Mahakama yasema kesi ya Tundu Lissu, Juni 2, 2025 itakuwa 'Live'

Mahakama ya Tanzania inapenda kuwatangazia umma kwamba Shauri la Jinai Namba 8606/2025 na namba 8607/2025 kati ya Jamhuri na Tundu Antiphas Lissu ambayo yamepangwa kutajwa na kusikilizwa kesho Jumatatu tarehe 2 Juni, 2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam Kisutu, pamoja na kwamba Mshtakiwa atafikishwa Mahakamani, lakini mwenendo wote wa Mashauri haya, utarushwa mubashara (live).

Lengo la Mahakama kurusha mubashara matangazo ya mwenendo wa mashauri haya ni kuwawezesha Wananchi popote pale walipo na ambao wanapenda kufuatilia mwenendo wa mashauri kuweza kufuatilia bila kuwa na ulazima wa kufika Mahakamani. Aidha, hatua hii ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania, ambao unalenga kuimarisha uwazi, uwajibikaji na matumizi ya teknolojia katika huduma ya utoaji haki.

Tunaomba Umma ufahamu kuwa, Mahakama ya Wazi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam Kisutu ni ndogo ikiwa na uwezo wa kuchukua watu 80 tu. Kwa uwezo huo imekubalika watakaoingia ni Mawakili wa Serikali na Watu wengine (10), Mawakili Utetezi na Watu wengine (60) na Waandishi wa Habari (10).

Aidha, ikumbukwe kwamba Mahakama hiyo inatumiwa na Mahakimu Wakazi zaidi ya 10 ambao watakuwa wanaendesha Mashauri mbalimbali katika Mahakama hiyo. Hivyo, tunashauri na kusisitiza Wananchi wote wenye nia ya kufuatilia mashauri hayo wafuatilie akaunti ya Mahakama kupitia kiungo kitakachowasilishwa kabla ya Mashauri kuanza.

Mahakama inawahakikishia umma na Watanzania wote kuwa itaendelea kutoa haki kwa uwazi, kwa wakati na kwa wote. Tunawahimiza Wananchi wote kuendelea kushirikiana na Mahakama katika kujenga mfumo wa utoaji haki unaozingatia misingi ya Kikatiba, Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali.

Kiungo cha matangazo hayo mubashara kitapatikana kabla ya saa 2:30 Asubuhi tarehe 2 Juni, 2025 kupitia kurasa/ akaunti rasmi za Mahakama ya Tanzania katika Mitandao ya Jamii na tovuti ya Mahakama www.judiciary.go.tz kabla ya mashauri kuanza.

Aidha, watakaohudhuria Mahakamani tunawasisitiza kuchukua tahadhari zote za magonjwa ya mlipuko kama Taarifa kwa Umma iliyotolewa na Wizara ya Afya tarehe 20 Mei, 2025 inavyoelekeza.

CHAMI, Gerard Julius, Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Mahakama ya Tanzania
Wamebana wameachiaaa
Tmk family
 
Sisi tutafika Mahakamani kwa amani endeleeni kurusha live kwa walionje ya Dar mana ile link yenu ina load muda wote hadi session inaisha
 
Halafu wataagiza TCRA kubinya bandwidth ili watetezi wasisikike wanapoishoot maswali serikali
 
Upande wa Jamhuri wajipange haswa,Mawakili watakuwa na weledi wa juu kujipatia ujiko kwa hii platform.

NB:Kwa TCRA hii,kesho network inaweza zimwa miji mikubwa yote.
 
Nice

Mahakama ya Tanzania inapenda kuwatangazia umma kwamba Shauri la Jinai Namba 8606/2025 na namba 8607/2025 kati ya Jamhuri na Tundu Antiphas Lissu ambayo yamepangwa kutajwa na kusikilizwa kesho Jumatatu tarehe 2 Juni, 2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam Kisutu, pamoja na kwamba Mshtakiwa atafikishwa Mahakamani, lakini mwenendo wote wa Mashauri haya, utarushwa mubashara (live).

