DOKEZO Mahakama yavunja ndoa ya Davis Mosha na mkewe aliyeishi naye miaka 28, anyimwa mali. Mosha adai kuibiwa $ milioni 1.4 na jaribio la kupewa sumu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mkuu za chini ya carpet ni kwamba huyo mama amefanya umafia wa kutisha, na umafia huo kama utajulikana, anaweza potea ulimwengu wa uraiani kwa miongo si chini ya mitatu.
 
Katika hali yoyote ile hilo suala halipo,mali ambao mke kazikuta ndio hazimuhusu ila yote yaliyotokea punde baada ya ndoa basi anahusika .

Rejea mke wa Mrema kupata mgao kidogo baada ya mumuwe kufariki wala ndoa haina muda sana.

Hiyo ni sheria ya mirathi.
Sio sheria ya talaka.
Talaka na mirathi ni vitu viwili tofauti kabisa mkuu.

Mke ni mmiliki wa mali za mume pale Mumewe akifariki halikadhalika na mume ni mmiliki wa mali za mkewe pale mke anapofariki.

Lakini linapokuja suala la talaka. Hali huwa tofauti. Kila mmoja anataja alichochuma na alichomiliki. Hiyo ndio HAKI.
 
Mke ana haki ya kupata mgawanyo wa mali kwa sababu amechum na mume hata kama alikuwa mama wa nyumbani ,pakitokea talaka lazima apate gawio .


Sheria za Tanzania mke ana uwezo hata wa kukopa kwa mgongo wa mumewe haswa jina wakati wote wapo hai.

Chukulia tu miaka 20 ya ndoa halafu watu waseme kwamba mali hazimuhusu sio kweli...katika hali ya kufa au kutalakiana kuna fungu mke anapata kama mchangiaji wa mali.

Mirathi ni ngumu kwa vile ina mlolongo mrefu pamoja wasia wa marehemu unaweza kutazamwa ila talaka ni haki yake kupata haijalishi mume kasemaje.
 
Jamii inakuendesha ndio maana upo hapa umejaa hasira

Kama isingekua jamii ungekua zako home ume-relax limume ushafukuza saa nyingi and you even dont bother

Wingu la jamii inavyo perceive ndio inakupa pressure kiama ndio maana upo hapa kutupa lecture sisi jamii walao tukuelewe upate faraja ya roho yako kwamba upo sahihi

Cha ajabu wewe upo sahihi na jamii haipo sahihi,ila upumbavu wa jamii ni LAZIMA ukupite na uchukue nafasi,so sad!

Pole my friend....
 

Hakuna sheria inayomzuia Mke kufanya kazi ya kuchuma Mali sijui kama unalijua hilo.

Kulea watoto haimpi sababu ya kupewa mgao. Mtoto anaweza kulelewa na mtu yeyote na huyo mtu asipewe Mali au mgao.
Wapo watoto wanalelewa na wajomba, bibi au mama wadogo na hiyo haimaanishi wanatakiwa kupewa mgao.

Mantiki ya kupewa mgao ni uzalishaji, mchango wa uchumi ndani ya familia.

Ni vizuri kila mtu afanye kazi ya kuzalisha mali. Kulea watoto sio kazi huo ni wajibu wa Mzazi.
 
Mwanaume kapata chuma kipya, kazaa naye.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Ndoa ya Mengi ilikuwaje? Mpaka anakufa mtalaka wake alikuwa analipwa kila mwezi baada ya kuachana 😅.

Mke hata awe goli kipa lazima apate labda usioe tu .!
 
Sasa ikiwa hakimu aliyeamua kesi hajapinga hayo madai ya wizi wa pesa na kutaka kuuwawa kwa sumu wewe unabisha kama nani? Na pengine hata wahusika huyajui maisha yao?
 
Sasa ikiwa hakimu aliyeamua kesi hajapinga hayo madai ya wizi wa pesa na kutaka kuuwawa kwa sumu wewe unabisha kama nani? Na pengine hata wahusika huyajui maisha yao?
Kwani hakimu ndio nan? Mtu awe na kesi ya kutaka kuua mtu halafu asifunguliwe mashtaka uliona wapi?


Mbona yule wa Msuya katoka kwa madai ya kuua kabisa.

Cheap politics someone's right is rigged
 
Mkuu za chini ya carpet ni kwamba huyo mama amefanya umafia wa kutisha, na umafia huo kama utajulikana, anaweza potea ulimwengu wa uraiani kwa miongo si chini ya mitatu.
Hizo zinaitwa rumours na zitabakia hivyo mpaka zithibitishwe mbele ya mahakama. Ukitaka kumuua nyani mpe jina baya. Inaelekea pia kuwa aliyekuwa mume wake nae sio malaika lakini watu wanamezea.

Amandla...
 
Double standards zipi bwana wee. Mwanaume mpaka anapozaa nje ya ndoa jua mke hajielewi ameshindwa kumu handle mumewe ama ni mkorofi. Michepuko hutokea sababu ya wanawake kutowajibika ipasavyo na ndoa.
Ni lazima ujitetee. On the same token, mbona hamsemi mwanamke akitembea nje ni kwa sababu mume hajielewi, ameshindwa kumhandle ( pamoja na kuwa yeye ndio kichwa) au ni mkorofi ( anambamiza, anamdharau n.k.). Michepuko inatokea kwa sababu wanaume wanaona ni haki yao na wanajua kuwa jamii haita wahukumu vibaya.

Amandla...
 
Mgao unakuwepo ila mke anaweza kuondoka na kiduchu au kikkubwa kutegemeana na mchango wake kwenye hiyo mali. Halafu ni ngumu sana kama ni mama wa nyumbani kuthibitisha mchango wake. Pia inategemea watoto watakuwa chini ya uangalizi wa nani, kama ni baba, basi mgao kwa mwanamke utaendelea kuwa kiduchu kwani mwanaume atajitetea bado ana jukumu la kulea watoto. Sio rahisi ki hivyo kama wanawake tunavyojiaminisha. Halafu wanaume siku hizi ni wanjanja sana, Mali nyingi haziandikwi kwa majina yao hivyo ni ngumu kugagawanywa.
 

Company properties hazigawanywi kwenye kesi za talaka.

Jaji ameandika vizuri sana. Kuhusu hilo
 
Wanawake wa kibongo washamba sana. Akishakuwa na source ya hela anaona ni bora atafte mpenzi wake private wa kumpelekesha ila mumewe anamuona hana maana kwake tena😂.
Extrovert siku zote mwanamke au mwanaume akitokea dirishani kwenye uhusiano lazima mbeleni afeli na kujuta. Hii huwa ni karma.

Wanawake wengi siku hizi wanajuta hadi kukosa usingizi kwa ubaya waliowafanyia jamaa zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…