Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nafurahi kumuona Mwalimu wangu C.K.K Morris katika ubora wake!
View attachment 3072826
View attachment 3072827
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Rajabu Abdukahali Ibrahim almaarufu Harmonize ametiwa hatiani na mahakama kuu divisheni ya biashara tarehe 2 mwezi huu wa 8 kwa kushindwa kulipa kikamilifu mkopo wa kiasi cha shilingi milioni 300 alizokopa katika benki ya CRDB mwaka 2019.
Mkopo huo uliokuwa na riba ya 18% ulielezwa na msanii huyo kama uwekezaji kwenye shughuli zake za kimuziki ikiwemo studio ya kisasa ya uzalishaji wa muziki na video, ulikuwa ulipwe ndani ya miezi 36 (miaka mitatu).
Na ulikuwa mkopo wa awamu mbili, ya kwanza ikiwa milioni 100 kisha awamu ya pili milioni 200 ambazo awamu zote alipewa na benki hiyo mwaka huohuo wa 2019.
Moja ya makubaliano ilikuwa (Harmonize) kufungua akaunti ya kibiashara katika benki hiyo kisha kuiweka milioni 100 na kuifanya akaunti hiyo kuwa akaunti yake kuu katika shughuli zake za kiabishara, takwa hilo pamoja na mengine ikiwemo marejesho ya mkopo kwa kila mwezi yalishindwa kufikiwa na Harmonize.
Baada ya usumbufu uliopitiliza wa ulipaji wa mkopo huo kutoka kwa Harmonize, CRDB walifikia uamuzi wa kwenda mahakamani. Uamuzi huo ambao mahakama ilitoa wito mara kadhaa kwa Harmonize, lakini Harmonize hakufika mahakamani. Na hata mahakama ilipomuomba kutoa maelezo (Written statement of defence WSD) hakufanya hivyo.
CRDB waliendelea kumkumbusha Harmonize kulipa mkopo kila mara na kila njia hadi zikiwemo jumbe za WhatsApp, mwanzoni mwa mwaka 2022 Harmonize aliandika barua kwenda tawi la benki hiyo lililopo Mlimani City akiomba kulipa marejesho kwa kiasi cha 3.3 milioni badala ya utaratibu uliowekwa wa 10.8 milioni kila mwezi wakati huo deni la mkopo likiwa 109,731,733.46/= CRDB walikubali ombi lake hilo ila akitakiwa kulipa 3.9 milioni badala ya 3.3 milioni aliyokuwa ameomba.
Harmonize alifanikiwa kupunguza deni hilo hadi kufikia kiasi cha 103,185,755. Baada ya hapo hakulipa tena hadi kufikia hukumu iliyotolewa 2/08/2024 ambapo msanii huyo ametakiwa kulipa kiasi chote kilichobaki katika mkopo, gharama za kesi na fidia ya milioni 10 na nyinginezo kama mahakama ilivyoona.
Chanzo changu na mimi,
Nifah.
Naskia anapenda sana vijana...😜Mheshimiwa atamlipia
Gubu umenilisha maneno ww. Mimi nakueleza kitu ambacho kila siku nadeal nachoImeshawekwa acha gubu.
Mkuu shukrani sana kunitambua kawaida tu.Nafurahi kumuona Mwalimu wangu C.K.K Morris katika ubora wake!
Mama pesa anazo leo yanga tunamdai milioni 20Mbona wengi mnasema mama atalipa? Huyo mama ana pesa zisizokuwa na kaziza kulipia watu madeni tena makubwa ya mikopo?
Sio mtata ni anaishi juu ya uwezo wake lazima maji aite mma..Ila Harmonize ni mtata kwenye kulipa madeni, nakumbuka miaka kadhaa hapo nyuma amewahi kukimbia deni la kodi ya nyumba aliyokuwa akiishi huko Mbezi Beach kwa Mchagga mmoja kama 150 Milioni hivi.
