DOKEZO Mahakama yavunja ndoa ya Davis Mosha na mkewe aliyeishi naye miaka 28, anyimwa mali. Mosha adai kuibiwa $ milioni 1.4 na jaribio la kupewa sumu

DOKEZO Mahakama yavunja ndoa ya Davis Mosha na mkewe aliyeishi naye miaka 28, anyimwa mali. Mosha adai kuibiwa $ milioni 1.4 na jaribio la kupewa sumu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Wezi na mataperi wa taifa
Mwili wa binadamu ni very complex. Una njia mbali mbali za kujilinda. Hii ya kuona wenye mafanikio kuwa wamefanikiwa kwa njia haramu au umaskini wa mtu unatokana na kudhulumiwa ni njia moja. Angalia hii mifano 1. Vijijini huko kwenye umaskini, akitokea mtu akapata utajiri, wengine wanajiliwaza kwa kusema ni chinja chinja mnyonya damu. Kwa upande mwingine maskini atajiliwaza kwa kusema kuwa umaskini wake umetokana na kulogwa kwa kuonewa kijicho. 2. Marais wa nchi maskini wakielemewa mambo hukimbilia kusema mabeberu au vibaraka wake ndiyo chanzo. Pia baadhi ya jamii zilizotoka kwenye umaskini wa kutupwa, hujiliwaza kwa kuona kuwa umaskini wao umetokana na unyama wa jamii nyingine.
 
Ni mtoto wa uswahilini sana mixer singida line...awali alikuwa muislam...anyway kilichomuokoa Davis ni mizimu ya kiMangi via Makei.
sajo msaada kwenye tuta mkuu. Swali la kufikirika: hivi kama kuna wanandoa ambao mmoja wapo amenunua tiketi ya bahati nasibu na kushinda zawadi kubwa, zile fedha zitahesabika kama ''pato la pamoja'' kama ndoa itavunjika siku moja baada ushindi? Assume, fedha zilizonunu tiketi zilitoka mfukoni mwa aliyeshinda na hakumshirikisha kwa vyovyote mwenzake.
 
notorious anti marriage activist dronedrake kuja usome huku. Dah ndoa baana. Chaliifrancisco naye kalizwa mifugo yote kwa mke wake aliyemuacha nakwenda kwa ndawoo mwengine amebaki na mbusii wawili tu. Nyau kabisa huyu dogo. Afadhali adriz alilizwa tende na halua kutoka kwa mke wake mdogo
Mgerasi wewe ni umbwaaa
 
Mahakama inatoa hukumu kwa hearsay bila vithibitisho taaluma ya sheria wengi hamna ila mmetumia mihemuko kujibu hii ngoma ngumu sana.
Hakuna cha ugumu mme ulio mpenda unamuwekea sumu kwenye chakula? Mimi sinaga tamaa ikitokea mme wangu akanishinda wala sitompeleka mahakamani wala kudai chochote nitaondoka na begi langu akitaka kunipa atanipa atakacho ona nastahili, ķwetu nakula na kunywa bila kutumia jasho afu nina mikono miwili nafanya kazi maisha yanaendelea.

Siwezi muwekea sumu mtoto wa watu kisa mali. Mali kitu gani? Duniani tunatafuta furaha mali tutaziacha kwa nini nibebe dhambi zisizo kuwa za lazima.?
Narudia tena hata mwanaume anitendee unyama gani simuwekei sumu nitaondoka nimwache.

Hivi watu hamnaga huruma? Tusema mfano umemuwekea sumu mme kafa kweli mme ulie lala nae kitanda kimoja akifa kisa sumu ulimuwekea kwenye chakula, saa wanamzika wanashusha jeneza unajisikiaje?

