Mahakama yamuumbua waziri Magufuli na sheria zake za uongo

Mahakama yamuumbua waziri Magufuli na sheria zake za uongo

Wewe una mpinga magufuli kutokana na uwezo wako mdogo wa kufikiria!

Wew ndio unaonyesha uwezo mdogo kwa kushindwa hata kusoma hukumu ya mahakama kuu ya ardhi. Nilitegemea kuwasiliana na watu wanaoshusha nodno kwa vieleelzo kama nilivyofanya.
 
Katika siku za hivi karibuni umeibuka mgogoro mkubwa wa kijamii hapa nchini uliosababishwa na maamuzi ya kibabe ya Mhe John Magufuli kuhusiana na malor na mabasi, hivi sasa mgogoro huo unapelekea kuathiri vibaya uchumi wa nchi na kusababisha mfumuko wa bei na kuathiri ajira za wananchi wengi sana.

Ndani ya jamii zipo pande mbili zinazolumbana moja ikiongozwa na mtani wangu Jackton Manyerere ikimuunga mkono Mhe Magufuli kutokana tu na kauli yake ya mdomoni kuwa "analinda kusimamia na kufuata sheria" pasipo wahusika kuchukua hatua zozote kujiridhisha kama ni kweli kiongozi huyu analinda na kusimamia sheria kama navyojigamba. Na kundi la pili ni lile linalomuoona kiongozi huyu kama mtu mbabe na asiye na busara wala hekima hata kidogo kutokana na matendo na kauli zake za kibabe. Itakumbukwa kuwa hata Mhe Jakaya Kikwete aliwahi kumwambia hadharani kuwa apunguze ubabe, japo watu wengi sana walimpinga japo upo msemo wa wahenga kuwa "mnyonge mnyongeni haki yake mpeni" leo ukweli umejidhihiri.

Wote tunakumbuka sakata la "Hifadhi ya Barabara" ambapo Mhe Magufuli kwa muda mrefu sana amekuwa akidai kuwa anasimamia na kulinda Sheria ya barabara "The Highway Ordinance Cap 161 of 1967 GN 161 of 5/5/1967" (na wakati huo huo akipuuza na Sheria ya Ardhi ya Vijiji Namba 15 ya 1999 aliyoshiriki kuipitisha akiwa mbunge), alichukua maamuzi ya kibabe na yasiyo na utu ndani yake kwa kuiagiza TANROAD nchi nzima kuingia isivyo halali katika makazi ya wananchi, kuweka alama za "X" kwa maana ya "kuicondemn ardhi za wananchi na hivyo kuwasababishia athari mbali mbali za kijamii na kiuchumi na mara nyingine kubomoa nyumba za wananchi maskini kiasi cha kupeleka baadhi ya kaya kukosa kabisa makazi, kukosa vipato, watoto kushindwa kuendelea na masomo na athari zingine nyingi. Wapo watu waliopoteza maisha kwa magonjwa ya mshtuko wa damu baada ya kubomolewa nyumba zao isivyo halali, kuathiri kiakili kwa kushindwa kutumia ardhi zao kujiondolea umaskini n.k.

Hivi karibuni Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi imetoa hukumu katika kesi namba 80 ya 2005 iliyofunguliwa na Ndg Proches Tarimo na wenzake dhidi ya Wizara ya Ujenzi kupinga amri ya kuboma nyumba za wananchi zilizoko Mita 120 toka katika ya barabara pande zote; eneo la Mbezi Mwisho katika barabara kuu ya Morogoro iliyotolewa na TANROAD mwaka 2004, ikidai eneo hilo ni hifadhi ya barabara kwa mujibu wa sheria hiyo. Itakumbukwa kuwa amri hiyo ya TANROAD ilitolewa miaka mitatu baada ya Mhe John Magufuli kuteuliwa kwa mara ya kwanza kushika wadhifa wa Waziri wa Ujenzi na Rais Benjamin Mkapa na wananchi hao wamekuwa wakiishi maeneo hayo mika nenda rudi pasipo usumbufu wowote.

Itakumbukwa kuwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa barabara ya Morogoro na barabara zingine hapa nchini, ambao hivi sasa wanaoitwa wavamizi wa barabara na Mhe Magufuli, walihamishiwa katika maeneo hayo kwa nguvu tena wengine kwa kuchomewa makazi yao huko walikotolewa na Serikali ya awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere katika "Operesheni Vijiji Vya Ujamaa" iliyofanyika miaka ya 1970s wakati Mhe John Magufuli akiwa bado mtoto mdogo.

