Mahakama yaridhia kunyongwa aliyemuua Dereva Bodaboda

Mahakama yaridhia kunyongwa aliyemuua Dereva Bodaboda

Mahakama ya Rufani Morogoro, imetupilia mbali rufani ya Justine Chamashine aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kumuua dereva wa bodaboda, Joseph Frorence 'Msimbe'.

Uamuzi huo ulitolewa wiki iliyopita na Jopo la Majaji watatu likiongozwa na Jaji Mkuu Profesa Ibrahimu Juma. Majaji wengine ni Augustine Mwarija na Othman Makungu.

Chamashine alikata rufani kupinga hatia na adhabu aliyopewa na Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam. Majaji hao walisema baada ya kupitia hoja za pande zote mbili wamebaini hoja za rufani hazina mashiko na Mahakama Kuu ilimhukumu mrufani kwa usahihi. Walibainisha miongoni mwa hoja za mrufani kupinga adhabu hiyo ilikuwa ni kwamba Mahakama Kuu ilikosea kumhukumu kwa kutumia ushahidi wa kukutwa na vitu vya marehemu huku kukiwa hakuna ushahidi iwapo wakati Msimbe anauawa alikuwa akitumia pikipiki aliyokutwa nayo yeye.

Pia, alidai hakuna ushahidi wa malalamiko unaomuunganisha mrufani na pikipiki iliyoibwa kwasababu upande wa Jamhuri umeshindwa kumuita Ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuthibitisha umiliki wake.
Wakizichambua hoja hizo, Majaji walisema Jaji wa Mahakama Kuu alikuwa sahihi kusema mrufani ndiye aliyemuua Msimbe. Aidha, walisema ushahidi unaonyesha mrufani alikamatwa na polisi akiwa anamiliki pikipiki hiyo ilithibitishwa na mmiliki wake halali ambaye alimkabidhi Msimbe kufanya biashara ya kubeba abiria Januari 6, mwaka 2017.

Ilielezwa Januari 9, mwaka 2017, Msimbe aliuawa na siku iliyofuata saa 7:30 mchana askari walimkamata mrufani akiwa anaendesha pikipiki hiyo, ndipo walipomfungulia shtaka la mauaji kwasababu alikutwa na pikipiki iliyokuwa inaendeshwa na Msimbe.​

Majaji hao walisema kwa ushahidi huo, hawaoni hitimisho lingine isipokuwa kama Jaji wa mahakama ya chini alivyoeleza kwamba mrufani alihusika na mauaji ya Msimbe na kuiba pikipiki.

Majaji hao walisema kutokana na hali hiyo wameona hoja za mrufani hazina mashiko, hivyo wanaitupa rufani kama ilivyokatwa. Chamashine alitenda kosa hilo, Januari 9, mwaka 2017, eneo la Kikwaraza, Kata ya Mikumi, Wilaya ya Kilosa, Morogoro.
Ila hao majaji wanaendesha mahakama kwa hisia, hivi hao majaji wana akili timamu kweli?!

Kwahiyo kukutwa unaendesha pikipiki ambayo si mali ya marehemu, ila tu mtu kaamua kusema kwamba ilikuwa inaendeshwa na marehemu, basi mnanyonga mtu? What if kama mwenye hiyo pikipiki alimkabidhi afanyie kazina wala hajui chochote kuhusu hayo mauaji?
 
Unamhukumu vipi mtu kufa kwa ushahidi wa kimazingira tu?
Hata mimi nimeshangaa sana, kuna ushahidi gani kama hiyo pikipiki hajapewa na mwenye umiliki nayo afanyie biashara? Yaani mmliki kisa amesema alimoa marehemu basi, mnanyonga tu mtu?!!! Hapo kuna ushahidi gani usio na shaka?! Hawa vilaza wamekuwaje majaji, sijawahi ona majaji vilaza kama hawa toka nizaliwe, maana huwezi sema wamepewa rushwa, ni ukilaza na mihemko!
 
Kwahiyo Jamaa amehukumiwa kifo kwa sababu tu alikamwatwa na Pikipiki aliyokuwa anaendesha Marehemu?

Kwamba ameua wamethibitishaje sasa?
Na hata haijadhibitishwa kwamba ni kweli marehemu alikuwa anaendesha hiyo pikipiki, ukizingatia piansi mali ya marehemu.., ni hearsay tu ya mmiliki kwamba alimpa, tutaamini vipi? Aisee akate rufaa hadi dakika ya mwisho
 
Yan Leo pikipiki ipotee kesho ukutwe nayo wewe, mnataka kusema nin nyie huko juu mnaotetea, huyu ni muuaji,kama sio basi kahusika na anawajua wauaji awataje wakapumzike wote huko.

Nyumban kwetu sisi ni njian kuna siku usiku tunakula tukawatunasikia watu wanabishana hiv ila tunasikia kwa mbali yan tunakuja kushtuka yule boda anapiga kelele za msaada tunafika pale kashakatwa katwaapanga, kichwan, mabegan na mikononi, wezi wabayaa saaana
Sikikiza wewe nyau, pikipiki si mali ya marehemu, na hakuna ushahidi wowote kwamba hiyo pikipiki ilikuwa inaendeshwa na marehemu, zaidi ya maneno tu yabmmiliki kwamba alimpa marehemu afanye biashara, sasa mahakama haifanyi kazi kwa hisia au kuhisi tu, lazima pawe na udhibitisho kwamba kweli alikuwa anaendesha hiyo pikipiki..., na pia ionyeshwe kwamba mrufani kaua.., inawezekana alipewa na yeye afanye biashara na huyohuyo mmiliki halafu anamdondoshea jumba bovu
 
Sikikiza wewe nyau, pikipiki si mali ya marehemu, na hakuna ushahidi wowote kwamba hiyo pikipiki ilikuwa inaendeshwa na marehemu, zaidi ya maneno tu yabmmiliki kwamba alimpa marehemu afanye biashara, sasa mahakama haifanyi kazi kwa hisia au kuhisi tu, lazima pawe na udhibitisho kwamba kweli alikuwa anaendesha hiyo pikipiki..., na pia ionyeshwe kwamba mrufani kaua.., inawezekana alipewa na yeye afanye biashara na huyohuyo mmiliki halafu anamdondoshea jumba bovu
Kama alishindwa kutoa maelezo ameipataje hiyo pikipiki kwa nini asichukuliwe yeye ndio mtoa roho.
 