Hapa duniani nitatenda dhambi zote ila sitoshiriki dhambi ya kuua au jaribio la kuua.
 
sajo msaada kwenye tuta mkuu. Swali la kufikirika: hivi kama kuna wanandoa ambao mmoja wapo amenunua tiketi ya bahati nasibu na kushinda zawadi kubwa, zile fedha zitahesabika kama ''pato la pamoja'' kama ndoa itavunjika siku moja baada ushindi? Assume, fedha zilizonunu tiketi zilitoka mfukoni mwa aliyeshinda na hakumshirikisha kwa vyovyote mwenzake.
Mkuu, kwa mujibu wa sheria yetu, hiyo haiwezi kuhesabika kama pato la pamoja kwa kuwa hakuna ushiriki wa mwanandoa mwingine.

Lakini ukijenga hoja mahakamani kuwa labda mwanandoa mwingine ndiye aliyeshauri mwenzake akanunue tiketi, au labda alishiriki kuchagua namba za ushindi, na pia kwamba baada ya ushindi, mshindaji alimtaarifu mwenzake, labda aliomba ushauri wa matumizi ya pesa hiyo nk.. inaweza kuhesabika kama mali ya machumo ya pamoja.

Lakini, mtu anaweza sema kuwa mwenzake alikua anamkataza kubet, sasa anaposhinda betting inakuaje useme mali ya pamoja ilhali ulikuwa unapinga mwenzako asibet?? Inaonesha kabisa kuwa hamkuwa na nia moja kwenye kamari
 
Ukiolewa na mwanaume anaetimiza majukumu yake inabidi ushukuru sana. Kumsomesha huyo binti Uturuki haimfanyi Davis ashindwe kushindwa kuhudumia mke na watoto. Karne hizi kupata mwanaume anaeweza kuihudumia familia ni kazi sana. Na pia ukiangalia umri umeshaenda. Kama alikuwa anaona Davies anatumia hela vibaya angetakiwa ajipange azitafute za kwake. Hata Ulaya na Marekani wanawake hawataki shida. Mwanamke anaolewa na tajiri. Na tajiri anachukua likizo fupi na anaenda kujiliwaza na mchepuko na mke halalamiki. Mwanamke kama anataka kuhudumiwa anatakiwa ajishushe. Na pia ajitambue kuwe yeye ni Mke. Wanaume wanao-oa ni wachache sana siku hizi. Kuna msemo tuliambiwa na mababu zetu wanaume tusioe wanawake wazuri. Lakini ukiangalia kuna mfano wa mwanamme mzuri na mwanaume tajiri. Mwanaume tajiri na mwanamke mzuri wanasumbuliwa sana na vishawishi vya mapenzi. Ukipenda Boga penda na ua lake. Kama maisha ya mwanaume tajiri huyawezi tafuta masikini uwe nae.

Kwamba mwanamke kuolewa na kuhudumiwa na mume aliemchagua mwenyewe kwa hiyari yake ni Msaada??

Kwamba ndoa ni lazima kwa mwanamke kiasi kwamba mpaka vitisho vya uhai na kifo vitumike??

Kwamba kutokua muaminifu kwenye ndoa na kusimamia viapo vya ndoa kwa mwanaume hiyo ni haki yake??

Kwamba wanaume wote matajiri kuwa wazinifu ndio style yao na haki yao ya maisha??

Kwamba unawafahamu wanaume wa Ulaya wenye michepuko na wanaenda kupumzika nayo huku mke akitoa baraka zake??

Kwamba style za maisha ya wanaume wa Ulaya ni haki yenu wanaume wa Afrika kuziiga ila ni kosa na dhambi kubwa kwa wanawake wa Afrika kuishi/kutaka kuishi Kama wanawake wa huko Ulaya (Feminists)??

Umefikiri kwa kutumia nini haswa?

Unapanda mbegu za bangi unatarajia kuvuna mchicha?!

Mwanamke sio Malaikah. Mwanamke ni binaadam tu Kama wewe, tofauti yake kubwa ni maumbile ya viungo vya uzazi.

Tamaa ulizonazo wewe nae pia anazo hizo hizo.

Vishawishi vinavyokuandama wewe nae pia vinamsonga tena pengine zaidi yako.

Magumu na machungu ya maisha yana kipomo sawa sawa kati yako na yeye na wakati mwingine yeye ni kikubwa zaidi.

