwenye akaunti ya mahakama.
Kama marehemu alikuwa na madeni basi kuna utaratibu wa kuyalipa moja kwa moja.
Kuhusu Bank na Mobile money sijui inakuwaje ila kwa PSSSF haiwezekani pesa kutumwa kwenye akaunti ya mahakama. Hata kama mnufaika amezaliwa leo basi itabidi afunguliwe akaunti yake na hela itatumwa huko.
 
 
Mc
Pesa kuwa approved ni zoezi la miezi mingapi ikishaingizwa Mirathi account?

Kama shauri la Mirathi lilifunguliwa mahakama ya mwanzo na hatua zote zimatamatika,msimamizi anatakiwa kufuatilia mahakama ngazi ipi kujua kinachoendelea?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…