Wewe una mpinga magufuli kutokana na uwezo wako mdogo wa kufikiria!
Ngoja Magufuli aje akumwagie data zake hapa.
Katika siku za hivi karibuni umeibuka mgogoro mkubwa wa kijamii hapa nchini uliosababishwa na maamuzi ya kibabe ya Mhe John Magufuli kuhusiana na malor na mabasi, hivi sasa mgogoro huo unapelekea kuathiri vibaya uchumi wa nchi na kusababisha mfumuko wa bei na kuathiri ajira za wananchi wengi sana.
Ndani ya jamii zipo pande mbili zinazolumbana moja ikiongozwa na mtani wangu Jackton Manyerere ikimuunga mkono Mhe Magufuli kutokana tu na kauli yake ya mdomoni kuwa "analinda kusimamia na kufuata sheria" pasipo wahusika kuchukua hatua zozote kujiridhisha kama ni kweli kiongozi huyu analinda na kusimamia sheria kama navyojigamba. Na kundi la pili ni lile linalomuoona kiongozi huyu kama mtu mbabe na asiye na busara wala hekima hata kidogo kutokana na matendo na kauli zake za kibabe. Itakumbukwa kuwa hata Mhe Jakaya Kikwete aliwahi kumwambia hadharani kuwa apunguze ubabe, japo watu wengi sana walimpinga japo upo msemo wa wahenga kuwa "mnyonge mnyongeni haki yake mpeni" leo ukweli umejidhihiri.
Wote tunakumbuka sakata la "Hifadhi ya Barabara" ambapo Mhe Magufuli kwa muda mrefu sana amekuwa akidai kuwa anasimamia na kulinda Sheria ya barabara "The Highway Ordinance Cap 161 of 1967 GN 161 of 5/5/1967" (na wakati huo huo akipuuza na Sheria ya Ardhi ya Vijiji Namba 15 ya 1999 aliyoshiriki kuipitisha akiwa mbunge), alichukua maamuzi ya kibabe na yasiyo na utu ndani yake kwa kuiagiza TANROAD nchi nzima kuingia isivyo halali katika makazi ya wananchi, kuweka alama za "X" kwa maana ya "kuicondemn ardhi za wananchi na hivyo kuwasababishia athari mbali mbali za kijamii na kiuchumi na mara nyingine kubomoa nyumba za wananchi maskini kiasi cha kupeleka baadhi ya kaya kukosa kabisa makazi, kukosa vipato, watoto kushindwa kuendelea na masomo na athari zingine nyingi. Wapo watu waliopoteza maisha kwa magonjwa ya mshtuko wa damu baada ya kubomolewa nyumba zao isivyo halali, kuathiri kiakili kwa kushindwa kutumia ardhi zao kujiondolea umaskini n.k.
Hivi karibuni Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi imetoa hukumu katika kesi namba 80 ya 2005 iliyofunguliwa na Ndg Proches Tarimo na wenzake dhidi ya Wizara ya Ujenzi kupinga amri ya kuboma nyumba za wananchi zilizoko Mita 120 toka katika ya barabara pande zote; eneo la Mbezi Mwisho katika barabara kuu ya Morogoro iliyotolewa na TANROAD mwaka 2004, ikidai eneo hilo ni hifadhi ya barabara kwa mujibu wa sheria hiyo. Itakumbukwa kuwa amri hiyo ya TANROAD ilitolewa miaka mitatu baada ya Mhe John Magufuli kuteuliwa kwa mara ya kwanza kushika wadhifa wa Waziri wa Ujenzi na Rais Benjamin Mkapa na wananchi hao wamekuwa wakiishi maeneo hayo mika nenda rudi pasipo usumbufu wowote.
Itakumbukwa kuwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa barabara ya Morogoro na barabara zingine hapa nchini, ambao hivi sasa wanaoitwa wavamizi wa barabara na Mhe Magufuli, walihamishiwa katika maeneo hayo kwa nguvu tena wengine kwa kuchomewa makazi yao huko walikotolewa na Serikali ya awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere katika "Operesheni Vijiji Vya Ujamaa" iliyofanyika miaka ya 1970s wakati Mhe John Magufuli akiwa bado mtoto mdogo.
