Mahakama yazuia ombi la kampuni ya NSK kuifilisi Dangote Cement

Duh bora asee, jana nilifadhaika sana kusikia, mtoa mada alinichanganya sana.
 
Tulidanganywa kuwa anafanya service ya week mbili kumbe anakusanya virago vyake aondoke uwekezaji bongo umemshinda.

=====

Mahakama Kuu imezuia kufungwa kwa Kiwanda cha Dangote Cement Limited ambacho mdeni wake aliomba kifungwe....
Mtoa mada awali ulikurupuka ukaandika uongo kuwa kiwanda kinafungwa sababu Tanzania kuna sera mbaya za uwekezaji. Kuna mtu alikurekebisha ndio unajifaraghua na paragrapha kibao. Huna akili bali ni poyoyo Return Of Undertaker
 
Ukweli siku zote unachelewa lakini kwa regime hii ya uwongo uwongo na uzandiki hakuna kitakachofichwa tusikijue.

Soon tutasikia, Mwekezaji alikuwa akiikosesha 'serekale' mapato, huku wakiwa wamekaza shingo.!
Hapa atakuja Kabudi, atatoa mimacho na kusema aaaah wacha Dangote aende, watanzania wana uwezo wa kufunga mikanda na kuvumilia, tutashinda tu.
 
Mpaka sasa huu mtambo aujaanza fanya kazi,kutokana na matatizo ya kiufundi .Dangote ananunua bado umeme toka kampuni inayoitwa TURBINE POWER ya wakenya inayozalisha umeme kutokana na Gesi.umeme anaotumia Dangote kwa siku ni zaidi ya umeme wa mkoa wa Mtwara. Hivyo akisema atumie umeme wa Tanesco mtwara yote itakosa umeme na bado utakuwa aumtoshi.

Kuzalisha umeme wake bado akumsaidii kuepuka matumizi ya makaa ya mawe! kwenye viwanda vya cement Uchomaji wa Gypsum ufanywa na gas,mafuta mazito au makaa ya mawe cjajua why Dangote akufunga gas powered Kiln japo gesi inapatikana Mtwara.....Bado tuna safari ndefu sana Watanzania kuja kufika nchi ya ahaadi.

Mungu ibariki Tanzania🙏
 
Kwa maujenzi haya ya stingler Joji, Standard Geji na mabarabara matumizi ya Cement hapa Tanzania yameongezeka sana na hilo alitakiwi lilete sababu ya kiwanda kutaka kufilisiwa!!. Tukiondoa ushabiki maandazi kuna kitu sehemu hakipo sawa... Ningesema hapa hicho kitu lakini naishia hapa
 
Unamaanisha huyu bush lawyer ndio wakili msomi?
Bush lawyer ndio nini kwanza?
Nafamhamu vizuri Mselewa toka UDSM pale School of Law, na alikuwa mwalimu mzuri sana kwa wanafunzi wenzake.
 
'WHERE WE DARE TO TALK OPENLY.'

Hii ndio kaulimbiu ya JF, sasa mkuu ya nini kuwa muoga kiasi hiko? c'mon brother!
 
The question is why Dangote and not others such as Heidelberg - Twiga Cement TPC PLC started 1959 up to date, Tanga Cement - Simba..started 1978, Lafargel Helcim Tembo at Mbeya started over 30years are still producing without conflict even Camel Cement started 2006....

Kikubwa nachokiona Dangote ana shida zake pamoja na kulaumu nchi kadhaa za Afrika kuwa sera kandamizi kwa wawekezaji na ana mfumo wa kireberali katika kushinikiza nchi anazowekeza kufuata matakwa yake... Mfano nishati anayotumia kwenye uzalishaji wake anaizalisha mwenyewe hii ni kitu kizuri kwake ila kuna sheria ambazo anazikuta kabla yake katika kuzalisha nishati ambazo huenda zinakinzana na takwa lake nk. Ambapo utaratibu wa kuzibadili unahitaji mchakato wa bunge kwanza nk.