Huku Mhe John Magufuli akijigamba "kulinda na kutetea sheria" ya "The Highway Ordinance Cap 161 of 1967" Mahakama Kuu iliyoitamka kuwa batili tokea mwaka 2002 amewasababishia wakazi waishio pembezoni mwa barabara ya Morogoro madhara makubwa ya kisaikolojia, Kijamii na Kiuchumi kwa kuvamia Mita 120 za ardhi za wananchi toka katika ya barabara pande zote mbili za barabara na kuzuia maendelezo ya aina yoyote. Aidha kwa wakati mbali mbali amekuwa akiwaagiza TANROAD kuboma nyumba za wananchi isivyo halali kama ambavyo Mahakam Kuu imetamka.

Kifupi katika hukumu yake Mahakam Kuu Kitengo cha Ardhi imemuunga mkono Raisi Jakaya Kikwete kwa kutambua kuwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa barabara kuu ahpa nchini sio wavamizi wa barabara kama ambavyo Mhe Magufuli amekuwa akidai na kutumia wadhifa wake kuuaminisha umma wa watanzania hivyo. Na imetamka kuwa ardhi husika ni mali ya wananchi kupitia Sheria ya Ardhi ya Vijiji Kifungu cha 15 kwa kuwa waliwekwa hapo walipo na Serikali hiyo hiyo anayoitumikia Mhe Magufuli.

Mahakama hiyo pia imetamka kuwa kwa kuzingatia Sheria ya Mipango Miji eneo la hifadhi ya barabara kwa Jiji la Dar es Salaam ni Mita 30 tu pande zote mbili toka katika ya barabara; na kwa kuwa wanaoishi pembezoni waliwekwa hapo na Serikali katika operesheni Vijiji wanapaswa kulipwa fidia kwa mujibu wa Sheria za Ardhi na ikaeleza utaratibu wa kufuatwa na TANROAD kuamisha ardhi husika kutoka "Ardhi ya Kijiji" kuwa "Hifadhi ya barabara"

Kwa faida ya wasomaji wangu, ibara ya 27 (1) ya Kanuni ya Sheria ya Barabara Namba 13 ya 2007 zilizotolewa kupitia GN Notice No 21 ya tarehe 23 Januari 2009 inaeleza upana wa njia za barabara za lami hapa nchini. Na kwa barabara kuu upana huo usipungue Mita 3.25. Hivyo hivi sasa upana njia za barabara ya Morogoro Road yenye njia mbili ni Mita 6.5.

Hivyo katika upana halali wa hifadhi ya barabara uliotamkwa na Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kupitia hukumu hii wa Mita 30 kila upande wa barabara ya Morogoro. Upo uwezekano wa kujengwa njia 8 mpya za barabara kila upnde na kufanya barabara ya Morogoro Road kuwa ya njia 18 kabla ya TANROAD kuwafikia wananchi walioko nje ya Mita 30 za hifadhi ya barabara zilzotamkwa na Mahakama.

Kibaya zaidi Mhe John Magufuli anavunja hata Sheria ya barabara Na 13 ya 2007 na Kanuni zake 2009 ambzo katika ibara ya Ibara ya 27 (2,4,5) zinamtaka kuwa mara baada ya Waziri wa Ujenzi kuridhika kuwa ardhi fulani inahitajika kwa ajili ya maendeleo ya barabara, atafanya mawasiliano na Wizara wa Ardhi, kwa ajili ya ardhi hiyo kuhifadhiwa baada ya wananchi wanaomiliki ardhi hiyo kulipwa fidia. Na kuwa siku 60 baada ya wananchi kulipwa fidia ndipo Mamalaka ya brabara (TANROAD) itawataka wananchi kuondoka katika ardhi husika.

Baada ya Sheria mpya ya barabara ya 2007 kuongeza eneo la hifadhi ya barabara kutoka Mita 22.86 za zamani hadi Mita 30 kila upande kwa barabara zote kuu. Je Waziri Magufuli aliitia Sheria yake ya barabara kama ilivyofafanua haki za wananchi hapo juu au mara tu aliporejea kuwa Waziri katika Wizara hiyo mwaka 2010/11 aliwaagiza Mameneja wa TANROAD nchi nzima kuweka alama za X katika nyumba za wananchi zilizoko katika hizo Mita 8 zilizoongezeka kutokea 2009?.
Kama alifanya hivyo ukandamizaji wa haki za wananchi wa kiasi hicho ndio ""kulinda kusimamia na kufuata sheria"?


