Mahakama yaamuru Cyprian Musiba kulipa faini ya Tsh. bilioni 6 kwa kumchafua Bernard Membe

Mahakama yaamuru Cyprian Musiba kulipa faini ya Tsh. bilioni 6 kwa kumchafua Bernard Membe

Kwa hiyo huyu mwamba kwa sasa ana madeni yapatayo 13bilion! Manake kule kuna shangazi Fatuma alipata tuzo ya 7b na huku Membe 6b. Nadhani sasa Musiba ni raia anayedaiwa madeni makubwa kuliko raia yeyote hapa nchini na anastahili sifa ya Highly Indebted Poor Person (HIPC).
Ukijumlisha na lile deni letu la taifa ambalo kila mtanzania anadaiwa milioni na kitu hivi, itakua shilingi ngapi kwa musiba anayodaiwa?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata akiweka rehani kila anachomiliki ikiwemo tupu yake ya nyuma hatopata hiyo pesa kulipa.
Hili ni fundisho kubwa sana la kutomtegemea sana mwanadamu mwenzio katika kudhalilisha wengine. Mungu ni wa wote, anaweza chelewa kutoa hukumu lakini abadan haachi kutenda haki.
 
Hivi asipo lipa inakuwaje yaani? Lwa mfano nimeamuliwa kukulipa kiasi fulani cha pesa na mahakama lakini nikashindwa au kwa makusudi nikagoma kukulipa. What next?
 
Musiba kapata Msiba Bible inasema Ole wake amtegemeae mwanadadamu na je akishindwa kulipa mahakama imefafanua anafungwa miaka mingapi
 
huyu jamaa alijisahau sana, alijua nchi haina sheria yoyote ile, nashukuru tu wazee wastaafu wao wameamua kubakia kimya. Watu hawa ndiyo wanaweza kuuza hata siri za nchi kwa ujira, hawaaminiki hata kidogo ukirusha mfupa tu basi akili yote inahamia tumboni.
 
Magufuli angekuwa hai wangemtia musiba hatiani?
 
Back
Top Bottom