So huwezi kutaka kulazimisha takwa lako kwa simu moja tu kwa Rais kisa wewe ni mwekezaji mkubwa...... Swali la msingi unaporuhusu mwekezaji unategemea nini? Kama ni kufaidisha nchi...iwe kwa kodi, ajira, unafuu wa bei za bidhaa, upatikanaji rahisi, fedha za kigeni, furusa nk. Sasa unaona huvipati in full extent unafanyaje? Kuna attached clip hapo juu ilikuwa ya Mwaka 2017 kwenye FT Summit Africa nataka niseme interview kama ile na maswali na majibu huwa vinaandaliwa mahususi kusifu au kushinikiza nchi husika kukubali masharti ya fulani fulani ili kuendelea kuzalisha massive profit bila kumjali mnufaika ambaye ni nchi husika.
Tuna mkanganyo kwenye aina ya mifumo inayo ongoza uchumi wa nchi zetu za kiafrika kati socialism na capitalism tunaichanganya ili kuunda globalization kuna mengi hapo nk.

Dangote ni oppotunist, innovative na predominant so ukiwa una vyote hivi unakuwa Dangote... Magufuli anatamani watanzania tuibuke madongete wapya wa Afrika issue ipo kwenye technical of to know how. Hapo tunakuja wasaidizi wake wanaendaje how committed they are, sera zetu ni zipi na sheria zetu zikoje katika kupata 50/50... Assalamu Alaikum.
 
Mkigombana ndani yaa nyumba Mungu huondoa baraka vile vile kama Nchi inamanung'uniko uchumi huyumbayumba
 
Mbona viwanda vingine vinafanya kazi?
 
Tulishasema wafanyabiashara wababaishaji lazima waondoke mapema. No way ufisadi awamu hii hauruhusiwi la sivyo lazima kifungo kinamhusu!

Wewe ni fala siunkula kwa mgongo wa kod zetu
 
Hapa watu lazima wakae miezi 3 bila salary sio kwa balaa hili, badala ya serikali kuingilia japo iwape unafuu wa kodi ili sehemu ya pesa walipie madeni kunusuru kuathiri supply na vibarua vya watu wake yenyewe itakaa kimya kama haioni.. Kinaweza kisifungwe lakini kikauzwa kufidia deni
 
Is Tanzania a country to invest?

Dangote wellcome in Kenya for further investment
Nakumbuka kipindi cha JK wawekezaji walikuwa wanapewa tax holiday kwa muda fulani japo walikuwa wanatumia vibaya but ilisaidia kuweka mzunguko wa pesa kwenye uchumi na kufanya demand iwe kubwa hivyo kuzidi kuchochea biashara mpya lakini huyu wa sasa hajui chochote kuhusu uchumi zaidi ya kujenga jenga tu mavitu yasiyo na maana
 
Nakubaliana na kila neno lako.

Kashindwa mwenyewe. Asitutie wazimu.

And he is a lightweight too, umeona hiyo clip iliyowekwa humu?

Kaulizwa Tanzania unaendeleaje na uwekezaji? Kajibu tatizo la Tanzania ni business policy, bunge limekomaa na sheria ya gawio la 16% shares za kampuni kwenda kwa serikali. Nilipoenda kuongea na Rais Mstaafu (hajamtaja, atakuwa ni yule mpole mpole aliyemwalika nchini ) akanambia usikonde, hiyo sheria haikuhusu manake hauko kwenye madini.

Kwa hiyo ni Wanageria wenzie kwenye management wanampiga halafu wanamdanganya, mzee tatizo gawio!

Au, ni mwongo, a congenital liar, alizoea serikali za kimagumashi na viongozi syconphants, wapigaji wanaomchekea chekea, sasa kakutana na bandido lenzake halimfagilii utajiri wake, kakoma kuringa.

Aondoke. Saruji haikushuka bei Dangote alipokuja, hit the road Jack!
 
Habari mbaya, Ajira za watanzania zinapotea kwa mara nyingine
Dah! Jamaa alivyoingia madereva wengi sana walipata ajira na kwa mshahara angalau..! Mungu awasimamie pengine na Dangote serikali imemkalia kooni kiasi cha kushindwa kumudu kodi
 
Tulishasema wafanyabiashara wababaishaji lazima waondoke mapema. No way ufisadi awamu hii hauruhusiwi la sivyo lazima kifungo kinamhusu!
Duuuh!!
Kwani unalipwa kwa kuandika katika kila uzi!?
Huu uzi ni maji marefu kwako.
Umeonyesha jinsi gani unakurupuka kama hiyo ID yako.
 
Uwekezaji kumbe ni rahisi hivi,
Yaani unatengeneza jina tu kisha mengine yanatiririka tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…