Na hapa ndipo unapokosea.
Ufahamu wako umevipa thamani vitu (pesa + mali) na sio utu, kwa mentality hii husitegemee utulivu kwenye Ndoa.
Kuwindana will be your way of life, wewe na huyo mwenzio na atakae muwahi mwenzie (Case ya DM na mkewe hapa) ndio mjanja.
Uzuri wa mbio za sakafuni huishia ukingoni.
Inakuwaje binaadam wa sasa mnaona wenza wenu ni kama maadui zenu?
Mwana Ndoa unakaa ndoani huku mwenza humuamini hata ukucha, mnaishi kwa kuviziana na kuoteana Kama vibaka ndani ya Ndoa?
Unamzalisha na kumpa jukumu la malezi ya kizazi chako mwanamke ambae kutwa unamnanga na kuona hatoshi kuwa binaadam Kama wewe Kisa tu ni jinsia Ke?
Umewaza matokeo ya kizazi chako kitakachotokana na huyo mwanamke?
Bado tunashangaa kwanini jamii inaenda mrama?!
Kila kukicha unajaza negativity tu kuhusu wenza kwenye Ndoa na ubaya wa Ndoa, positivity na uzuri wa Ndoa vitavutwaje kuwafikia?!
Mwisho wa siku Maisha na Uhai wako hapa duniani na baadae ndani ya Ardhi, ni wewe mwenyewe unaamua yaweje, hakuna miujiza wala maajabu yatafanyika zaidi yako wewe.
We create our future through what we do and believe today, what we do and who we are today is a product of our actions and choices of Yesterday.
We create our own Hell and Heaven.
Na wala hakuna nafuu kati ya Mwanamke wa sasa na Mwanaume wa sasa, they are all cut from the same cloth. Ngoma itaendelea kunoga.