Mahakama yazuia ubunge wa Halima Mdee na wenzake 18 kuguswa kuanzia leo Juni 27, 2022

Niwaonavyo hawa makamanda bado ni loyal kwa CDM na wanaendelea kuwa na mapenzi na chama chao. Shida pekee iliyopo ni kwamba wana tofauti za kimtazamo na top brass ya CDM.

Vikao vya maamuzi vya vyama yetu vya kisiasa huwa ni rubber stamp tu ya kurasimisha decisions za wenyeviti. Yeyote anayekosana na mwenyekiti huwa hasilimiki. Historia imesheheni mifano mingi ya hao wahanga. Sasa hivi Ayatollah Mbowe akiachia kiti, akakichukua mtu mwingine ambaye hana mtazamo tofauti na kina Mdee, utashangaa wajumbe wa CC na BK watakavyobadili gia angani. Wanaweza kutangaza msamaha usiokuwa na masharti yoyote kwa Mdee na wenzake.

Wenyeviti wa vyama vya siasa waache selfishness na kuweka maslahi ya vyama vyao mbele. Hulka zao za dictatorship hazina manufaa yoyote kwa vyama vyao.
Tatizo lipo kwa hawara wa mwenyekiti yule mama Joyce Mukya. Ndo anafosi baby wake amuondoe Mdee ili yeye apate nafasi.
 
Hilo jina unajiita halafu unakuwa mjinga wa kiwango hiki ni kumdhalilisha mwenye jina
 
Maridhiano makubwa yameshafanyika, chadema hawataki vile viti na hata kama wakitolewa still hawatapeleka watu wengine

Ni kama swala la ruzuku Tu mpaka Leo hawataki Kwa sababu zao binafsi

Viongozi wakuu wamefaidika na maridhiano ya kwao Kwa manufaa yao

Lisu kalipwa pesa zake mbowe nae biashara zake zimefunguliwa vizuri
Kwa hiyo hoja yako ni nini?

Yaani wenzio wamepata walivyokuwa wameibiwa halafu wewe unalalama "kwanini wamepata!!??". You must be very stupid..!!

Na kwani wamepata vya kuhongwa au haki na mali ya jasho lako?

Wamechukua vya kwao walivyokuwa wamenyang'anywa kwa nguvu na kwa hila na huyo SUKUMA GANG mwenzetu mwendazake Jiwe..
 
Hawa watu wakiambiwaga fact wanatukana matusi tu ndio eanachojua.
Wanaambiwa kilasiku humu DJ anajua mchoro A to Z hawaelewi wana kaza mafuvu tu.
Muda ni msemakweli namba moja.
Umeandika ujinga mtupu
 
Tuliwaambia mkatutukana hafukuzwi mtu CHADEMA na hafukuziki ovyo!!!!
KUNA MAANA FULAN KUWA PALE BUNGENI NA MKUU WENU ANAJUA FIKA ….

Kama hajui wawafungulie kesi ya kufoji saini ya Mnyika!

Wajinga ndo waliwao , kaeni kushabikia msiyoyajua!!

Nasikia CHADEMA ngazi za chini wamemwangukia KINANA asaidie Bahati nzuri Memo nimeipata! Who is KINANA then ? You are jocking
Cc Evarist Chahali
Britanicca

Vipi mkuu unaji cc mwenyewe? Ama ndio back up!
 
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo Jumatatu Juni 27, 2022 imetoa zuio la muda la kutofanyika chochote kwenye Ubunge wa Halima Mdee na wenzake 18 mpaka pale itakaposikiliza maombi ya rufaa yao.

Chanzo: MwanaHalisi

===========

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo Jumatatu Juni 27, 2022 imetoa zuio la muda kuhusu kutofanyika chochote kwenye Ubunge wa Halima Mdee na wenzake 18 mpaka pale Mahakama hiyo itakaposikiliza maombi ya Rufaa yao.

Hatua hiyo imekuja baada ya CHADEMA kupitia kwa mawakili wake akiwemo Peter Kibatala, kuwasilisha pingamizi la awali wakipinga maombi mapya ya akina Mdee dhidi yao ambapo wanaiomba mahakama hiyo iwape kibali cha kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama wa chama hicho.

Mdee na wenzake wamefungua maombi Mahakama Kuu dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema (iliyosajiliwa) wakiomba ridhaa ya kufungua shauri la kupinga kuvuliwa uanachama wa Chadema.

Sambamba na maombi hayo ya ridhaa namba 27 ya mwaka 2022, pia wamefungua maombi ya amri ya zuio dhidi ya NEC na Spika, kutochukua hatua dhidi ya uamuzi wa Chadema kuwavua uanachama.

Maombi hayo yaliyopangwa kusikilizwa na Jaji Mustapha Ismail yametajwa leo Jumatatu Juni 27,2022, ndipo mawakili wa Chadema wakaibua pingamizi, dhidi ya maombi hayo ya zuio.
Tukutane 2025 😂😂
 
Kwani aliyeandika kitabu cha 'MFALME JUHA' alilenga nini? Ni mambo halisi ambayo dola inaona sio sahihi lakini inalazimisha yawe sahihi.
Kesi ya kijuha ni ngumu sana kuiamua, inasubiri waamuzi na sio sheria.
Ova
 
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo Jumatatu Juni 27, 2022 imetoa zuio la muda la kutofanyika chochote kwenye Ubunge wa Halima Mdee na wenzake 18 mpaka pale itakaposikiliza maombi ya rufaa yao.