Unapomtaka mwanamke kukuvumilia katika shida na raha na wewe unategemewa usimame upande huo huo hizo shida a raha zikiwa upande wake.

Unapomtarajia Mkeo kuvumilia madhaifu yako na mapungufu yako ndivyo inavyotarajiwa kutoka kwako pia kuyavumilia mapungufu yake na kuyaelewa madhaifu yake.

Maisha hapa duniani sio mashindano maana mwisho wa siku hesabu sio za pamoja, kila mtu ana zake.

Maisha ya Ndoa pia sio mashindano ni makubaliano ya watu wazima kwa hiyari zao kutengeneza/kuendeleza kizazi chao.

Inapofikia hatua mnaanza kuwa washindani ndani ya Ndoa, hiyo Ndoa haifai tena kuwepo.

Na mawazo na akili Kama zako ndizo zimetufikisha hapa. Hawa wanawake wa sasa ni kizazi cha wanawake walionyanyaswa na “kumilikiwa na kizazi cha wanaume ambao ni mababa zenu ninyi wavulana wa sasa.

Tarajia hali kuwa mbaya zaidi ya sasa maana watoto wakike wanazidi kuamka na ku retaliate, kumbukumbu za mama zao zipo damuni.

Kibaya zaidi baba zenu ninyi wavulana wapo busy kushindana kuwamiliki wanawake kiasi kwamba wamesahau uanaume halisi haswa ni upi so hawana tena nyenzo za kuwaandaa kuwa wanaume halisi.

Chaos is yet to come! Tuvute pumzi.
 
Mfanyabiashara Davis Mosha ameacha na mke wake wa ndoa aliyeishi naye kwa miaka 28 amekwenda kufoji nyaraka za kampuni hukumu imetolewa mke hajapewa urithi hata pini.

Masikini ya Mungu Huyu Mkewe ndiye alikuwa muhasibu wa kampuni zote za huyu mfanyabiashara kwa miaka 20.

Majaji wetu hukumu kama hizi ni za ukandamizaji, mawakili tunaomba msaidie kama hii hukumu ni halali na mahakama zetu zinatoa haki nimeona uonevu mtupu humu Pesa imenunua haki.

Je hii ni sawa?

==========
MAAMUZI YA MAHAKAMA
  • Ndoa kati mlalamikaji na mlalamikiwa imevunjwa na talaka imetoka.
  • Hakuna mali zilizopatikana kwa pamoja kwenye ndoa.
  • Uangalizi wa mtoto Daniela Davis Mosha unakuwa chini ya mlalamikaji(Baba)
  • Mdaiwa anapewa ruhusa ya kuwa na mtoto kipindi cha likizo na siku yenye nafasi kwa mtoto
  • Mdaiwa amekatazwa kutumia jina la mlalamikaji Davis Mosha na amerejeshewa majina yake ya awali
  • Kila mmoja atabeba gharama za kesi

View attachment 2912748View attachment 2912749View attachment 2912750View attachment 2912751View attachment 2912752View attachment 2912753View attachment 2912754View attachment 2912755View attachment 2912756View attachment 2912757View attachment 2912758View attachment 2912759View attachment 2912760View attachment 2912761View attachment 2912762View attachment 2912763View attachment 2912764View attachment 2912765View attachment 2912766View attachment 2912767View attachment 2912768
Kuna sababu kubwa chini ya carpet kwa nini huyo mke wa Mosha hakudai chochote katika hii kesi ya kusisimua.
 