Kwa kuwa ibara 107 107A (1) ya Katiba ya Jamahuri ya Muungano wa Tanzania inatamka "The Judiciary shall be the authority with final decision in dispensation of justice in the United Republic of Tanzania". Kupitia hukumu iliyotajwa hapo juu ni wangapi humu JF watakubalina na mimi kuwa Mhe Magufuli hawezi kuwa na sifa ya "kufuata, kulinda na kusimamia sheria" kutokana na ukweli kuwa alishiriki kama mbunge kupitisha Sheria ya Ardhi Namba 15 mwaka 1999 na katika utendaji wake kwa muda wote tokea ateuliwe kuwa Waziri wa Ujenzi kwa mara ya kwanza mwaka 2000 na Rais Benjamin Mkapa hadi sasa amekuwa akiipuuza sheria hiyo na kutoa kipaumbele kwa "Kijikanuni" ambayo Mahakama Kuu imetamka kuwa ilipoteza nguvu kutokea 1999 lipotungwa, kupitishwa na kuwa Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na 15. Sheria sio kama Menu katika migahawa ambapo mlaji huchagua anataka kula nini.



 
Last edited by a moderator:
Maelezo yako ni mazuri japo marefu sana! Nadhani umekuwa too much negative than reality.... kazi nzuri ya Magufuli hakuna asiyeijua. Unapoponda kiasi hiki hata kama kuna ukweli flani, wewe ndo unaonekana mzushi tu.....

je nani atawalipia masiha ya watu waliopoteza maisha kwa ugonjwa wa mshtuko wa moyo baada ya kubomolewa nyumba kutokana na Magufuli kuiagiza TANROAD kimakosa kuwatuhumu isvyo halali kuwa ni wavamizi wa barabara? Hiyo pekee haitoshi kukufanya uone umuhimu wa Magufuli kuchukua sheria zote za nchi kwa pamoja badala ya kuchukua "Kikanuni" kimoja na kuwaaathiri maelfu ya watu isivyo halali. Wapi uliwahi kuona hifadhi ya barabara ya Mita 120 kila upande wa barabara; yaani uwanja wa mpara na robo (goli hadi goli) kila upande wa barabara.

Sipondi ila nashisha sheria za ukweli ukweli zilizopitishwa katika machekecheke ya waliobobea katika sheria. Kalagabao na uvuvi wako wa kutegemea kauli za Magufuli badala ya kujishughulisha kutafuta sheria ili usome mwenyewe
 
je nani atawalipia masiha ya watu waliopoteza maisha kwa ugonjwa wa mshtuko wa moyo baada ya kubomolewa nyumba kutokana na Magufuli kuiagiza TANROAD kimakosa kuwatuhumu isvyo halali kuwa ni wavamizi wa barabara? Hiyo pekee haitoshi kukufanya uone umuhimu wa Magufuli kuchukua sheria zote za nchi kwa pamoja badala ya kuchukua "Kikanuni" kimoja na kuwaaathiri maelfu ya watu isivyo halali. Wapi uliwahi kuona hifadhi ya barabara ya Mita 120 kila upande wa barabara; yaani uwanja wa mpara na robo (goli hadi goli) kila upande wa barabara.

Sipondi ila nashisha sheria za ukweli ukweli zilizopitishwa katika machekecheke ya waliobobea katika sheria. Kalagabao na uvuvi wako wa kutegemea kauli za Magufuli badala ya kujishughulisha kutafuta sheria ili usome mwenyewe

Mkuu kuna babara upana wake ni mkubwa sana, nafirkiri wewe mgeni na wala sikulaumu:

Atlanta Highway.jpg
 


Nashukuru sana Mloganzila kwa kunipatia ushahidi huo wa picha ukimuonyesha Mhe Magufuli akilidanganya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia kuupotosha umma. Katika hukumu maelezo yake Mhe Magufuli maenukuliwa zaidi ya mara tatu akiwataka wananchi wanaofikiri kuwa wameonewa kwenda Mahakamani na ndio walivyofanya wananchi wa Mbezi Mwisho.

Nianze kwa kuzungumzia kesi ya awali ya boma boma nafikiri ilifanyika mwaka 2002 wakati wa upanuzi wa kwanza wa Morogoro Road, bado wakati ule watanzania walikuwa wakiheshimu sana majina ya mawakili wakubwa na ninakumbuyka kuwa waathrika walimtumia Prof Mgongo Fimbo. Katika kuonyesha kuwa wakili wa waathrika alikuwa mzembe au iliingiliwa kwa namna yoyote na katika hukumu yake Mahakama Kuu iltamaka yafuatayo:-

1) Waathirika hawakuonyesha walipata ardhi husika vipi?
2) Waathirika hawakuonyesha wataathirika vipi?

