Mahakama yamuumbua waziri Magufuli na sheria zake za uongo

Mahakama yamuumbua waziri Magufuli na sheria zake za uongo

Nimefurahi kujifunza kuwa bado kuna vijiji vya ujamaa kando kando mwa barabara ya Morogoro! Idumu siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.
 
Nimefurahi kujifunza kuwa bado kuna vijiji vya ujamaa kando kando mwa barabara ya Morogoro! Idumu siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.

Ndugu yangu Bishoke Vijiji katika Jiji la Dar es Salaam vilifutwa mwaka 1985 kwa Jiji zima kutangazwa eneo la Mipango Miji lakini watu waliokuwa wakimiliki ardhi enzi za Vijiji na kwa utaratibu wowote halali baada ya hapo wanabaki na haki ya umiliki wa ardhi hiyo kwa mujibu wa sheria ya ardhi ya vijiji kwa kuwa inatambua umilkiwa ardhi husika tokea tarehe 1 Januari 1970 kama invyosomeka katika Kifungu cha 15 cha Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya 1999 kinachotamka kuwa “Ugawaji waardhi uliofanywa kwa mtu au kundi la watu waishio au waliotakiwa kuhamia nakuishi katika kijiji wakati wowote kati ya 01 Jan 1970 hadi 31 Des 1977 , kamaugawaji huo ulifanywa kwa mujibu wa sheria au kinyume cha sheria aubila kuzingatia sheria yoyote, sasa inathibitishwa kuwa ugawajihuo ni halali na kwamba daima ni wenye nguvu ya kutoa haki na wajibuwa kisheria kwa kundi la watu waliogawiwa ardhi hiyo....."Aidh kifungu cha 16 kinatamka .......... masharti ya kifungu 15yatatumika kila mara ugawaji wa ardhi ya kijiji ulipofanywa na halmashauri yakijiji au mamlaka nyingine yoyote mnamo na baada ya 01 jan 1978 hadi tarehe yakuanza kutumika kwa sheria hii.
Ikumbukwe kuwa maeneo ya Kimara, Mbezi, Kibamba na Kiruvia vyote hivi vikuwa na vijiji vya ujamaa na waliokuwa wanavijiji na waliofuata baadaye wanalindwa na Sheria hii pia japokuwa Mhe Magufuli hataki kukubali ukweli huo. Kimsingi hakuna eneololote liliokuwa mashambani hapa Tanzania ambalo halikuwa aradhi ya Kijiji
 
Kwa faida ya wasomaji wangu na kwa lengo la kutompatia fursa Mhe John magufuli kuwadanganya watanzania kuwa kwa hukumu hii sasa sekta ya barabara hapa nchini itashindwa kuendelezwa. Ibara ya 27 (1) ya Kanuni ya Sheria ya Barabara Namba 13 ya 2007 zilizotolewa kupitia GN Notice No 21 ya tarehe 23 Januari 2009 inaeleza upana wa njia za barabara za lami (Lanes) hapa nchini. Na kwa njia moja ya barabara kuu (Trunk Roads) upana huo usipungue Mita 3.25. Hivi sasa upana njia za barabara ya Morogoro Road yenye njia mbili ni Mita 6.5.

Hivyo katika upana halali wa hifadhi ya barabara uliotamkwa na Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kupitia hukumu hii wa Mita 30 kila upande wa barabara ya Morogoro unatosha kujenga njia (lanes) 8 mpya za barabara za kuelekea Mlandizi, na njia 8 mpya za kuja Dar, hivyo kuifanya Morogoro Road kuwa ya njia (lanes) 18 kama tutakuwa na uwezo wa kifedha wa kuzijenga, kabla ya TANROAD kuwafikia wananchi walioko nje ya Mita 30 toka katikati ya barabara ambao ndio hifadhi ya barabara iliyotamkwa na Mahakama.
...Kwa faida ya wasomaji waendelee kusoma Ibara ya 29(2)(a)-(g) ya Kanuni ya Sheria ya Barabara Namba 13 ya 2007 zilizotolewa kupitia GN Notice No 21 ya tarehe 23 Januari 2009.
Ibara ya 29(2)(a)-(g) inazungumzia specifically Morogoro Road road reserve widths i.e.
UN Rd to km 10 = 60m
km 10 to km 16 = 90m
km 16 to km 37 = 120m
km37 to km 69 = 60m
km 69 to km 70.60 (Ruvu Bridge) = 90m and
the remainder of the road to MG = 60m.
Halafu hizo lanes hujengi kama unaanika mpunga...kuna side walks, service roads, service lines, etc
 