Talaka ni pigo tosha hakuna kitu inauma mwanamke mwenye tamaa kuachwa na kuacha yale mapesa ya mosha
Inawezekana kuwa uko sahihi. Lakini tatizo kubwa katika jamii yetu ni kuona mali yote inayopatikana wakati wa ndoa ni ya mwanaume na anammegea mke wake kama fadhila tu. Kinachosikitisha ni kuwa wanawake wengi wanaamini hivyo pia kwa sababu nao hawathamini mchango wao katika mafanikio ya familia. Hata pale ambapo sheria inasema kuwa ana haki ya kupata mgao katika mali za familia wengi wanaishia kusema kuwa watamuachia Mungu hasa kama aliyekuwa mume wake ni tajiri au mtu mwenye nguvu katika jamii. Hapa mnamlaumu mwanamke kuwa kuwa ana tamaa kama vile kuwa na tamaa ni dhambi. Huyo mume wake asingekuwa na tamaa angepata huo utajiri? Wanaume wangapi wamepata mafanikio kwa sababu mwanamke ana tamaa ya maendeleo ikiwa pamoja na mali? Huyu mwanamke anaitwa malaya wakati aliyekuwa mume wake sio tu ana mipango ya kando na hata mahakama imekiri kuwa amezaa na angalau mmoja wao. Unafik na double standards zenu zinaudhi kwa kweli.

Amandla...
 
Naulizia Shida yake Nancy Ni Mali tu au Kuna kingine? Jamani wanaume mjifunze, Wanawake shida Yao kwenye ndoa ni Mali sio upendo ndio maana vitabu vya Mungu vimeandika tuishi nao kwa akili hawafai, Ona Nancy anavyodhalilisha watoto wake ndugu zake, Ni muongo mpka hata asili yake Anadanganya eti msingida sio msingida huyo ni mndengereko wa rufiji, Sio msingida.

Amekwenda kuungana na lawyer tapel Diana Matundanye Wametengeneza fake documents mmesikia Wapi 9 Dec sikukuuu ya uhuru mahakama zipo wazi eti ndio wame file appeal, Msicheze na sheria na haki halafu mnaponda mahakama kwa utapeli wenu, Judgment ipo mmeweka aliyeondoa case ni yeye Mwenyewe.

Leo Nancy uje kutukana mahakama kwenye mtandao hivi hiyo ni haki, unatafuta huruma kwenye kuponda mhimili wa mahakama yenye kutoa haki, Jamani someni hiyo judgment muone Wapi hakimu kamnyima haki Nancy, Mlitaka hakimu afanye nini kwa yeye kutoa case yake na lawyer wake alikuwepo pale mahakamani.
Nancy waambie wanaokushikia sikio Ukweli, hey BibiTiti na Fundi Mchundo??
Sasa ana lalamika nini ikiwa haya yaliyo andikwa ni yake? Na alitaka mwenyewe na hataki chochote?
 
Attachments

  • IMG_1790.jpeg
    IMG_1790.jpeg
    118.8 KB · Views: 8
Kuna sababu kubwa chini ya carpet kwa nini huyo mke wa Mosha hakudai chochote katika hii kesi ya kusisimua.
Mara nyingi wanawake hawadai kwa kutoelewa haki yao na kwa kuhofia kukosa hata yale makombo ambayo anaweza kupata. Jamii nayo mara nyingi inamkatisha tamaa hasa kama mume ana fedha. Wanaishia kwenda kwa waganga kujaribu kuokoa ndoa yao au kuokoka na kumuachia Mungu. Inasikitisha sana.

Amandla...
 
Kwamba mwanamke kuolewa na kuhudumiwa na mume aliemchagua mwenyewe kwa hiyari yake ni Msaada??

Kwamba ndoa ni lazima kwa mwanamke kiasi kwamba mpaka vitisho vya uhai na kifo vitumike??

Kwamba kutokua muaminifu kwenye ndoa na kusimamia viapo vya ndoa kwa mwanaume hiyo ni haki yake??

Kwamba wanaume wote matajiri kuwa wazinifu ndio style yao na haki yao ya maisha??

Kwamba unawafahamu wanaume wa Ulaya wenye michepuko na wanaenda kupumzika nayo huku mke akitoa baraka zake??

Kwamba style za maisha ya wanaume wa Ulaya ni haki yenu wanaume wa Afrika kuziiga ila ni kosa na dhambi kubwa kwa wanawake wa Afrika kuishi/kutaka kuishi Kama wanawake wa huko Ulaya (Feminists)??

Umefikiri kwa kutumia nini haswa?

Unapanda mbegu za bangi unatarajia kuvuna mchicha?!

