Mahakama yamuachia huru Lengai Ole Sabaya, yasema ushahidi wa Jamhuri una utata
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewaachia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita baada ...
Afadhali atendewe haki
P
 
Mungu ni mwema kila hatua dua kijana mzalendo na mchapakazi leo ameigaragaza mahakama mkoani arusha tunazidi kukuombea tuliowengi ili uwe huru urudi uraiani tujenge nchi.
 
wamwachie tu sasa kijana wa watu maana ameteseka sana huko mahabusu.

nadhani mpaka sasa Chadema watakua wameshafurahi vya kutosha hivyo apewe haki yake.
 
Kuna watu wanaishi hii dunia wakiwa ni watu wenye maana Kwa watu tuu, lakini kwa Mungu ni mashetani wakubwa!

Kwa siasa za kijinga na ushetani Lengai kakaa jela bule tuu na uonezi tupu, kisa siasa!!
 
Cha muhimu ameshashika adabu... Akileta tena ujinga tutamnywa supu wenyewe huku mtaani
 
komaaa sabaya komaa, ma CCM siyo watu wema kabisaa, yaani walikutuma kunyanyasa watu na mwisho wamekuachia kesi wewe na mama yako
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewaachia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita baada ya ushahidi uliotolewa na Jamhuri kugubikwa na utata, hivyo kushindwa kuthibitisha mashtaka yaliyokuwa yanawakabili na kuwatia hatiani...
Hata ya Moshi itayeyuka tu.........ni ngumu sana kumfunga mtu mliyekuwa mnashirikiana naye......ila mnamwambia tu zuga zuga huko upepo utulie......
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewaachia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita baada ya ushahidi uliotolewa na Jamhuri kugubikwa na utata, hivyo kushindwa kuthibitisha mashtaka yaliyokuwa yanawakabili na kuwatia hatiani.

Mbali na Sabaya wengine ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

Hata hivyo Sabaya, Nyegu, Aweyo na Msuya wataendelea kubaki mahabusu katika gereza la Karanga kwa kuwa wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi.

Hukumu hiyo imetolewa leo Ijumaa Juni 10 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Patricia Kisinda aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo.

Hii ni kesi ya pili Sabaya kushinda ambapo Mei 6, 2022 na wenzake wawili Sylvester Nyegu na Daniel Mbura, walishinda rufaa iliyokuwa ikisikilizwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha, waliyokata kupinga hukumu ya miaka 30 iliyokuwa imetolewa na na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Hakimu Kisinda amesema kuwa mbali na sababu hizo, mahakama imegundua kuwa hati ya mashitaka ilikuwa na mapungufu na kuwa ushahidi uliotolewa dhidi yao mahakamani hapo haujaweza kuthibitisha mashtaka hayo

Chanzo: Mwananchi
Hiyo haituhusu, Bado tupo NGORONGORO, hatudanganyiki.
 
ABAYA NA WENZAKE WAACHIWA HURU

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewaachia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya pamoja na wenzake sita waliokuwa wanakabiliwa na Kesi ya Uhujumu Uchumi.

Mahakama imesema ushahidi uliotolewa na Mashahidi wa upande wa Jamhuri ulikuwa na utata. Pia imeelezwa kuwa Hati ya Mashtaka ilikuwa na mapungufu ya Kisheria.

Hata hivyo, Sabaya na wenzake Sylvester Nyegu, John Aweyo na Nathan Msuya wataendelea kubaki Mahabusu kutokana na Kesi nyingine ya Uhujumu Uchumi waliyonayo Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi.
Kapona na hii? tusubiri ya Kilimanjaro
 
Back
Top Bottom