Mahakama yamtia hatiani Harmonize, atakiwa kuilipa mamilioni CRDB!

Mahakama yamtia hatiani Harmonize, atakiwa kuilipa mamilioni CRDB!

Ila Harmonize ni mtata kwenye kulipa madeni, nakumbuka miaka kadhaa hapo nyuma amewahi kukimbia deni la kodi ya nyumba aliyokuwa akiishi huko Mbezi Beach kwa Mchagga mmoja kama 150 Milioni hivi.
Anavyopost anakula maisha kuonesha mkwanja upo kumbe ana hali ngumu na madeni

Kumbe mm nipo vizuri,kuliko hawa wasanii wanaopost post Instagram kua wapo safi 😀
 
ni kigezo gani walitumia kumkopesha 300m? dhamana ilikuwa nini? sisi mbona huwaga mnapiga mnada tu nyumba hamna cha kwenda mahakamani?

ila misamwanda na mikopo ni sukari kwenye supu ya kuku hatakama ni kikoba hauwezi rejesha,
Watuulize sisi Walimu tulikopa tukaenda kulipia watoto English Medium sahivi njaa kali Mshahara unabaki na laki mbili.
 
Back
Top Bottom