Ndo angesema pikipiki ya marehemu aliipata wapi ndani ya masaa 24 baada ya kifo chake?
Pikipiki haikuwa ya marehemu, ni ya mtu mwingine, na hakuna ushahidi kwamba alikuwa anaiendesha siku ya tukio zaidi ya maneno tu ya mmiliki
 
Yeye aliyehukumiwa ilibidi awaonyeshe waliyemuuzia pikipiki, sasa kama pikipiki ilitoka kwa marehemu ikaja kwake, tena kwa tofauti ya siku moja, unategemea nini?
Mahakama haijataka kujua yeye kaipataje, kwamba kauziwa au kaiotaje hilo swala hawataka kujua, sasa atawaonyesha vipi?
 
Unapozungumzia matumizi ni lazima ufafanue ni matumizi gani!!?, labda alikuwa anaitorosha kwa kuiendesha au alikuwa anaitafutia soko huku akiiendesha nk, juu ya yote kama hakuhusika na tukio la kuua na kupora angeeleza kaipataje hiyo pikipiki, just simple case.
Mahakama haijataka kusikia kwamba kaipataje, sasa ataelezaje na hakuna aliye tayari kusikiliza?
 
Aeleze basi yeye aliipataje. Halafu kakutwa na vitu vya marehemu, alivipata wapi?
Vitu vya marehemu wanavyodai ndio hiyo pikipiki, na haijadhibitishwa na TRA kama ni ya marehemu, na inasemekana si ya marehemu, bali mmliki anadai tu alimpa marehemu, maneno tu, hakuna udhibitisho. Na hata mtu akijutwa navyo, inabidi apewe nafasi ya kueleza mahakama kavipataje, hajapewa nafasi hiyo
 
Kwahiyo aliuziwa bila ushahidi wa watu wala wa kimaandishi ?

Aliyemwuzia si angejulikana ?
Pikipiki ya wizi kuna vibali flani inakosa na inajulikana ni ya wizi.

Mwenye pikipiki alitoa ushahidi wa vibali na wa maneno kuwa Marehemu alikuwa anatumia pikipiki kwa ruhusa yake ya kutafuta pesa. Na baadhi ya vibali alikuwa navyo.

Sasa Mjomba unanunua pikipiki kama unavyonunua Embe unategemea nini ?

Ndio maana kesi imedumu muda mrefu ni kwamba Mahakama ilitaka kujiridhisha.

Na mara zote kesi ya Mauaji mtuhumiwa anapewa Wakili wa Serikali bure ili kumsaidia kuepusha kumwadhibu mtu kwa kubahatisha.
Kwahiyo mtu akinunua bidhaa bila kibali auwawe? Ni jukumu la mahakama kudhibitisha kwamba kaua, sio otherwise.., na hapa sijaona wapi kapewa nafasi ya kueleza wapi kapata hiyo pikipiki
 
Na amini kuna zaidi, mfano kashindwa toa maelezo ya msingi na yanayoeleweka kusema aliitoa wapi, hapo panaweza amua kama yeye ni muuwaji.

Mfano, akijaribhwu kubisha kwamba pikipiki ni yake anayo miaka mingi, na ikathibitika ni ya marehemu, kwa nini aseme uongo
Imedhibitishwaje umiliki wakati hata TRA hawajapewa nafasi ya kudhibitisha?
 
Ni hivi; Mtu aliyeuawa (kama inavyoelezwa) aliuawa na kuporwa pikipiki, yaani sababu ya kuuawa kwake ni ili aporwe pikipiki au aliuawa katika mazingira ya kupambana ili asiporwe pikipiki, kesi hapo inakuwa ni ya Mauaji na hiyo ya uporaji inakufa kifo cha mende, Uchunguzi lazima uwe na mwanzo na mwanzo wake ndio hapo kwamba; siku ya pili TU baada ya tukio ndipo mtu kakutwa/kakamatwa na pikipiki ile ile aliyokuwanayo mtu (bodaboda) aliyeuawa, sasa ilikuwa ni jambo rahisi tu kwa huyo mtu kujibu hili swali; Pikipiki hii umeipataje?? --- bila shaka ni majibu ya swali hili ndiyo yamemtia hatiani kwenye mauaji ya dereva wa boda boda.
Imedhibitishwaje kwamba ni ile ile? Kwa kuangalia rangi yake? Kumbuka TRA hawajapewa nafasi ya kudhibitisha umiliki
 
Aliye uawa hakua mmiliki, sasa mtuhumiwa alitaka TRA waje kufanya nini mahakamani?????? Kumbuka mmiliki halisi alisha fika mahakamani kuthibitisha!
Huyo mmiliki halisi kadhibitishwa vipi bila TRA kudhibitisha mahakamani? Na inadhibitishwa vipi ilikuwa inaendeshwa na marehemu muda wa mauaji?
 
Back
Top Bottom