Hivyo Mahakama imeshindwa kufanya consideration.

Baada ya utangulizim, katika picha hizi Mhe Magufuli anaonekana akijibu swali kuhusu barabara ya Usagara-Kisesa ambapo amedai kuwa barabara hiyo ni ya toka wakati wa Mjerumani na ilikuwa ikitwa T8 na pia akaendelea kuwa Sheria za barabara zimekuwepo toka mwaka 1932 na kufanyiwa marekebisho mwaak 1940,42,49,57,59,67.

Nasema Mhe Magufulia alikuwa akilidanganya Bunge la Jmahiri ya bMuungano wa Tanzania kwa sababu Kifungu cha 15 cha sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya 1999 kinatamka kuwa ""Ugawaji wa ardhi uliofanywa kwa mtu au kundi la watu waishio au waliotakiwa kuhamia na kuishi katika kijiji wakati wowote kati ya 01 Jan 1970 hadi 31 Des 1977 , kama ugawaji huo ulifanywa kwa mujibu wa sheria au kinyume cha sheria au bila kuzingatia sheria yoyote, sasa inathibitishwa kuwa ugawaji huo ni halali na kwamba daima ni wenye nguvu ya kutoa haki na wajibu wa kisheria kwa kundi la watu waliogawiwa ardhi hiyo....." Aidh kifungu cha 16 kinatamka .......... masharti ya kifungu 15 yatatumika kila mara ugawaji wa ardhi ya kijiji ulipofanywa na halmashauri ya kijiji au mamlaka nyingine yoyote mnamo na baada ya 01 jan 1978 hadi tarehe ya kuanza kutumika kwa sheria hii.

Kwa mujibu wa Kifungu cha Sheria ya Ardhi ya Vijiji Nama 5 ya 1999 ambapo wakati kinapitishwa Mhe Magufuli pia alikuwa ni mbunge Sheria zote za barabara alizozitaja Mhe Magufuli zinapoteza uhalali na nguvu kama ambavyo hukumu ya Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi ilivyosema. Sheria anazozitaja Mhe Magufuli zinzweza kuwa na nguvu katika ardhi ambayo haijawahi na mpaka sasa sio ardhi ya Kijiji. Kwingine kote ni anatumia ubabe tu na ni kazi ya wabunge walioko katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa tanzania kuhakikisha kuwa Waziri huyu mbabe anatii sheria za nchi ipasavyo.

Kuthibitisha kuwa Mhe Magufuli hana nia ya kutii sheria
Ibara ya Ibara ya 27 (2,4,5) za kanuni za Sheria ya Barabara Na 13 ya 2007 zilizotolewa 2009 kupitia zilizotolewa kupitia GN Notice No 21 ya tarehe 23 Januari 2009 zinamtaka bayana kuwa "mara baada ya Waziri wa Ujenzi kuridhika kuwa ardhi fulani inahitajika kwa ajili ya maendeleo ya barabara, atafanya mawasiliano na Wizara wa Ardhi, kwa ajili ya ardhi hiyo kuhifadhiwa kwa wananchi wanaomiliki ardhi hiyo kulipwa fidia. Na kuwa siku 60 baada ya wananchi kulipwa fidia ndipo Mamalaka ya brabara (TANROAD) itawataka wananchi kuondoka katika ardhi husika".

Sheria mpya ya barabara Na 13 ya 2007 iliongeza eneo la hifadhi ya barabara kutoka Mita 22.86 za zamani hadi Mita 30 kila upande kwa barabara zote kuu. Ni lini Waziri Magufuli aliwasiliana na Wizara ya Ardhi kwa ajili ya Kuhifadhi hizo Mita 8 zilitamkwa na sheria mpya ya barabara kuwa hifadhi ya barabara. Kilichofanyika ni Waziri Magufuli kuwaagiza Mameneja wa TANROAD nchi nzima kuweka alama za X katika nyumba za wananchi zilizoko katika hizo Mita 8 zilizotamkwa kuongezeka katika hifadhi ya barabara tokea 2009?.
Je huku ndio "kulinda kusimamia na kufuata sheria" akam anavyojigamba? Cha kushangaza wabunge wote wa Bunge wale chama tawala na upinzani wanamwacha mbabe huyu aendelee kusigina haki za wananchi anavyotaka.

Hatusemi kuwa barabara zisijengwe, ni ukweli kuwa miaka ya 1970 watu walihamishiwa katika vijiji vya ujamaa kwa nguvu na wengine hata kuchomewa nyumba na mashamba yao, wakapakiwa katika malori chini ya mitutu ya bunduki na kuja kugawiwa ardhi katika vijiji vya ujamaa pembezoni mwa barabara na Chama na Serikali hii hii anayoitumikia Mhe Magufuli.

