Mahakama yavunja ndoa ya Kafulila na Jesca Kishoa

Mahakama yavunja ndoa ya Kafulila na Jesca Kishoa


Kituo Jumuishi Huduma za Kimahakama, Mirathi na Ndoa, Temeke kimeivunja rasmi ndoa kati ya wanasiasa machachari David Kafulila na Jesca Kishoa kupitia shauri la ndoa No 217 ya 2022.

Ndoa hiyo iliyofungwa Aprili 22, 2014 ilivunjwa rasmi Februari 20, 2023 baada ya wanandoa hao kutengana tangu mwaka 2019 kabla Mahakama ione ndoa hiyo imevunjika kiasi cha kutorekebishika.

Wakati hati ya madai ikionyesha kiini cha mgogoro huo ni ugomvi na utengano, Mahakama imevunja ndoa baina ya wawili hao huku ikitoa amri kwa mama kubaki na watoto na kila mzazi kuwa na wajibu wa kuchangia gharama za matunzo kwa asilimia 50.

“Maombi ya Jesca Kishoa akiitaka Mahakama ione ndoa kati yake na David Kafulila imevunjika kiasi cha kutorekebishika na kuomba amri ya Mahakama kuvunja ndoa hiyo, mjibu maombi aliwasilisha majibu yake na hakuwa na pingamizi juu ya maombi yaliyopo mahakamani.

“Eden Kilatu na rashid Hussein, mawakili wasomi wamemwakilisha mleta maombi na mjibu maombi mtawalia. Kilatu ameiomba Mahakama itoe hukumu kwa kuzingatia shauri la Joseph Warioba Butiku vs Perucy Muganda Butiku (1987) TLR 1,” alieleza nakala ya hukumu iliyotolewa na Hakimu Mwandamizi Swai.S.O.

Hakimu Swai ameeleza kwa upande wake hana mashaka kuwa ndoa ya wadaawa imevunjika kiasi cha kutorekebishika chini ya kifungu 107 (2) (f) cha sheria ya ndoa.

“Kwa msingi huo amri ya kuivunja ndoa na talaka inatolewa. Sambamba na hilo, watoto wataishi chini ya uangalizi wa mama yao. Mjibu maombi atakuwa na haki ya kuwaona na kuwa na watoto wake mwishoni mwa juma na vipindi vya likizo za masomo,” ameeleza Jaji Swai.

Katika hukumu hiyo ameeleza kuwa chini ya kifungu 129 cha Sheria ya Ndoa, mjibu maombi anawajibika kutoa matunzo ya watoto kikamilifu.“Ada za shule zitaendelea kulipwa kwa uwiano linganifu (asilimia 50) kwa kila mzazi katika shule watakazokubaliana pamoja.

Hayo ndiyo maamuzi ya Mahakama. Kutokana na asili ya shauri hili hakuna amri ya gharama inatolewa. Imeamuliwa na kuagizwa hivyo,” imeeleza Hakimu Swai.

MWANANCHI
Huyo Jesca Kishoa sio mmoja wa wabunge waliyofoji viti maalum CHADEMA? Kafulila aliingia cha kike hapo. Hiyo sio wife material.
 
Inaonekana Kafulila ana matatizo makubwa, ukitazama historia yake ya kuhamahama vyama kutokana na kukosa uvumilivu na utovu wa nidhamu, na sasa ndoa kuvunjika ni ushahidi kuwa ana matatizo makubwa.
Issue ya ndoa ni kitu kingine kabisa huwezi kumlaumu mtu, tena soma kwa makini muomba maombi ni Jessica na mjibu maombi ni Kafulila ambaye hakuwa na pingamizi kwa muomba maombi ya talaka.

Kafulila amefanya kitu wanaume wengi wanakosa uthubutu wa kufanya na kuishia kufa kwa stroke.
 
Watu bwana, wanawake fresh na ma singo maza yako kibao lakini mtu anamchukua mke wa tumbili na kumshawishi kuvunja ndoa wakati ndoa yake yeye iko intact.
Mimi nilitaka mchepuko nachukua singo maza bila ku disturb ndoa za watu.
 
Issue ya ndoa ni kitu kingine kabisa huwezi kumlaumu mtu, tena soma kwa makini muomba maombi ni Jessica na mjibu maombi ni Kafulila ambaye hakuwa na pingamizi kwa muomba maombi ya talaka.

Kafulila amefanya kitu wanaume wengi wanakosa uthubutu wa kufanya na kuishia kufa kwa stroke.
Chief FB kigogo zipo nyingi sijui ipi ni ipi
 
Wapo wanawake wema tu na wanadumu kwenye ndoa zao lakini jambo hilo linategemea sana na malezi aliyokulia

Wanawake wengi wakishakuwa na kipato cha uwakika na wanaweza wakajisimamia wenyewe ktk maisha, basi kama yupo kwenye ndoa basi hiyo ndoa kudumu ni kudra za m/mungu tu.
 
Back
Top Bottom