Mahakama yasema kesi ya Tundu Lissu, Juni 2, 2025 itakuwa 'Live'

Mahakama yasema kesi ya Tundu Lissu, Juni 2, 2025 itakuwa 'Live'

PureView zeiss

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2016
Posts
14,521
Reaction score
46,663
Kwa mujibu wa mahakama wenyewe watarusha matangazo ya moja Kwa moja kutoka mahakamani.
Kwa mara ya Kwanza tutashudia matangazo hayo ya mahakama ikiwa kweli Wanafanya hivyo
20250601_220528.jpg
 
photo_2025-06-01_22-11-20.jpg

Mahakama ya Tanzania inapenda kuwatangazia umma kwamba Shauri la Jinai Namba 8606/2025 na namba 8607/2025 kati ya Jamhuri na Tundu Antiphas Lissu ambayo yamepangwa kutajwa na kusikilizwa kesho Jumatatu tarehe 2 Juni, 2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam Kisutu, pamoja na kwamba Mshtakiwa atafikishwa Mahakamani, lakini mwenendo wote wa Mashauri haya, utarushwa mubashara (live).

Lengo la Mahakama kurusha mubashara matangazo ya mwenendo wa mashauri haya ni kuwawezesha Wananchi popote pale walipo na ambao wanapenda kufuatilia mwenendo wa mashauri kuweza kufuatilia bila kuwa na ulazima wa kufika Mahakamani. Aidha, hatua hii ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania, ambao unalenga kuimarisha uwazi, uwajibikaji na matumizi ya teknolojia katika huduma ya utoaji haki.

Tunaomba Umma ufahamu kuwa, Mahakama ya Wazi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam Kisutu ni ndogo ikiwa na uwezo wa kuchukua watu 80 tu. Kwa uwezo huo imekubalika watakaoingia ni Mawakili wa Serikali na Watu wengine (10), Mawakili Utetezi na Watu wengine (60) na Waandishi wa Habari (10).

Aidha, ikumbukwe kwamba Mahakama hiyo inatumiwa na Mahakimu Wakazi zaidi ya 10 ambao watakuwa wanaendesha Mashauri mbalimbali katika Mahakama hiyo. Hivyo, tunashauri na kusisitiza Wananchi wote wenye nia ya kufuatilia mashauri hayo wafuatilie akaunti ya Mahakama kupitia kiungo kitakachowasilishwa kabla ya Mashauri kuanza.

Mahakama inawahakikishia umma na Watanzania wote kuwa itaendelea kutoa haki kwa uwazi, kwa wakati na kwa wote. Tunawahimiza Wananchi wote kuendelea kushirikiana na Mahakama katika kujenga mfumo wa utoaji haki unaozingatia misingi ya Kikatiba, Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali.

Kiungo cha matangazo hayo mubashara kitapatikana kabla ya saa 2:30 Asubuhi tarehe 2 Juni, 2025 kupitia kurasa/ akaunti rasmi za Mahakama ya Tanzania katika Mitandao ya Jamii na tovuti ya Mahakama www.judiciary.go.tz kabla ya mashauri kuanza.

Aidha, watakaohudhuria Mahakamani tunawasisitiza kuchukua tahadhari zote za magonjwa ya mlipuko kama Taarifa kwa Umma iliyotolewa na Wizara ya Afya tarehe 20 Mei, 2025 inavyoelekeza.

CHAMI, Gerard Julius, Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Mahakama ya Tanzania
 
Kwa mujibu wa mahakama wenyewe watarusha matangazo ya moja Kwa moja kutoka mahakamani.
Kwa mara ya Kwanza tutashudia matangazo hayo ya mahakama ikiwa kweli Wanafanya hivyoView attachment 3353060
Acheni UHUNI, tutafika Mahakamani kufuatilia shauri la Mhe. Lissu LIVE. Nani asiyejua mnatoa hukumu zenu kwa kufuata MAELEKEZO kutoka Ikulu? Mahakama ilikwisha wekwa MFUKONI na serikali ya CCM siku nyingi.
 
Pamoja na hii (kama tu notice hii sio feki au bosheni), wapenzi na wafuasi wa CHADEMA fikeni mahakamani kwa wingi kumpa support kiongozi wenu Tundu Lissu...

Aidha, mahakama wekeni TV screens za kutosha nje ya mahakama penye uwazi ili watakaoshindwa kupata nafasi ndani ya mahakama wafuatilie kesi hiyo kwa nje....

By the way, kwanini source iwe kiungo cha mahakama tu..?

Kama kweli mahakama inataka kufanya haki itendeke na ionekane kutendeka ni kwanini wasiruhusu vyombo vingine vya habari vilivyo tayari hususani hizi YouTube channels ambazo ni accessible kwa watu wengi na popote walipo, mfano JamboTV, ChanzoTV, Mwanzo Plus TV nk nk zirushe matangazo hayo..?

Urasimu wa kesi hii kurushwa na source Moja tu ya mahakama pekee itasababisha kufanyika kwa censorship, kwa ku - skip baadhi ya matukio kwa vile serikali kujiona inaaibika...

Hii ni kinyume kabisa na kujinasibu kwa mahakama kuwa inataka kuimarisha openess ya uendeshaji wa mashauri yake...
 
Tutasubiri kama ni kweli, isiwe wanatupanga tusifike mahakamani!
 
Back
Top Bottom