Wakati huo chini ya Mwalimu Nyerere magari na mafuta vilikuwa vikinunuliwa kwa vibali sio kwa uhuru kama sasa hivyo hapakuwa na haja ya mabarabara mengi kama sasa. Ni kwanini wakulima wanyonge na maskini waliopoteza ardhi, kuchomewa nyumba na mashamba yao na kuhamishiwa kwa nguvu katika vijiji vya ujamaa leo hii ajitokeze mbabe mwingine kuwapora ardhi na kuwabomolea nyumba zao tena bila fidia? Thisi double tragedy!!!!!!

Wananchi hawa wanatakiwa kulipwa fidia kuanzia ya kupotezewa ardhi, nyumba mashamba na mali zingine wakati wa vijiji vya ujamaa na kukoseshwa fursa za kutumia ardhi waliyogawiwa chini ya opereshani vijiji kwa miaka yote hii tokea Mhe Magufuli ateuliwe kuwa Waziri wa Ujenzi kw amara ya kwanza mwaka 2000.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kuna babara upana wake ni mkubwa sana, nafirkiri wewe mgeni na wala sikulaumu:

View attachment 115902
hao wenzetu hawakufanya hivyo kwa ilihali wakiwakosesha wananchi wao makazi, nina imani waliwalipa wote fidia inavyotakiwa. Hata Mhe Magufuli anaweza kuigeuza dar nzima kuwa Hifadhi ya barabara kikubwa ni haki ya wananchi kulipwa fidia kwa kuwa si kweli wamevamia barabara. Wengi wao waliletwa hapo kwa mitutu ya bunduki.

Inawezekana hayo wengi hamyajui kwa kuwa ukitaka kumficha Mtanzaina jambo liweka katika maandishi. Ni nadra sana kwa wengi wetu kujisomea kujua tulikotoka ndio maana akijitokeza mbabe mmoja kama Mhe Magufuli wengi wetu humwamini. Sisi tumeyajua haya yote kutokana na kujisomea sio kwamba tuna elimu kubwa ila tunajisomea sana.
 
Yawezekana yapo maeneo ambayo magufuli amekiuka sheria!! Lakini si kwa kiwango ambacho unaeleza wewe! Sijawahi kumsikia magufuli akitaja mt120 za barabara ambavyo unasema wewe, huwa anaongelea mita 60 (30+30) labda kama una ushahidi huo utuletee.

Pia watu wanaobomolewa ni waliovamia eneo la 45mt..linalotamkwa na sheria ya zamani.
Code:
Watu walioko nje ya mt 22.5 lakinj ndani ya mt 30  kutoka katikati ya barabara kuu wamewekewa alama ili waweze kupewa fidia kwa mujibu wa sheria.lakini km umejenga ndani ya eneo hilo baada ya seheria basi wewe hustahili kupewa fidia! Na ndiyo anayoyahubiri magufuli!!
Tembelea kati ya Kimara hadi Kiruvia utakuta mabango ya hifadhi ya barabara yaliyowekwa mwaka 2004 Mita 120 toka katika ya barabara ya Morogoro kila upande toka Stop Over hadi Kiruvia.

Pia alimuagiza Mkandarasi aliyekuwa akiifanyia barabara ya Morogoro ukarabati aitwaye "SCANPHIL COLAS" kuingia isivyo halalai katika ardhi hiyo (Mita 120) na kupanda mawe ya mpaka wa barabara na pia kupanda miti ya mikenge. Wewe hujiulizi tu iweje eneo kati ya Ubungo hadi Kibaha kubaki kama kijiji hamna maghorofa, mabenki, supermarket n.k ilihali maeneo pembezoni mwa barabara zingine kama vile barabara ya Kilwa, Bagamayo baada ya mita 30 tu za hifadhi ya barabara kuna maghorofa na huduma mbali mbali za kijamii.

Yaani wewe acha tu huyu jamaa amewatia watu umaskini kuanzia alipoteuliwa kushika wadhifa huo kwa mara ya kwanza mwaka 2000. Kesho nitakuleteeni picha.

