This is wrong in so many ways. Bora angekuwa mama wa nyumbani (nayo sio sawa pia) Kama ameshiriki kuchuma nae kwa miaka 20 hiyo ni dhulma.
Lakini mali hazijanisikitisha sana kama ndoa kuvunjika. Miaka 28? Ni madhaifu gani hayo ambayo hawakuweza kuyavumilia baada ya miaka 28?
Ni ngumu sana mwanaume kumuacha mwanamke wake wa miaka 28 ukiona amefanya hayo maamuzi jua kuna kitu amekiona ambacho kwake ni hatari sana na akiendelea kukaa ndani ya huo uhusiano atapoteza zaidi.
Kuhusu kuishi miaka28 na mwanamke haikupi haki za kupata mgao kwasababu mwanaume ni tajiri na wewe umekuwapo akiwa anatajirika.
Shida wanawake eneo hili mnajificha kwenye kivuli cha mke wa Ndoa ila unaweza kuta kwa mfano,kipindi chote hiki mwanaume amekuwa hali nyumbani sababu mkewe hamuandalii chakula bali house girl.
Au hawakuwa na mahusiano ya kimapenzi mazuri yaani ndani hakuna amani na mwanaume amekuwa anamkwepa tu mwanamke ili kuavoid matatizo.
Kitu kingine kama mwanamke alishiriki kwenye utafutaji na alikuwa muajiriwa na alikuwa na mshahara na stahiki za mfanyakazi then anastahili kulipwa kama ni mafao au malimbikizo ya mshahara kama yapo nje ya hapo hawezi tumia neno tumechuma wote iwe kigezo cha kudai mgao wa lazima, so hadi wafanyakazi nao wote basi wakitaka kuondoka wadai mgao wa kampuni na mali kutoka kwa bosi wao.
Hizi sheria za Ndoa inatakiwa kufanyiwa reviews upya ili ziwe fair maana zinawapa wanawake wa sasa maslahi yasiyoendana na hulka na tabia zao. Sheria zinapotafsiriwa zinamtafsiri mwanamke au mke kwa taswira ya wanawake wa miaka ya nyuma ambao walikuwa na ustaarabu wao na walijiheshimu na hawakuwa na makuu na waliitumikia Ndoa kama taasisi na walitaka kudumu nayo.
Hawa wanawake wa kisasa ndoa haina umuhimu na hawaiheshimu wala kuitumikia kama taasisi bali kwao ndoa ni kijiwe cha kujichumia mali za bure na kujipatia matumizi yao ya kila siku. Hawa wanatakiwa kubadilishiwa utaratibu.