Mahakama yasema kesi ya Tundu Lissu, Juni 2, 2025 itakuwa 'Live'

Mahakama yasema kesi ya Tundu Lissu, Juni 2, 2025 itakuwa 'Live'

Pamoja na hii (kama tu notice hii sio feki au bosheni), wapenzi na wafuasi wa CHADEMA fikeni mahakamani kwa wingi kumpa support kiongozi wenu Tundu Lissu...

Aidha, mahakama wekeni TV screens za kutosha nje ya mahakama penye uwazi ili watakaoshindwa kupata nafasi ndani ya mahakama wafuatilie kesi hiyo kwa nje....

By the way, kwanini source iwe kiungo cha mahakama tu..?

Kama kweli mahakama inataka kufanya haki itendeke na ionekane kutendeka ni kwanini wasiruhusu vyombo vingine vya habari vilivyo tayari hususani hizi YouTube channels ambazo ni accessible kwa watu wengi na popote walipo, mfano JamboTV, ChanzoTV, Mwanzo Plus TV nk nk zirushe matangazo hayo..?

Urasimu wa kesi hii kurushwa na source Moja tu ya mahakama pekee itasababisha kufanyika kwa censorship, kwa ku - skip baadhi ya matukio kwa vile serikali kujiona inaaibika...

Hii ni kinyume kabisa na kujinasibu kwa mahakama kuwa inataka kuimarisha openess ya uendeshaji wa mashauri yake...
Kurusha proceedings za Mahakama hairuhusuwi isipokua tu kama Mhusika ataomba na Hakimu husika ataruhusu, mtu yeyote anaweza kuomba na akaruhusiwa kama walivyofanya hao, sasa kosa la Mahakama ni lipi? Wakirusha live kosa, wasiporusha pia kelele, watanzania mfanyiwe nini?
 
02 June 2025
Hakimu Mkazi Mkuu
Mahakama ya Kisutu
Dar es Salaam

Hakina pressure ya umma kutaka kesi iwe mahakama ya wazi imefanikiwa sana leo, channel kibao HD, dunia inafuatilia kesi ya Tundu Lissu

Haki itatendeka kwa pande ya Tundu Lissu na pia upande wa Jamhuru maana ndani ya korti, ndani ya mipaka ya Tanzania na nje ya mipaka watu wanafuatilia mwenendo wa kesi hii ya kihistoria kwa ukaribu na kujifunza mengi kuhusu raia, dola, madhataka na mfumo wa haki jinai unavyo fanya kazi ili haki ipatikane kwa anayetuhumiwa na mtuhumu.

1748852694187.jpeg
 
Back
Top Bottom