Watu walioko nje ya mt 22.5 lakinj ndani ya mt 30 kutoka katikati ya barabara kuu wamewekewa alama ili waweze kupewa fidia kwa mujibu wa sheria.lakini km umejenga ndani ya eneo hilo baada ya seheria basi wewe hustahili kupewa fidia! Na ndiyo anayoyahubiri magufuli!![/QUOTE]

KUHUSU HII HOJA KATIKA UZI WAKO. MADA YETU IMEJIKITA KATIKA KUFUATA, KUSIMAMIA NA KULINDA SHERIA Sheria ya barabara Na 13 ya 2007 na Kanuni zake 2009 NDIO AMBAZO ZILIONGEZA HIFADHI YA BARABARA KUTOKA MITA 22.86 HADI MITA 30. HII IKIWA NI KUINGIA KATIKa ARDHI ZA WANANCHI. SHERIA HIYO PIA IKAWEKA UTARATIBU WA KUFUATWA ibara ya Ibara ya 27 (2,4,5) ya Kanuni za Sheria ya Brabara Na 13 ya 2007 zilizopitishwa 2009 zinamtaka kuwa mara baada ya Waziri wa Ujenzi kuridhika kuwa ardhi fulani inahitajika kwa ajili ya maendeleo ya barabara, atafanya mawasiliano na Wizara wa Ardhi, kwa ajili ya ardhi hiyo kuhifadhiwa baada ya wananchi wanaomiliki ardhi hiyo kulipwa fidia. Na kuwa siku 60 baada ya wananchi kulipwa fidia ndipo Mamlaka ya brabara (TANROAD) itawataka wananchi kuondoka katika ardhi husika.

SHERIA HII TUNAYOZUNGUMZIA IMETUNGWA NA WIZARA YA UJENZI NA KUWASILISHWA BUNGENI KWA AJILI YA KUPITISHWA NA IKAPITA KUWA SHERIA. HIVYO SHERIA HIYO INATAKA PALE ARDHI YA WANANCHI ITAKAPOTWALIWA KWA AJILI YA BARABARA KWANZA WANANCHI WAMUONE MTUMISHI KUTOKA WIZARA YA ARDHI AMBAYE ANAHUSIKA NA KUWALIPA FIDIA. NDIPO SIKU 60 BAADA YA KULIPWA FIDIA WAMUONE MTUMISHI KUTOKA TANROAD KATIKA ARDHI YAKE. KATIKA UZI WAKO UNADAI
WATU WALIOKO NJE YA MITA 22.86 LAKINI NDANI YA MITA 30 NDIO WAMEWEKEWA ALAMA ZA X.

MASWALI
1) ALAMA HIZO ZA X WAMEWEKEWA NA MTUMISHI KUTOKA IDARA IPI YA SERIKALI? WIZARA YA ARDHI AU TANROAD?

2) KAMA ALAMA HIZO NCHI NZIMA ZIMEWEKWA NA WATUMISHI KUTOKA TANROAD, FROM THE CITIZEN'S POINT OF VIEW NI KWA MUJIBU WA SHERIA IPI INAYOMPA TANROAD MAMLAKA YA KUINGIA KATIKA ARDHI FRESH INAYOTAMKWA NA KATIKA SHERIA YA BARABARA LAKINI HAIJALIPIWA FIDIA?

3) JE VITENDO KAMA HIVI SIO WAZIRI WA UJENZI MHE JOHN MAGUFULI KUVUNJA SHERIA YA BARABARA NAMBA 13 NA KANUNI ZAKE ZA 2009 NA PIA KUVUNJA KATIBA ALIYOAPA KUIKLINDA NA HAKI ZA KIKATIBA ZA WATANZANIA WALIOINGILIWA KATIKA ARDHI NA MAKAZI YAO NCHI NZIMA?

4) KAMA WAZIRI WA UJENZI ANASHINDWA KUZINGATIA SHERIA YA BARABARA ILIYOPENDEKEZWA NA WIZARA YAKE, ATAWEZA VIPI KUZINGATIA SHERIA ZINGINE ZA NCHI?

4) KWA KUWA ALAMA HIZO ZA X KATIKA ARDHI NA MAKAZI YA WANANCHI ZIMEWEKWA MUDA MREFU ULIOPITA NCHI NZIMA NA HAKUNA DALILI YOYOTE YA WAATHRIKA WALIOTWALIWA ARDHI YAO KULIPWA FIDIA KWA MUJIBU WA SHERIA, ILIHALI HAWAWEZI TENA KUITUMIA ARDHI HIYO WALA MAJENGO HAYO KWA KUPANGISHA, KAMA DHAMANA N.K ILI KUJIONDOLEA UMASKINI. HII NI HAKI?

NI MADHARA GANI YA KISAIKOLOJIA, KIJAMII NA KIUCHUMI WANANCHI HAWA NCHI NZIMA WANAYAPATA KWA KUINGILIWA KATIKA ARDHI N MAKAZI YAO NA TANROAD KINYUME CHA SHERIA YA BARABARA NAMBA 13 YA 2007?
 