Huku Mhe John Magufuli akijigamba "kulinda na kutetea sheria" ya "The Highway Ordinance Cap 161 of 1967" Mahakama Kuu iliyoitamka kuwa batili tokea mwaka 2002 amewasababishia wakazi waishio pembezoni mwa barabara ya Morogoro madhara makubwa ya kisaikolojia, Kijamii na Kiuchumi kwa kuvamia Mita 120 za ardhi za wananchi toka katika ya barabara pande zote mbili za barabara na kuzuia maendelezo ya aina yoyote. Aidha kwa wakati mbali mbali amekuwa akiwaagiza TANROAD kuboma nyumba za wananchi isivyo halali kama ambavyo Mahakam Kuu imetamka.
Kifupi katika hukumu yake Mahakam Kuu Kitengo cha Ardhi imemuunga mkono Raisi Jakaya Kikwete kwa kutambua kuwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa barabara kuu ahpa nchini sio wavamizi wa barabara kama ambavyo Mhe Magufuli amekuwa akidai na kutumia wadhifa wake kuuaminisha umma wa watanzania hivyo. Na imetamka kuwa ardhi husika ni mali ya wananchi kupitia Sheria ya Ardhi ya Vijiji Kifungu cha 15 kwa kuwa waliwekwa hapo walipo na Serikali hiyo hiyo anayoitumikia Mhe Magufuli.
Mahakama hiyo pia imetamka kuwa kwa kuzingatia Sheria ya Mipango Miji eneo la hifadhi ya barabara kwa Jiji la Dar es Salaam ni Mita 30 tu pande zote mbili toka katika ya barabara; na kwa kuwa wanaoishi pembezoni waliwekwa hapo na Serikali katika operesheni Vijiji wanapaswa kulipwa fidia kwa mujibu wa Sheria za Ardhi na ikaeleza utaratibu wa kufuatwa na TANROAD kuamisha ardhi husika kutoka "Ardhi ya Kijiji" kuwa "Hifadhi ya barabara"
Kwa faida ya wasomaji wangu, ibara ya 27 (1) ya Kanuni ya Sheria ya Barabara Namba 13 ya 2007 zilizotolewa kupitia GN Notice No 21 ya tarehe 23 Januari 2009 inaeleza upana wa njia za barabara za lami hapa nchini. Na kwa barabara kuu upana huo usipungue Mita 3.25. Hivyo hivi sasa upana njia za barabara ya Morogoro Road yenye njia mbili ni Mita 6.5.
Hivyo katika upana halali wa hifadhi ya barabara uliotamkwa na Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kupitia hukumu hii wa Mita 30 kila upande wa barabara ya Morogoro. Upo uwezekano wa kujengwa njia 8 mpya za barabara kila upnde na kufanya barabara ya Morogoro Road kuwa ya njia 18 kabla ya TANROAD kuwafikia wananchi walioko nje ya Mita 30 za hifadhi ya barabara zilzotamkwa na Mahakama.
Kibaya zaidi Mhe John Magufuli anavunja hata Sheria ya barabara Na 13 ya 2007 na Kanuni zake 2009 ambzo katika ibara ya Ibara ya 27 (2,4,5) zinamtaka kuwa mara baada ya Waziri wa Ujenzi kuridhika kuwa ardhi fulani inahitajika kwa ajili ya maendeleo ya barabara, atafanya mawasiliano na Wizara wa Ardhi, kwa ajili ya ardhi hiyo kuhifadhiwa baada ya wananchi wanaomiliki ardhi hiyo kulipwa fidia. Na kuwa siku 60 baada ya wananchi kulipwa fidia ndipo Mamalaka ya brabara (TANROAD) itawataka wananchi kuondoka katika ardhi husika.
Baada ya Sheria mpya ya barabara ya 2007 kuongeza eneo la hifadhi ya barabara kutoka Mita 22.86 za zamani hadi Mita 30 kila upande kwa barabara zote kuu. Je Waziri Magufuli aliitia Sheria yake ya barabara kama ilivyofafanua haki za wananchi hapo juu au mara tu aliporejea kuwa Waziri katika Wizara hiyo mwaka 2010/11 aliwaagiza Mameneja wa TANROAD nchi nzima kuweka alama za X katika nyumba za wananchi zilizoko katika hizo Mita 8 zilizoongezeka kutokea 2009?. Kama alifanya hivyo ukandamizaji wa haki za wananchi wa kiasi hicho ndio ""kulinda kusimamia na kufuata sheria"?