Maelezo yako ni mazuri japo marefu sana! Nadhani umekuwa too much negative than reality.... kazi nzuri ya Magufuli hakuna asiyeijua. Unapoponda kiasi hiki hata kama kuna ukweli flani, wewe ndo unaonekana mzushi tu.....

Unahaki ya kutoa comment zako ila ni wajibu wako kusoma uzi na kuutafakari kabla ya kutoa comment zako. Hapa ulichokifanya ni kukimbilia swala la haki na swala la wajibu ukasahau. mleta uzi anaonyesha jinsi gani Magufuli anatumia sheria feki kuwaumiza wananchi, na ndio mahali aliposimamia. Sasa wewe unalazimisha amsifie Magufuli? Ila sio mbaya kama wewe ni secretary wa magufuli unaweza ukaanzisha Thread yako na ukamsifia bosi wako.
 
tumesoma vizuri .... ikiwa na pamoja ya kutoa reference ya mwaka 2007 kwa kesi ya 2005!! .... mwambie ajipange tena aandike kitu kinachoeleweka kwa kifupi na aache chuki binafsi na magufuli!

Kesi ni 2005, kesi imeendeshwa kwa miaka mingapi? Reference ya 2007 yawezekana ikatumika kwa namna moja au nyingine.
 
Unahaki ya kutoa comment zako ila ni wajibu wako kusoma uzi na kuutafakari kabla ya kutoa comment zako. Hapa ulichokifanya ni kukimbilia swala la haki na swala la wajibu ukasahau. mleta uzi anaonyesha jinsi gani Magufuli anatumia sheria feki kuwaumiza wananchi, na ndio mahali aliposimamia. Sasa wewe unalazimisha amsifie Magufuli? Ila sio mbaya kama wewe ni secretary wa magufuli unaweza ukaanzisha Thread yako na ukamsifia bosi wako.

Pia huyo anaye mtetea magufuli, aweke na vielelezo/reference kama mwenzake (mleta uzi) alivyofanya.
 
Nitarudi katika wakati mwingine ufaao, lakini nakupongeza mtoa thread maana umechambua mambo mengi kwa kina na kwa vifungu husika vya sheria hizo, nitapitia attachment ulizoweka ili kuwa na neno pia la kusema juu ya hizo fact ulizoshusha hapo juu.
CC WATANABE
 
Last edited by a moderator:
Bado ni hii ya malori na mabasi ile tena upande wake ndo itamtoa kabisa kwenye uwanja wa siasa na kubaki kuwa mtazamaji tu kama akina sisi
 