Mwanamke sio Malaikah. Mwanamke ni binaadam tu Kama wewe, tofauti yake kubwa ni maumbile ya viungo vya uzazi.

Tamaa ulizonazo wewe nae pia anazo hizo hizo.

Vishawishi vinavyokuandama wewe nae pia vinamsonga tena pengine zaidi yako.

Magumu na machungu ya maisha yana kipomo sawa sawa kati yako na yeye na wakati mwingine yeye ni kikubwa zaidi.

Unapomtaka mwanamke kukuvumilia katika shida na raha na wewe unategemewa usimame upande huo huo hizo shida a raha zikiwa upande wake.

Unapomtarajia Mkeo kuvumilia madhaifu yako na mapungufu yako ndivyo inavyotarajiwa kutoka kwako pia kuyavumilia mapungufu yake na kuyaelewa madhaifu yake.

Maisha hapa duniani sio mashindano maana mwisho wa siku hesabu sio za pamoja, kila mtu ana zake.

Maisha ya Ndoa pia sio mashindano ni makubaliano ya watu wazima kwa hiyari zao kutengeneza/kuendeleza kizazi chao.

Inapofikia hatua mnaanza kuwa washindani ndani ya Ndoa, hiyo Ndoa haifai tena kuwepo.

Na mawazo na akili Kama zako ndizo zimetufikisha hapa. Hawa wanawake wa sasa ni kizazi cha wanawake walionyanyaswa na “kumilikiwa na kizazi cha wanaume ambao ni mababa zenu ninyi wavulana wa sasa.

Tarajia hali kuwa mbaya zaidi ya sasa maana watoto wakike wanazidi kuamka na ku retaliate, kumbukumbu za mama zao zipo damuni.

Kibaya zaidi baba zenu ninyi wavulana wapo busy kushindana kuwamiliki wanawake kiasi kwamba wamesahau uanaume halisi haswa ni upi so hawana tena nyenzo za kuwaandaa kuwa wanaume halisi.

Chaos is yet to come! Tuvute pumzi.
Hakuna mtu mwenye pesa anaweza kuvumilia shida. Kama hauna pesa hauwezi kuelewa hii kauli. Dada yangu kama unataka unyenyekewe kwenye ndoa kama malaika. Tafuta mume masikini na umhudumie kila kitu umpe mpaka hela ya bia. Na kuahidi hata ndugu zake watakutetea ukikosea. Tatizo wanawake wengi mnachukulia uzuri wenu una thamani. Thamani ya binadamu yeyote duniani ni kiasi cha disposable income anachokimkliki. Mwanamke kama hauna hela kubali kuwa mnyonge. Usishindane na mumeo kwa kumkomoa. Wewe na mumeo ni vitu viwili tofauti. Yeye ndio anakuhudumia kila kitu. Na uwezo wake wa kukuhudumia ndio unaosababisha wanawake wenzako wamsumbue. Maisha yana sheria zake. Maisha ni kuchagua nimeshaelezea hapo juu uchague kutokana na maisha unayotaka. Sikubaliani na mwanaume anaetembea na mahawara huku hatimizi majukumu yake kama mume.
 
Mwili wa binadamu ni very complex. Una njia mbali mbali za kujilinda. Hii ya kuona wenye mafanikio kuwa wamefanikiwa kwa njia haramu au umaskini wa mtu unatokana na kudhulumiwa ni njia moja. Angalia hii mifano 1. Vijijini huko kwenye umaskini, akitokea mtu akapata utajiri, wengine wanajiliwaza kwa kusema ni chinja chinja mnyonya damu. Kwa upande mwingine maskini atajiliwaza kwa kusema kuwa umaskini wake umetokana na kulogwa kwa kuonewa kijicho. 2. Marais wa nchi maskini wakielemewa mambo hukimbilia kusema mabeberu au vibaraka wake ndiyo chanzo. Pia baadhi ya jamii zilizotoka kwenye umaskini wa kutupwa, hujiliwaza kwa kuona kuwa umaskini wao umetokana na unyama wa jamii nyingine.
Point nzuri sana utafika mbali
 
Back
Top Bottom