Kwa kuwa ibara 107 107A (1) ya Katiba ya Jamahuri ya Muungano wa Tanzania inatamka "The Judiciary shall be the authority with final decision in dispensation of justice in the United Republic of Tanzania". Kupitia hukumu iliyotajwa hapo juu ni wangapi humu JF watakubalina na mimi kuwa Mhe Magufuli hawezi kuwa na sifa ya "kufuata, kulinda na kusimamia sheria" kutokana na ukweli kuwa alishiriki kama mbunge kupitisha Sheria ya Ardhi Namba 15 mwaka 1999 na katika utendaji wake kwa muda wote tokea ateuliwe kuwa Waziri wa Ujenzi kwa mara ya kwanza mwaka 2000 na Rais Benjamin Mkapa hadi sasa amekuwa akiipuuza sheria hiyo na kutoa kipaumbele kwa "Kijikanuni" ambayo Mahakama Kuu imetamka kuwa ilipoteza nguvu kutokea 1999 lipotungwa, kupitishwa na kuwa Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na 15. Sheria sio kama Menu katika migahawa ambapo mlaji huchagua anataka kula nini.
Maelezo yako ni mazuri japo marefu sana! Nadhani umekuwa too much negative than reality.... kazi nzuri ya Magufuli hakuna asiyeijua. Unapoponda kiasi hiki hata kama kuna ukweli flani, wewe ndo unaonekana mzushi tu.....
je nani atawalipia masiha ya watu waliopoteza maisha kwa ugonjwa wa mshtuko wa moyo baada ya kubomolewa nyumba kutokana na Magufuli kuiagiza TANROAD kimakosa kuwatuhumu isvyo halali kuwa ni wavamizi wa barabara? Hiyo pekee haitoshi kukufanya uone umuhimu wa Magufuli kuchukua sheria zote za nchi kwa pamoja badala ya kuchukua "Kikanuni" kimoja na kuwaaathiri maelfu ya watu isivyo halali. Wapi uliwahi kuona hifadhi ya barabara ya Mita 120 kila upande wa barabara; yaani uwanja wa mpara na robo (goli hadi goli) kila upande wa barabara.
Sipondi ila nashisha sheria za ukweli ukweli zilizopitishwa katika machekecheke ya waliobobea katika sheria. Kalagabao na uvuvi wako wa kutegemea kauli za Magufuli badala ya kujishughulisha kutafuta sheria ili usome mwenyewe
hao wenzetu hawakufanya hivyo kwa ilihali wakiwakosesha wananchi wao makazi, nina imani waliwalipa wote fidia inavyotakiwa. Hata Mhe Magufuli anaweza kuigeuza dar nzima kuwa Hifadhi ya barabara kikubwa ni haki ya wananchi kulipwa fidia kwa kuwa si kweli wamevamia barabara. Wengi wao waliletwa hapo kwa mitutu ya bunduki.Mkuu kuna babara upana wake ni mkubwa sana, nafirkiri wewe mgeni na wala sikulaumu:
View attachment 115902
Tembelea kati ya Kimara hadi Kiruvia utakuta mabango ya hifadhi ya barabara yaliyowekwa mwaka 2004 Mita 120 toka katika ya barabara ya Morogoro kila upande toka Stop Over hadi Kiruvia.Yawezekana yapo maeneo ambayo magufuli amekiuka sheria!! Lakini si kwa kiwango ambacho unaeleza wewe! Sijawahi kumsikia magufuli akitaja mt120 za barabara ambavyo unasema wewe, huwa anaongelea mita 60 (30+30) labda kama una ushahidi huo utuletee.
Pia watu wanaobomolewa ni waliovamia eneo la 45mt..linalotamkwa na sheria ya zamani.Code:Watu walioko nje ya mt 22.5 lakinj ndani ya mt 30 kutoka katikati ya barabara kuu wamewekewa alama ili waweze kupewa fidia kwa mujibu wa sheria.lakini km umejenga ndani ya eneo hilo baada ya seheria basi wewe hustahili kupewa fidia! Na ndiyo anayoyahubiri magufuli!!