Tembelea kati ya Kimara hadi Kiruvia utakuta mabango ya hifadhi ya barabara yaliyowwekwa mwaka 2004 Mita 120 toka katika ya barabara kila upande. Wewe hujiulizi tu iweje eneo katia ya Ubungo hadi Kibaha kubaki kama kijiji ilihali maeneo pembezoni mwa barabara zingine kama vile barabara ya Kilwa, Bagamayo kuna maghorofa na huduma zingine.

Yaani wewe acha tu huyu jamaa amewatia watu umaskini kuanzia alipoteuliwa kushika wadhifa huo kw amara ya kwanza mwak 2000. Kesho nitakuletea picha.

Wakati nawapongeza kwa kushinda kesi na hivyo kustahili kulipwa fidia na hasara ambayo mmesababishiwa na maamuzi yasiyo sahihi,lakini siina hakika kama ni kweli eneo la hifadhi ni mita 120!

Kuhusu ukubwa wa.eneo la barabara ya Morogoro kuanzia Ubungo mpaka Kibaha naona ni sahihi kabisa kama tunapanga mipango ya maendeleo kwa kuangalia miaka 50 mbeleni. Hizo barabara za Kilwa na Bagamoyo ni vichochoro kama vibarabara vya kawaida mjini. Tutembee hata kwa majirani zetu Kenya,hapo Nairobi tujifunze ujenzi wa miundombinu.
 
Mkuu. Huenda seriakli ikakata rufaa na kushinda. Kuwekwa na serikali ni tofauti na kuwa kwenhe eneo lililopimwa. Mfano watu wa mabwepande wamewekwa pale hawajapewa eneo. Wanaweza kunywanganywa wakati wowote. Kama umefika nchi za wenzetu utaona umbali wa makazi na highways. Moshi wamejitahidi sana. Super highways inakuwa na eneo kubwa zaidi la hifadhi. Cha msingi kama una uwezo usinunue kiwanja ambacho hakijapimwa na epuka viwanja wa barabarani.

Mkuu nakushukuru kwa kuelewa mada vyema. Upungufu wa Mhe Magufuli anapokataa kuwa watu walioko katika eneo hilo hawastahili fidia. hata hukumu ya Mahakama imesema hivyo ukiwa ndani ya mita 30 ukitakiwa kupisha barabara haki yako ni fidia kwa kuwa uliwekwa na serikali hiyo hiyo. Iweje tokea mwaka 2004 awvamie watu walioko Mita 120 toka katikati ya barabara? Ni kwa sheria ipi?
 
Watanzania wengi wanapenda kazi za kukagua magari zifanywe na Majembe Auctions, sheria za barabara ziwe chini ya wakwere, wasifuate oooops wenzetu wanasema Highway Code, hakuna maswala ya alama barabarani wala nini. Wakifa kama Nzi ni kazi ya Mwenyezi Mungu oooops sio nzi yule mshabiki wa Mashoga.

Ukanda wa barabara uwekwe na watu walipwe mafao yao barabara ziwe zenye viwango vinavyokubalika kimataifa, Tanzania waache kuajili hawa wachina na wageni ambao ni economic migrant badala yake waajiri Watanzania waliobobea kwenye nyanja za highway code, mbona wapo wengi tu mfano Canada, Alaska, UK ugerumani, Uholanzi nk. wawape tu expert pecs waone jinsi hii nchi itakavyochukua sura mpya. Roho ya korosho anaondoka nayo M K W E R E kuanzia 2015 baada ya uchaguzi Wabongo rudini nyumbani kujenga nchi yenu. Ebo?

Magufuli hapewi uwezo anaohitaji na hii serikali dhoofu ambayo inaachia maharamia kutimiza uovu wao.
 
Jamani Mh Magufuli siyo mwnasheria labda wanasheria walimshauri vibaya. Maana amekuwa anasimamia sheria na kuzilinda, sioni kwa nini wanasheria wa serkali hawakuona mkanganyiko huu ulivyoonekana katika hukumu. Kwa nini hawakumtaadharisha mapema ili kuokoa gharama, maana sasa ninaona uwezekano mkubwa wa serkali kulipa fidia kubwa kwa watu walioonewa.

Mkuu tafuta mtu aliyeko Ofisi ya Mwanasheria Mkuu au Kitengo cha sheria Tanroad akueleze namna ambavyo wamekuwa wakimpatia ushauri wao laikini kutokana na ubabe wake hataki kusikia chochote. Ndio maana akiletwa Waziri mwingine kesi hizo zinztulia na wnaanchi wanapata haki zao kulipwa fidia. Akirejeshwa Magufuli tu matatizo yanaanza kana kwamba hzo hela za kulipa watu fidia zinatoka mfukoni kwake.

