Mahakama yamtia hatiani Harmonize, atakiwa kuilipa mamilioni CRDB!

Mahakama yamtia hatiani Harmonize, atakiwa kuilipa mamilioni CRDB!

Upuuzi kabisa mtu unakuta anatamba eti kazi ya ualimu ni kazi ya Laana,Sasa tangu nizaliwe sijawahi sikia mwalimu kafikishwa mahakamani Kwa kushindwa kulipa mkopo wa benki au kauziwa assets zake Kwa kushindwa kurejesha mikopo ya benki.


Sasa Harmonize kashindwa kulipa M 100,Huu upuuzi,Sitaicha kazi ya ualimu kamwe,hapa navuta Muda nije niende nikavute mpunga M 32 nione mtu ananilaumu Kwa kutegemea mikopo , nijivinjari zaidi.Asante Mungu kwa kazi ya ualimu,Kiufupi huwezi toboa maisha bila kukopa ,kama unakopesheka kopa
Na hapa ni unatumia kishikwambi cha serikali kuombea huu mkopo 😅
 
Vijana wengi ofisi haziendelei mana hakuna mipaka kati ya hela ya ofis na maendeleo na pesa ya bata. Hii kitu inafelisha wengi sana. Kavhukua milion 100 za studio kali afrika masharik na kati kaenda kununua mitumba ya kina stukiiizi pale kinondoni kila wiki anaipeleka maintenance
 

View attachment 3072826
View attachment 3072827

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Rajabu Abdukahali Ibrahim almaarufu Harmonize ametiwa hatiani na mahakama kuu divisheni ya biashara tarehe 2 mwezi huu wa 8 kwa kushindwa kulipa kikamilifu mkopo wa kiasi cha shilingi milioni 300 alizokopa katika benki ya CRDB mwaka 2019.

Mkopo huo uliokuwa na riba ya 18% ulielezwa na msanii huyo kama uwekezaji kwenye shughuli zake za kimuziki ikiwemo studio ya kisasa ya uzalishaji wa muziki na video, ulikuwa ulipwe ndani ya miezi 36 (miaka mitatu).
Na ulikuwa mkopo wa awamu mbili, ya kwanza ikiwa milioni 100 kisha awamu ya pili milioni 200 ambazo awamu zote alipewa na benki hiyo mwaka huohuo wa 2019.

Moja ya makubaliano ilikuwa (Harmonize) kufungua akaunti ya kibiashara katika benki hiyo kisha kuiweka milioni 100 na kuifanya akaunti hiyo kuwa akaunti yake kuu katika shughuli zake za kiabishara, takwa hilo pamoja na mengine ikiwemo marejesho ya mkopo kwa kila mwezi yalishindwa kufikiwa na Harmonize.

Baada ya usumbufu uliopitiliza wa ulipaji wa mkopo huo kutoka kwa Harmonize, CRDB walifikia uamuzi wa kwenda mahakamani. Uamuzi huo ambao mahakama ilitoa wito mara kadhaa kwa Harmonize, lakini Harmonize hakufika mahakamani. Na hata mahakama ilipomuomba kutoa maelezo (Written statement of defence WSD) hakufanya hivyo.

CRDB waliendelea kumkumbusha Harmonize kulipa mkopo kila mara na kila njia hadi zikiwemo jumbe za WhatsApp, mwanzoni mwa mwaka 2022 Harmonize aliandika barua kwenda tawi la benki hiyo lililopo Mlimani City akiomba kulipa marejesho kwa kiasi cha 3.3 milioni badala ya utaratibu uliowekwa wa 10.8 milioni kila mwezi wakati huo deni la mkopo likiwa 109,731,733.46/= CRDB walikubali ombi lake hilo ila akitakiwa kulipa 3.9 milioni badala ya 3.3 milioni aliyokuwa ameomba.

Harmonize alifanikiwa kupunguza deni hilo hadi kufikia kiasi cha 103,185,755. Baada ya hapo hakulipa tena hadi kufikia hukumu iliyotolewa 2/08/2024 ambapo msanii huyo ametakiwa kulipa kiasi chote kilichobaki katika mkopo, gharama za kesi na fidia ya milioni 10 na nyinginezo kama mahakama ilivyoona.

Chanzo changu na mimi,

Nifah.
Nifah kumbe ni mtu wa mahakamani!Nimekukubali
 
Back
Top Bottom