Umejiunga JF lini? Hizo unazoona huko juu, bila mimi kutuma zisingepanda, mods wamerekebisha uzi, mtoa mada hakuweka wala hakutaka kuweka na alisema kwa maneno yake, fatilia uzi, mimi nikazileta. Mshamba mama yko.Sasa mleta mada hizi nakala si kashaweka huko juu?!?! We vipi?!?! Fungua uzi wako acha ushamba!
Dah mbona mimi ni kijana nisipate hiyo fursaNaskia anapenda sana vijana...😜
Shida yeye ana njaa pia meneja wake jembe nae njaa,alimtoa wasafi ampige pesa zake...jembe kabaki kumtafutia show za ccm na yanga hana jipyaPamoja na kujitapa kununua magari ya kifahari na lingine akamuhonga yule bibi malaya lakini milioni 100+ ameshindwa kulipa 🤔🤔 wasanii wa bongo wengi njaa kali sana ni sifa tuu zina wafichia aibu
Lyrics kali sanaaaa hii.Unakopa hela ya biashara unaenda kumtrombea Kajala.pumbavuu
Naona afua ya akili ya kijana wetu inaenda kupigika soon
View attachment 3072826
View attachment 3072827
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Rajabu Abdukahali Ibrahim almaarufu Harmonize ametiwa hatiani na mahakama kuu divisheni ya biashara tarehe 2 mwezi huu wa 8 kwa kushindwa kulipa kikamilifu mkopo wa kiasi cha shilingi milioni 300 alizokopa katika benki ya CRDB mwaka 2019.
Mkopo huo uliokuwa na riba ya 18% ulielezwa na msanii huyo kama uwekezaji kwenye shughuli zake za kimuziki ikiwemo studio ya kisasa ya uzalishaji wa muziki na video, ulikuwa ulipwe ndani ya miezi 36 (miaka mitatu).
Na ulikuwa mkopo wa awamu mbili, ya kwanza ikiwa milioni 100 kisha awamu ya pili milioni 200 ambazo awamu zote alipewa na benki hiyo mwaka huohuo wa 2019.
Moja ya makubaliano ilikuwa (Harmonize) kufungua akaunti ya kibiashara katika benki hiyo kisha kuiweka milioni 100 na kuifanya akaunti hiyo kuwa akaunti yake kuu katika shughuli zake za kiabishara, takwa hilo pamoja na mengine ikiwemo marejesho ya mkopo kwa kila mwezi yalishindwa kufikiwa na Harmonize.
Baada ya usumbufu uliopitiliza wa ulipaji wa mkopo huo kutoka kwa Harmonize, CRDB walifikia uamuzi wa kwenda mahakamani. Uamuzi huo ambao mahakama ilitoa wito mara kadhaa kwa Harmonize, lakini Harmonize hakufika mahakamani. Na hata mahakama ilipomuomba kutoa maelezo (Written statement of defence WSD) hakufanya hivyo.
CRDB waliendelea kumkumbusha Harmonize kulipa mkopo kila mara na kila njia hadi zikiwemo jumbe za WhatsApp, mwanzoni mwa mwaka 2022 Harmonize aliandika barua kwenda tawi la benki hiyo lililopo Mlimani City akiomba kulipa marejesho kwa kiasi cha 3.3 milioni badala ya utaratibu uliowekwa wa 10.8 milioni kila mwezi wakati huo deni la mkopo likiwa 109,731,733.46/= CRDB walikubali ombi lake hilo ila akitakiwa kulipa 3.9 milioni badala ya 3.3 milioni aliyokuwa ameomba.
Harmonize alifanikiwa kupunguza deni hilo hadi kufikia kiasi cha 103,185,755. Baada ya hapo hakulipa tena hadi kufikia hukumu iliyotolewa 2/08/2024 ambapo msanii huyo ametakiwa kulipa kiasi chote kilichobaki katika mkopo, gharama za kesi na fidia ya milioni 10 na nyinginezo kama mahakama ilivyoona.
Chanzo changu na mimi,
Nifah.
Ndo ulikua hivi mwanetu?