Kama kweli angekuwa na uchungu na fedha za Serikali angekwisha chukua maamuzi ya kujiuzuli kutoka serikali yenye watumishi wanaohifadhi mabilioni ya fedha za walalahoi Uswisi, sio kuwakandamiza wananchi wanyonge.
 
1. Binafsi nakuona umeguswa na Dr.Magufuli kufuta 5% ya uzito wa magari

2. Umejitahidi kuandika lakini unatia huruma kupoteza muda wako, naijua sana sheria ya barabara unayoisema, Morogoro road ni barabara pekee yenye upana tofauti tofauti ukiacha barabara zingine zote inchini.

3. Uongo mkubwa kuwa Morogoro road itajengwa 18 lanes

4. Mengine wenzangu watanisaidia kwa vile naona umeumizwa, but pole piga ua Dr.Magufuli hakuna sehemu utakuta ana tatizo kisheria, yangu macho.



Nakushauri usome uzi wangu upya hususana kuhusu 18 lanes kabla ya kukurupuka kujibu bila ya facts
 
Last edited by a moderator:
Kelele za mpangaji hazimzuii mwenye nyumba kupata usingizi..piga ua Magufuli ni Jembe!!!hakipunguzwi kitu hapo...sheria ni msumeno.
 
Nakushauri usome uzi wangu upya hususana kuhusu 18 lanes kabla ya kukurupuka kujibu bila ya facts

Naomba niquote kipengere cha uzi wako, kama uwezo wangu wa kufikiri siku hizi ni mbovu basi sitochangia tena:

"Hivyo katika upana halali wa hifadhi ya barabara uliotamkwa na Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kupitia hukumu hii wa Mita 30 kila upande wa barabara ya Morogoro. Upo uwezekano wa kujengwa njia 8 mpya za barabara kila upnde na kufanya barabara ya Morogoro Road kuwa ya njia 18 kabla ya TANROAD kuwafikia wananchi walioko nje ya Mita 30 za hifadhi ya barabara zilzotamkwa na Mahakama"
 
Naomba niquote kipengere cha uzi wako, kama uwezo wangu wa kufikiri siku hizi ni mbovu basi sitochangia tena:

"Hivyo katika upana halali wa hifadhi ya barabara uliotamkwa na Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kupitia hukumu hii wa Mita 30 kila upande wa barabara ya Morogoro. Upo uwezekano wa kujengwa njia 8 mpya za barabara kila upnde na kufanya barabara ya Morogoro Road kuwa ya njia 18 kabla ya TANROAD kuwafikia wananchi walioko nje ya Mita 30 za hifadhi ya barabara zilzotamkwa na Mahakama"

Ninachomaanisha ni kuwa katika upana wa hifadhi ya barabara wa Mita 60 yaani Mita 30 ulitamkwa na Mahakama kuwa ndio halali baada ya waliomo kulipwa fidia stahiki, unatosha kujenga njia za barabara (lanes) mpya 18 zikizingatia upana wa Mita 3.25 uliotamkwa na Kanuni ya Sheria ya Barabara Na 13 ya 2007. Hivyo hapakuwepo sababu yoyote ya Mhe Magufuli kuiagiza TANROAD kuvamia ardhi na makazi ya wananchi nje ya Mita 30 hadi 120 katika barabara ya Morogoro.
 
1. Binafsi nakuona umeguswa na Dr.Magufuli kufuta 5% ya uzito wa magari

2. Umejitahidi kuandika lakini unatia huruma kupoteza muda wako, naijua sana sheria ya barabara unayoisema, Morogoro road ni barabara pekee yenye upana tofauti tofauti ukiacha barabara zingine zote inchini.

3. Uongo mkubwa kuwa Morogoro road itajengwa 18 lanes

4. Mengine wenzangu watanisaidia kwa vile naona umeumizwa, but pole piga ua Dr.Magufuli hakuna sehemu utakuta ana tatizo kisheria, yangu macho.



Chongo huitwa kengeza!!! Kupenda kubaya jamani,
yaani unaambiwa mahakama imemkuta magufuli anatekeleza sheria kwa kuvunja sheria wewe bado huelewi, SHERIA YENYEWE NI YA VIJIJI VYA UJAMAAAAAA.
yaani unaudhi kama jiwe.
 
Last edited by a moderator:
"The penalty good men pay for indifference to public affairs is to be ruled by evil men"-plato
 
Back
Top Bottom