Lengo la Mahakama kurusha mubashara matangazo ya mwenendo wa mashauri haya ni kuwawezesha Wananchi popote pale walipo na ambao wanapenda kufuatilia mwenendo wa mashauri kuweza kufuatilia bila kuwa na ulazima wa kufika Mahakamani. Aidha, hatua hii ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania, ambao unalenga kuimarisha uwazi, uwajibikaji na matumizi ya teknolojia katika huduma ya utoaji haki.

Tunaomba Umma ufahamu kuwa, Mahakama ya Wazi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam Kisutu ni ndogo ikiwa na uwezo wa kuchukua watu 80 tu. Kwa uwezo huo imekubalika watakaoingia ni Mawakili wa Serikali na Watu wengine (10), Mawakili Utetezi na Watu wengine (60) na Waandishi wa Habari (10).

Aidha, ikumbukwe kwamba Mahakama hiyo inatumiwa na Mahakimu Wakazi zaidi ya 10 ambao watakuwa wanaendesha Mashauri mbalimbali katika Mahakama hiyo. Hivyo, tunashauri na kusisitiza Wananchi wote wenye nia ya kufuatilia mashauri hayo wafuatilie akaunti ya Mahakama kupitia kiungo kitakachowasilishwa kabla ya Mashauri kuanza.

Mahakama inawahakikishia umma na Watanzania wote kuwa itaendelea kutoa haki kwa uwazi, kwa wakati na kwa wote. Tunawahimiza Wananchi wote kuendelea kushirikiana na Mahakama katika kujenga mfumo wa utoaji haki unaozingatia misingi ya Kikatiba, Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali.

Kiungo cha matangazo hayo mubashara kitapatikana kabla ya saa 2:30 Asubuhi tarehe 2 Juni, 2025 kupitia kurasa/ akaunti rasmi za Mahakama ya Tanzania katika Mitandao ya Jamii na tovuti ya Mahakama www.judiciary.go.tz kabla ya mashauri kuanza.

Aidha, watakaohudhuria Mahakamani tunawasisitiza kuchukua tahadhari zote za magonjwa ya mlipuko kama Taarifa kwa Umma iliyotolewa na Wizara ya Afya tarehe 20 Mei, 2025 inavyoelekeza.

CHAMI, Gerard Julius, Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Mahakama ya Tanzania
 
Lazima kuna shinikizo
Ni hofu kubwa iliyo waingia mioyoni mwao.
Umati uliojitokeza mara ya kwanza hapo mahakamani, na picha zilivyo mwonyesha Tundu Lissu akiwa mahakamani hapo hazikuwa za kuwatia moyo hawa watu.

Hatua hii ni kujaribu ku'manage' hali hiyo isiwe hasi sana kwao kwa upande wa wananchi.
 
Kwa mujibu wa mahakama wenyewe watarusha matangazo ya moja Kwa moja kutoka mahakamani.
Kwa mara ya Kwanza tutashudia matangazo hayo ya mahakama ikiwa kweli Wanafanya hivyoView attachment 3353060
Malengo Yao .

1. Kuwa-please western people kinafki
2. Kudhibiti watu kufika mahakamani kwa kigezo kwamba wanaweza kufuatilia kesi hata wakiwa nyumbani
 
Kwa mujibu wa mahakama wenyewe watarusha matangazo ya moja Kwa moja kutoka mahakamani.
Kwa mara ya Kwanza tutashudia matangazo hayo ya mahakama ikiwa kweli Wanafanya hivyoView attachment 3353060
CCM wamejiamini nn? Mara mahakama inaamuru tume ya uchaguzi iwe huru kweli vyombo vya usalama vifanye kazi zake za msingi bila kuathiri upigaji kura na kutangazwa kwa matokeo
 
Nimeshangaa mbunge kughushi elimu yake halafu hadi Sasa hajakamatwa😭😭😭😭 Abasi tarimba
Kama yeye ndiye aliyeshiriki kuzitunga hizo Sheria halafu zimhukumu mwenyewe 🤔🤔🤔 Ndugu ungekuwa wewe ungeweza😂😂😂😂😂
 
1748809402180.jpg
 
Back
Top Bottom