feyzal
JF-Expert Member
- Apr 20, 2016
- 7,683
- 15,128
Kipindi hiki nadhani alikua na mzungu na ndo alikua ametoka wasafiUnakopa hela ya biashara unaenda kumtrombea Kajala.pumbavuu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kipindi hiki nadhani alikua na mzungu na ndo alikua ametoka wasafiUnakopa hela ya biashara unaenda kumtrombea Kajala.pumbavuu
Si kuna kipindi Dk. Bashiru alisema ccm haitatumia tena wasanii, itatumia bendi yake ya TOT.Atapata SHOW moja tu kabambe ya CCM ya kumnadi mama katika kampeni za Urais...hapo atapata mara 3 ya hizo pesa
Kwani kuno Shido ???
Uko sahihi. Hiki kibibi kisivyo na simile kinaweza kumlipia.Mheshimiwa atamlipia
Na hapa ni unatumia kishikwambi cha serikali kuombea huu mkopo 😅Upuuzi kabisa mtu unakuta anatamba eti kazi ya ualimu ni kazi ya Laana,Sasa tangu nizaliwe sijawahi sikia mwalimu kafikishwa mahakamani Kwa kushindwa kulipa mkopo wa benki au kauziwa assets zake Kwa kushindwa kurejesha mikopo ya benki.
Sasa Harmonize kashindwa kulipa M 100,Huu upuuzi,Sitaicha kazi ya ualimu kamwe,hapa navuta Muda nije niende nikavute mpunga M 32 nione mtu ananilaumu Kwa kutegemea mikopo , nijivinjari zaidi.Asante Mungu kwa kazi ya ualimu,Kiufupi huwezi toboa maisha bila kukopa ,kama unakopesheka kopa
Sasa mleta mada hizi nakala si kashaweka huko juu?!?! We vipi?!?! Fungua uzi wako acha ushamba!
Nifah kumbe ni mtu wa mahakamani!Nimekukubali
View attachment 3072826
View attachment 3072827
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Rajabu Abdukahali Ibrahim almaarufu Harmonize ametiwa hatiani na mahakama kuu divisheni ya biashara tarehe 2 mwezi huu wa 8 kwa kushindwa kulipa kikamilifu mkopo wa kiasi cha shilingi milioni 300 alizokopa katika benki ya CRDB mwaka 2019.
Mkopo huo uliokuwa na riba ya 18% ulielezwa na msanii huyo kama uwekezaji kwenye shughuli zake za kimuziki ikiwemo studio ya kisasa ya uzalishaji wa muziki na video, ulikuwa ulipwe ndani ya miezi 36 (miaka mitatu).
Na ulikuwa mkopo wa awamu mbili, ya kwanza ikiwa milioni 100 kisha awamu ya pili milioni 200 ambazo awamu zote alipewa na benki hiyo mwaka huohuo wa 2019.
Moja ya makubaliano ilikuwa (Harmonize) kufungua akaunti ya kibiashara katika benki hiyo kisha kuiweka milioni 100 na kuifanya akaunti hiyo kuwa akaunti yake kuu katika shughuli zake za kiabishara, takwa hilo pamoja na mengine ikiwemo marejesho ya mkopo kwa kila mwezi yalishindwa kufikiwa na Harmonize.
Baada ya usumbufu uliopitiliza wa ulipaji wa mkopo huo kutoka kwa Harmonize, CRDB walifikia uamuzi wa kwenda mahakamani. Uamuzi huo ambao mahakama ilitoa wito mara kadhaa kwa Harmonize, lakini Harmonize hakufika mahakamani. Na hata mahakama ilipomuomba kutoa maelezo (Written statement of defence WSD) hakufanya hivyo.
CRDB waliendelea kumkumbusha Harmonize kulipa mkopo kila mara na kila njia hadi zikiwemo jumbe za WhatsApp, mwanzoni mwa mwaka 2022 Harmonize aliandika barua kwenda tawi la benki hiyo lililopo Mlimani City akiomba kulipa marejesho kwa kiasi cha 3.3 milioni badala ya utaratibu uliowekwa wa 10.8 milioni kila mwezi wakati huo deni la mkopo likiwa 109,731,733.46/= CRDB walikubali ombi lake hilo ila akitakiwa kulipa 3.9 milioni badala ya 3.3 milioni aliyokuwa ameomba.
Harmonize alifanikiwa kupunguza deni hilo hadi kufikia kiasi cha 103,185,755. Baada ya hapo hakulipa tena hadi kufikia hukumu iliyotolewa 2/08/2024 ambapo msanii huyo ametakiwa kulipa kiasi chote kilichobaki katika mkopo, gharama za kesi na fidia ya milioni 10 na nyinginezo kama mahakama ilivyoona.
Chanzo changu na mimi,
Nifah.
Hata ukikaa nayo siku hizi uki google kesi zote unazipata online. Ww andika tu Crdb v Harmonise mzigo huoooNakala ya hukumu ninayo, ila sitoiweka hapa.
Hawa wasanii wanapenda misifa ya kijinga sana,Huenda kazi ilimlipa yeye katanuliaIla Harmonize ni mtata kwenye kulipa madeni, nakumbuka miaka kadhaa hapo nyuma amewahi kukimbia deni la kodi ya nyumba aliyokuwa akiishi huko Mbezi Beach kwa Mchagga mmoja kama 150 Milioni hivi.
Ningependa ulete za Ommy dimpoz nae... Maana anawaweka roho juu sana vijana wetu. Usikute hata gari hana yule mshamba 😂Ninazo nyingi sana, mchawi muda tu sipati wa kuandika.
Tujifunze sio kila mwenye muonekano wa maisha mazuri ana amaniWengine tukamuonea wivu Kajala kumbe!