Tatizo letu watumiaji wa social networks huwa tunabwabwaja tu humu kama tuko kijiweni kwa vile tu tuna computer na simu za kubonyabonya muda wowote tukitaka.hivi kwenu ninyi mnaompinga mleta mada ni wangapi mmefuatilia hii ishu na kujua undani wake?tunaojua hili sakata la Moro road tunakubaliana na mleta mada.Wanaofanya kazi chini ya Magufuli wengi wanakubaliana na mleta huu uzi.wananchi wana uchungu wa kuvurugiwa maisha na mtu asiyefuata sheria nyie mnabaki kupiga porojo tu humu.Kama si busara za Pinda wakati ule kumzuia huyu bwana basi watu wengi zaidi wangekuwa wanalia saa hizi.kuna mambo mengi yametokea Moro road.sasa hivi maeneo mengi ya huko hayana maji kwa sababu STRABAG wamekata mabomba mengi ya maji katika kufumua barabara hii.ni vilio tupu kwa baadhi ya maeneo ya magomeni,manzese,ubungo hadi kimara na viunga vyake.hata kama hawa wananchi ni minority it doesn't mean hawana haki.ilipaswa kutafakari zoezi zima ili kujua jinsi gani litafanyika bila mtu kuumia.ukizingatia barabara hii sasa ni mara ya pili au tatu inajengwa,ni kwa nini serikali inakurupuka tu bila kuangalia haya?watu wakose nyumba zao,wanaobaki wakose maji,huyu mwananchi ataona faida gani kwa maendeleo ya barabara ikiwa yanamkosesha maji,kitu muhimu zaidi?serikali ina mipango mizuri lakini namna watu wake wanavyoitekeleza,inasababisha wananchi wasione umuhimu wake na kuiona mibaya.hawa akina Magufuli ni janga kwa serikali.wengine hatutazami miwani nzuri,suti nadhifu,kiingereza kingi na vyeti vyenye A's.tunatazama how you integrate that with life realities.kiongozi mzuri haitaji popularity ili kufanya kazi yake.anahitaji akili nzuri,elimu,uelewa wa kazi yake na majukumu yake utokanao na uzoefu,uaminifu kwa watu WOTE anaowaongoza(wote na si wengi) pamoja na maamuzi sahihi na ya haki na kwa wakati sahihi huku akizingatia mahitaji ya jamii hiyo.ukipenda sifa sana hautaweza kufuata hizo kanuni hapo juu na mwanzoni utasifiwa sana lakini jamii haitakosa watu makini watakaoyaona makosa yako na kukosoa taratibu lakini kwa uhakika dosage yao itaiingia jamii na hapo utakuwa na wakati mgumu.mnaomsifia sana Magufuli kumbukeni na KUMKOSOA.hapo mtamsaidia sana!hili suala ni la kiutendaji zaidi na sio siasa.hebu na tuziweke siasa kando basi na kumzungumzia Magufuli kama waziri na si mtu binafsi,"wa port" au kada wa chama.
 
Magufuli ndiye huyu huyu alieuza nyumba za serikali msijisahaulishe jamani.yeye alijiuzia 3
 
Umejitahidi sana kuandika mambo mengi ya kumchafua magufuli kuliko kuongelea pande mbili za shilingi uandishi kama huu tunaitwa wa kinafiki usiolenga uhalisia wa mambo,
Kazi ya magufuli ni kubwa sana kwenye jamii hii hata kama kunamapungufu huwezi kumlinganisha na wanasiasa wengine na siyo kwa ubaya ulioweka wewe pole najua inakuuma magufuli akifanya kazi nzuri.
 
Magufuli ndiye huyu huyu alieuza nyumba za serikali msijisahaulishe jamani.yeye alijiuzia 3
Huu sasa umbea unaweza kutwambia namba za nyumba alizojiuzia au akili za kibavicha ndizo zinazokuongoza kichwani mwako.
 
Mkuu. Huenda seriakli ikakata rufaa na kushinda. Kuwekwa na serikali ni tofauti na kuwa kwenhe eneo lililopimwa. Mfano watu wa mabwepande wamewekwa pale hawajapewa eneo. Wanaweza kunywanganywa wakati wowote. Kama umefika nchi za wenzetu utaona umbali wa makazi na highways. Moshi wamejitahidi sana. Super highways inakuwa na eneo kubwa zaidi la hifadhi. Cha msingi kama una uwezo usinunue kiwanja ambacho hakijapimwa na epuka viwanja wa barabarani.
Viwanja vingapi Tanzania vimepimwa?
 
