Mahakama yavunja ndoa iliyodumu miaka 21 bila wanandoa kushiriki tendo la ndoa

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Dar es Salaam. Mahakama ya Mwanzo Buguruni imevunja ndoa ya mwimbaji wa nyimbo za injili, Rebecca Magaba na Zabron Maselege baada ya wanandoa hao kutoshiriki tendo la ndoa kwa zaidi ya miaka 18.

Pia, Mahakama hiyo imetoa amri mali zote walizochuma wanandoa hao, ikiwamo shamba la eka 10 lililopo Bagamoyo, maduka mawili yaliyopo Bonyokwa na Mahengo na shamba la miti ya mikaratusi lililopo Kigoma zichukuliwe na Maselege na kiwanja kilichopo Madale kitabaki kwa Rebecca.

Hakimu Mkazi, Mwinyiheri Kondo alisema Mahakama imevunja ndoa hiyo baada ya kuona wanandoa hao wanafanya matendo ya ndoa ambayo si ya kawaida.

Kondo alisema katika ushahidi uliotolewa na Rebecca alidai hawakuwahi kufanya tendo la ndoa tangu wafunge ndoa kutokana na mume wake kutokuwa na korodani.

Alisema kutokana na hilo, Mahakama hiyo imevunja ndoa hiyo, hivyo ndani ya siku 45 haki ya kukata rufaa kwa mdaiwa ipo wazi.

Katika kesi hiyo, Rebecca aliiomba Mahakama hiyo ivunje ndoa hiyo kisheria baada ya kuishi na mume wake kwa miaka 21 bila ya kushiriki tendo la ndoa.


Mwananchi
 
Hiyo sentensi ya mwisho imekaa kichokozi au labda mimi tu.
 
Nishawahi Pata mpenzi mlokole akaniambia ananipenda kweli ila hataki tushiriki hilo tendo

kwakua namimi nilimpenda kweli nikakubali tukapeana ahadi mpaka NDOA kweli mahusiano

yakaanza,siku - wiki - mwezi - miezi - mwaka tuna romance mashine inasimama ila ndio haina pa kwenda

mwaka wa 1 mwaka wa 2 nikapata mchepuko 1 Chance one Goal,huyo katekista wangu tukaachana

ndani ya miaka miwili no kwichikwichi, kitanda kimoja, bafu 1,tunaishi ka tuko beach nikifikiriaga ile kipindi

najiona kama nilikuaga SAMSONI flani hivi mwenye miguvu ya ajabu, katika watu mbinguni tusingekosa ni kipindi cha miaka ile miwili.

sema kuna wakati najionaga nilikuaga boya au niliwekewa limbwata?!! ila kwa yesu hamna limbwata sasa niliwezaje etiiiiiiii? bwana weee mi hata sishangai hao wapeana talaka

wengine tulikufa na kiu na angali tumezungukwa na maji ya kila aina pembeni ila vigezo na masharti ilibidi vizingatiwe.

Sina ujinga huo sasa hivi,kama ni mbingu na niikose eboooo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…