Mahakama yaitaka CHADEMA kukabidhi nyaraka za Chama kwa Saidi na wenzake ndani ya siku 14

Mahakama yaitaka CHADEMA kukabidhi nyaraka za Chama kwa Saidi na wenzake ndani ya siku 14

The Supreme Conqueror

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2017
Posts
609
Reaction score
1,584
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, leo Jumatatu (29.09.2025) imetoa uamuzi mdogo katika kesi namba 8322/2025 iliyofunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Said Issa Mohamed na wenzake wawili dhidi ya Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa chama hicho.

Waleta maombi walikuwa wameiomba Mahakama kuamuru wapatiwe nyaraka mbalimbali za chama hicho kuanzia mwaka 2019 hadi 2024, ikiwemo muhtasari na ajenda za vikao vya Bodi ya Wadhamini na Kamati Kuu, pamoja na taarifa za mali na fedha za chama. Walidai kuwa nyaraka hizo zitawasaidia kuendeleza hoja zao katika kesi ya msingi.

Upande wa CHADEMA kupitia mawakili wake ulipinga ombi hilo, ukidai kuwa Said Issa hakuwa na uhalali wa kuwasilisha maombi hayo kwa kuwa hana tena nafasi ya uongozi ndani ya chama, na kwamba nyaraka alizoziomba tayari anazijua kutokana na nafasi yake ya uongozi wa muda mrefu.

Hata hivyo, Jaji Hamidu Mwanga ameridhia sehemu ya maombi hayo. Ameamuru CHADEMA kuwasilisha tamko la mali za chama, taarifa za fedha za Benki ya NBC pamoja na ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa kipindi cha miaka mitano, kuanzia 2019 hadi 2024. Mahakama imekataa maombi ya nyaraka nyingine, ikisema hayakuainishwa kwa ufasaha na kwamba baadhi ya taarifa za vikao haziwezi kuwekwa hadharani.

Kwa mujibu wa uamuzi huo, Chadema imetakiwa kuwasilisha nyaraka hizo ndani ya siku 14, huku waleta maombi wakipewa siku 9 za kuzichambua kabla ya kesi ya msingi kuendelea Oktoba 30, 2025.

Katika kesi hiyo ya msingi, Said Issa na wenzake wanaituhumu Chadema kwa kutenga Zanzibar katika shughuli zake, kutokuwepo kwa usawa kwenye mgawanyo wa mali na fedha, pamoja na kutoa kauli zinazodaiwa kuchochea udini na ubaguzi wa kijinsia.

 
Mtu alikuwa kiongozi miaka 15 kweli ulaji wao umezibwa
 
Hiki chama kama dhahabu, kinapita kwenye moto mkali sana.
Mbowe ndiyo sababu alikigeuza chama kuwa danguro na sakosi pia kwenye msafara wa kupigania haki ogopa sana kuwashirikisha waislamu
 
Na bado kiko imara miezi 3 sasa inaenda minne hakijafanya public rally yoyote ila bado kinaaminika na kinawanyima majizi na mafisadi amani ya moyo.
Mkuu 'Matrix19',moja ya hatari kubwa kabisa inayo kikabili chama ni Samia kubaki madarakani miaka mitano ijayo.

CHADEMA Mpya, kama ilivyo chini ya uongozi wa sasa; kamwe Samia hawezi kuvumilia hali hiyo.
Nionavyo; kesi kama hii iliyo undwa mahsusi kuifunga CHADEMA itaendelea muda wote huo; au kutazushwa mbinu nyingi nyingine za kuimaliza CHADEMA.

Samia hana subira, uwezo hata uvumilivu wa kutawala nchi kukiwa na chama ambacho hana uwezo wa kuhonga au kuwaweka karibu viongozi wake kama alivyo fanya na Mbowe.

Bahati ya CHADEMA itakuwa ni moja tu, Samia na Genge lake wasipewe nafasi ya kubaki kwenye madaraka baada ya Oktoba 29.
 
Back
Top Bottom