Tembelea kati ya Kimara hadi Kiruvia utakuta mabango ya hifadhi ya barabara yaliyowwekwa mwaka 2004 Mita 120 toka katika ya barabara kila upande. Wewe hujiulizi tu iweje eneo katia ya Ubungo hadi Kibaha kubaki kama kijiji ilihali maeneo pembezoni mwa barabara zingine kama vile barabara ya Kilwa, Bagamayo kuna maghorofa na huduma zingine.
Yaani wewe acha tu huyu jamaa amewatia watu umaskini kuanzia alipoteuliwa kushika wadhifa huo kw amara ya kwanza mwak 2000. Kesho nitakuletea picha.
Mkuu. Huenda seriakli ikakata rufaa na kushinda. Kuwekwa na serikali ni tofauti na kuwa kwenhe eneo lililopimwa. Mfano watu wa mabwepande wamewekwa pale hawajapewa eneo. Wanaweza kunywanganywa wakati wowote. Kama umefika nchi za wenzetu utaona umbali wa makazi na highways. Moshi wamejitahidi sana. Super highways inakuwa na eneo kubwa zaidi la hifadhi. Cha msingi kama una uwezo usinunue kiwanja ambacho hakijapimwa na epuka viwanja wa barabarani.
Jamani Mh Magufuli siyo mwnasheria labda wanasheria walimshauri vibaya. Maana amekuwa anasimamia sheria na kuzilinda, sioni kwa nini wanasheria wa serkali hawakuona mkanganyiko huu ulivyoonekana katika hukumu. Kwa nini hawakumtaadharisha mapema ili kuokoa gharama, maana sasa ninaona uwezekano mkubwa wa serkali kulipa fidia kubwa kwa watu walioonewa.
1. Binafsi nakuona umeguswa na Dr.Magufuli kufuta 5% ya uzito wa magari
2. Umejitahidi kuandika lakini unatia huruma kupoteza muda wako, naijua sana sheria ya barabara unayoisema, Morogoro road ni barabara pekee yenye upana tofauti tofauti ukiacha barabara zingine zote inchini.
3. Uongo mkubwa kuwa Morogoro road itajengwa 18 lanes
4. Mengine wenzangu watanisaidia kwa vile naona umeumizwa, but pole piga ua Dr.Magufuli hakuna sehemu utakuta ana tatizo kisheria, yangu macho.
Wewe una mpinga magufuli kutokana na uwezo wako mdogo wa kufikiria!
Mkuu kuna babara upana wake ni mkubwa sana, nafirkiri wewe mgeni na wala sikulaumu:
View attachment 115902
Nakushauri usome uzi wangu upya hususana kuhusu 18 lanes kabla ya kukurupuka kujibu bila ya facts
Naomba niquote kipengere cha uzi wako, kama uwezo wangu wa kufikiri siku hizi ni mbovu basi sitochangia tena:
"Hivyo katika upana halali wa hifadhi ya barabara uliotamkwa na Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kupitia hukumu hii wa Mita 30 kila upande wa barabara ya Morogoro. Upo uwezekano wa kujengwa njia 8 mpya za barabara kila upnde na kufanya barabara ya Morogoro Road kuwa ya njia 18 kabla ya TANROAD kuwafikia wananchi walioko nje ya Mita 30 za hifadhi ya barabara zilzotamkwa na Mahakama"
1. Binafsi nakuona umeguswa na Dr.Magufuli kufuta 5% ya uzito wa magari
2. Umejitahidi kuandika lakini unatia huruma kupoteza muda wako, naijua sana sheria ya barabara unayoisema, Morogoro road ni barabara pekee yenye upana tofauti tofauti ukiacha barabara zingine zote inchini.
3. Uongo mkubwa kuwa Morogoro road itajengwa 18 lanes
4. Mengine wenzangu watanisaidia kwa vile naona umeumizwa, but pole piga ua Dr.Magufuli hakuna sehemu utakuta ana tatizo kisheria, yangu macho.