Mahakama yavunja ndoa iliyodumu miaka 21 bila wanandoa kushiriki tendo la ndoa

Mahakama yavunja ndoa iliyodumu miaka 21 bila wanandoa kushiriki tendo la ndoa

Huyo bwana angetafuta namna nyingine ya kuficha siri yake huyo mwanamke amejitahidi lakini ilifikia mahali akachoka, angefanya hivyo yote hayo yasingetokea kuadhirika kiasi hicho.
Naunga hoja ..kwan lazima atumie kiungo chake?si kuna vitu vingine vingesapot .ila nao 21 yrs mnakuja achana ijumaa kuu leo? Wangemaliza uzee pamoja tu
 
Mahakama ya mwanzo Buguruni imevunja ndoa ya Rebbeca Magaba na ndugu Zabron Maselege. Hii ni baada ya wanandoa hao kutoshiriki tendo la ndoa kwa miaka 18.

Amri ya mahakama pia imetoa amri kuwa mali walizochuma kwa pamoja zigawanywe,ambapo bwana Zabron Maselege imeamriwa apate shamba la heka kumi mbalo lipo Bagamoyo, maduka mawili ambayo yapo Bonyokwa na Mahengo na shamba la mikaratusi ambalo lipo Kigoma. Huku Rebecca Magaba akiambulia kiwanja kilichopo Madale.

Mahakama imeamua kuvunja ndoa hiyo baada ya kutambua kuwa wanandoa hao wanatenda matendo ambayo si ya kindoandoa!

Rebecca Magaba amedai mahakamani hapo kuwa aliamua kuomba talaka sababu ndoa yao huwa haina tendo la ndoa kwa miaka Kumi na nane, huku akidai kuwa aliyekuwa mume wake hana korodani.

N.b Rebbeca Magaba ni mwanamuziki wa Injili za kumtukuza Mungu na ameishi na mume wake kwa miaka ishirini na moja.
Maajabu sana
 
Mungu amsaidie jamaa asifanye jambo la kipuuzi maana kapoteza mke na aibu yake imeshawekwa wazi kwa kila mtu wake wa karibu.. Mungu amsimamie aseee

Na kwa mnaodhihaki wakati hamjaweka jitihada yoyote kuwa hivyo mlivyo. Ombeni
Mungu asiwakumbushe kuwa
"kabla hujafa, hujaumbika"...
 
Mungu amsaidie jamaa asifanye jambo la kipuuzi maana kapoteza mke na aibu yake imeshawekwa wazi kwa kila mtu wake wa karibu.. Mungu amsimamie aseee

Na kwa mnaodhihaki wakati hamjaweka jitihada yoyote kuwa hivyo mlivyo. Ombeni
Mungu asiwakumbushe kuwa
"kabla hujafa, hujaumbika"...
Nafikiri ishu ilikuwa mali ikabidi wafike mahakamani, vinginevyo wangeyamaliza kimyakimya.
 
Kulikuwa na haja gani kumtaja huyo mwanaume jina kama sio kumdhalilisha kwa wanaomjua.
Ona sasa tumejua udhaifu wake.
Hawajamtendea haki huyo mwanaume kwa kumtangazia udhaifu wake

ni kheri humu mkuu maana kama kesi ishafikishwa mahakamani, story ishakuwa kubwa mtaani, kazini na kwa ndugu zake wote..
Kiufupi jamaa ana hali mbaya, kwanza kwa udhaifu wake na kuachwa tayari anaona maisha yake hayana thamani na kitendo cha aibu yake kuwekwa wazi.. Tayari ni mtihani mara mbili

Mungu amsimamie asichukue maamuzi magumu popote alipo
 
Nafikiri ishu ilikuwa mali ikabidi wafike mahakamani, vinginevyo wangeyamaliza kimyakimya.
itakuwa maana issue kama hizo huishia kwa wazee tu na isitoshe isingekuwa ngumu kuamuliwa na wazazi maana nina uhakika wanajua upungufu wa mtoto wao....
All in all yashatokea
 
Nishawahi Pata mpenzi mlokole akaniambia ananipenda kweli ila hataki tushiriki hilo tendo

kwakua namimi nilimpenda kweli nikakubali tukapeana ahadi mpaka NDOA kweli mahusiano

yakaanza,siku - wiki - mwezi - miezi - mwaka tuna romance mashine inasimama ila ndio haina pa kwenda

mwaka wa 1 mwaka wa 2 nikapata mchepuko 1 Chance one Goal,huyo katekista wangu tukaachana

ndani ya miaka miwili no kwichikwichi, kitanda kimoja, bafu 1,tunaishi ka tuko beach nikifikiriaga ile kipindi

najiona kama nilikuaga SAMSONI flani hivi mwenye miguvu ya ajabu, katika watu mbinguni tusingekosa ni kipindi cha miaka ile miwili.

sema kuna wakati najionaga nilikuaga boya au niliwekewa limbwata?!! ila kwa yesu hamna limbwata sasa niliwezaje etiiiiiiii? bwana weee mi hata sishangai hao wapeana talaka

wengine tulikufa na kiu na angali tumezungukwa na maji ya kila aina pembeni ila vigezo na masharti ilibidi vizingatiwe.

Sina ujinga huo sasa hivi,kama ni mbingu na niikose eboooo
Hahaha ulikuwa boya🤣🤣
 
Back
Top Bottom