Tatizo letu watumiaji wa social networks huwa tunabwabwaja tu humu kama tuko kijiweni kwa vile tu tuna computer na simu za kubonyabonya muda wowote tukitaka.hivi kwenu ninyi mnaompinga mleta mada ni wangapi mmefuatilia hii ishu na kujua undani wake?tunaojua hili sakata la Moro road tunakubaliana na mleta mada.Wanaofanya kazi chini ya Magufuli wengi wanakubaliana na mleta huu uzi.wananchi wana uchungu wa kuvurugiwa maisha na mtu asiyefuata sheria nyie mnabaki kupiga porojo tu humu.Kama si busara za Pinda wakati ule kumzuia huyu bwana basi watu wengi zaidi wangekuwa wanalia saa hizi.kuna mambo mengi yametokea Moro road.sasa hivi maeneo mengi ya huko hayana maji kwa sababu STRABAG wamekata mabomba mengi ya maji katika kufumua barabara hii.ni vilio tupu kwa baadhi ya maeneo ya magomeni,manzese,ubungo hadi kimara na viunga vyake.hata kama hawa wananchi ni minority it doesn't mean hawana haki.ilipaswa kutafakari zoezi zima ili kujua jinsi gani litafanyika bila mtu kuumia.ukizingatia barabara hii sasa ni mara ya pili au tatu inajengwa,ni kwa nini serikali inakurupuka tu bila kuangalia haya?watu wakose nyumba zao,wanaobaki wakose maji,huyu mwananchi ataona faida gani kwa maendeleo ya barabara ikiwa yanamkosesha maji,kitu muhimu zaidi?serikali ina mipango mizuri lakini namna watu wake wanavyoitekeleza,inasababisha wananchi wasione umuhimu wake na kuiona mibaya.hawa akina Magufuli ni janga kwa serikali.wengine hatutazami miwani nzuri,suti nadhifu,kiingereza kingi na vyeti vyenye A's.tunatazama how you integrate that with life realities.kiongozi mzuri haitaji popularity ili kufanya kazi yake.anahitaji akili nzuri,elimu,uelewa wa kazi yake na majukumu yake utokanao na uzoefu,uaminifu kwa watu WOTE anaowaongoza(wote na si wengi) pamoja na maamuzi sahihi na ya haki na kwa wakati sahihi huku akizingatia mahitaji ya jamii hiyo.ukipenda sifa sana hautaweza kufuata hizo kanuni hapo juu na mwanzoni utasifiwa sana lakini jamii haitakosa watu makini watakaoyaona makosa yako na kukosoa taratibu lakini kwa uhakika dosage yao itaiingia jamii na hapo utakuwa na wakati mgumu.mnaomsifia sana Magufuli kumbukeni na KUMKOSOA.hapo mtamsaidia sana!hili suala ni la kiutendaji zaidi na sio siasa.hebu na tuziweke siasa kando basi na kumzungumzia Magufuli kama waziri na si mtu binafsi,"wa port" au kada wa chama.
Na wewe tumia akili yako vizuri naomba niongelee kitu kimoja kwenye andiko lako kuhusu ujenzi wa barabara unaofanywa moro road .
Umedai kuwa mabomba ya maji yamekatwa sasa kwenye kukata mabomba magufuli anahusika vipi kwa hiyo ulitaka barabara isitngengenezwe ili mabomba yasikatwe hiyo akili kweli,
kwa nini tusiwatake waliopewa tenda ya kujenga wafuate taratibu za ujenzi ikiwa ni pamoja na kulinda hayo mabomba wewe unamdandia waziri kwani ndiye anajenga akili zingine za ajabu sana utadhani bavicha bana.
 
huu sasa umbea unaweza kutwambia namba za nyumba alizojiuzia au akili za kibavicha ndizo zinazokuongoza kichwani mwako.


unabisha.mambo haya yashajadiliwa sana humu na kwenye vyombo vya habari,sasa bisha maana ndiye aliyekuwa waziri mwenye dhamana kipindi hicho.kama siasa umeanza kufuatilia juzi sawa.subiri
 
Bado ni hii ya malori na mabasi ile tena upande wake ndo itamtoa kabisa kwenye uwanja wa siasa na kubaki kuwa mtazamaji tu kama akina sisi
Magufuli siyo kama akina mbowe ni kichwa kingine hili dua lako halitampata.
 
Back
Top Bottom