- Thread starter
- #81
binafsi nimekua mtetez mzuri wa ,agufuli lakini kwa fact huyu jamaa alizoziweka siwez pinga moja kwa moja hayuko sahihi maana kila kitu amejitaidi kukiweka sawa... ni kweli likua inasikitisha mtua leo aambiew mvamiz kwa sheria ya mwaka 67 wakat anaanza kukaa maneno hayo kulikua pori kabisa hata barabara watu walizianzisha wenyewe tu na kama ruling kweli imetolewa na mahakama basi magufuli inabidi ashauliwe vizuri na timu yake ya wanasheria na ikibid arud nyuma still he is the right man for the job!!!
Nakushukuru sana BONA kwa kuukubali ukweli. Hata sisi waathirika imetuchukua miaka zaidi ya 10 kutafiti sheria ili kubaini kuwa Mhe Magufuli anatuonea na kuuzungunza ukweli huo katika vyombo vya sheria na kuviwezesha kutoa maamuzi hayo. Kichekesho kilikuwa mahakamani ambapo wawakilishi wa wizara na TANROAD walishindwa kuifafanulia mahakama wapi Morogoro Road ilikuwa ikipita katika miaka hiyo ya 1932 hadi 67.
Kuhusu Mhe Magufuli kupatiwa ushauri anapatiwa sana na wasaidiz wake na viongozi wake wa juu lakini matokeo yake anaonyesha dharau kutokana na kujiamini kuwa anapendwa na wnaanchi. Utakumbuka alivytaka kubomoa ghrofa la Tanesco je Waziri Mkuu na Raisi Jk wangemwacha aendelee na ubomoaji huo na leo hii Mahakama inatamka sheria anayoitumia ni feki ingekuwaje?