Chanzo: MwanaHalisi

===========

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo Jumatatu Juni 27, 2022 imetoa zuio la muda kuhusu kutofanyika chochote kwenye Ubunge wa Halima Mdee na wenzake 18 mpaka pale Mahakama hiyo itakaposikiliza maombi ya Rufaa yao.

Hatua hiyo imekuja baada ya CHADEMA kupitia kwa mawakili wake akiwemo Peter Kibatala, kuwasilisha pingamizi la awali wakipinga maombi mapya ya akina Mdee dhidi yao ambapo wanaiomba mahakama hiyo iwape kibali cha kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama wa chama hicho.

Mdee na wenzake wamefungua maombi Mahakama Kuu dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema (iliyosajiliwa) wakiomba ridhaa ya kufungua shauri la kupinga kuvuliwa uanachama wa Chadema.

Sambamba na maombi hayo ya ridhaa namba 27 ya mwaka 2022, pia wamefungua maombi ya amri ya zuio dhidi ya NEC na Spika, kutochukua hatua dhidi ya uamuzi wa Chadema kuwavua uanachama.

Maombi hayo yaliyopangwa kusikilizwa na Jaji Mustapha Ismail yametajwa leo Jumatatu Juni 27,2022, ndipo mawakili wa Chadema wakaibua pingamizi, dhidi ya maombi hayo ya zuio.
Chadema wametimiza wajibu wao, nao ni kuwafukuza uanachama basi. Kazi ya kuwatoa bungeni ni ya mamlaka nyingine. Aliyewaingiza bungeni (serikali) ndio yenye jukumu la kuwatoa. Ningeweza kushawishika kuwa Chadema walihusika na kuwaingiza bungeni lakini serikali ilichemka Sana ilipojisahau na kumuingiza mtu aliyekuwa jela Nusrat, bungeni. Chadema hawana ubavu wa kumtoa mtu jela tena usiku. Tena kipindi cha Magu siyo Kweli. Ninashauri Chadema waendelee kufuatilia jambo hili huko mahakamani hata hivyo wategemee maamuzi tofauti. Serikali/ccm inawataka wabunge wa upinzani kwa maslahi yao na hawaiamini Chadema kama itakubali kuleta majina mapya bungeni, na ikikataa ni kuendeleza msimamo kuwa hakukuwa na uchaguzi huru 2020, hali itakayosababisha kukosa baadhi ya misaada au kukosa kuungwa mkono kwa serikali ya Samia na wadau wa demokrasia duniani kitu wanachokihitaji mno hasa awamu hii.
Issue ya hao wabunge Ni aibu tupu kwa bunge na serikali yake. Hivyo siyo kazi nyepesi kuwaondoa.
Kumbuka majibu ya Ndugai pamoja na ushauri wa busara wa spika Mstaafu Mzee Msekwa kuwa akina Halima hawapaswi kuwa bungeni yeye alijibu,nitawalinda kwa gharama zozote, hiyo kauli haikutoka kwake,yuko aliyemtuma na bila shaka anajuta huko aliko. Mbunge anapaswa kudhaminiwa na chama Cha siasa ndo katiba inavyosema. Haijalishi ubovu wa katiba ya vyama ilimradi chama kimesajiliwa na kiliwasilisha katiba yake kwa msajili mkuu wa vyama naye akaipokea na kuikubali itumike na hicho chama huwezi kuhoji matumizi yake kwa kuwa maamuzi yamegusa maslahi ya chama tawala.
 
Kumbe sarakasi zote na Halima na genge lake ni ubunge (matumbo yao) tu,ok fine,ila Chadema haina ishu na ubunge wao kwani hela inayochezewa kuwalipa mishahara na posho zao ni za Watanzania wote,Ila wasitumie jina la Chadema kwani siyo wanachama wetu tena..
 
Niwaonavyo hawa makamanda bado ni loyal kwa CDM na wanaendelea kuwa na mapenzi na chama chao. Shida pekee iliyopo ni kwamba wana tofauti za kimtazamo na top brass ya CDM.

Vikao vya maamuzi vya vyama yetu vya kisiasa huwa ni rubber stamp tu ya kurasimisha decisions za wenyeviti. Yeyote anayekosana na mwenyekiti huwa hasilimiki. Historia imesheheni mifano mingi ya hao wahanga. Sasa hivi Ayatollah Mbowe akiachia kiti, akakichukua mtu mwingine ambaye hana mtazamo tofauti na kina Mdee, utashangaa wajumbe wa CC na BK watakavyobadili gia angani. Wanaweza kutangaza msamaha usiokuwa na masharti yoyote kwa Mdee na wenzake.

Wenyeviti wa vyama vya siasa waache selfishness na kuweka maslahi ya vyama vyao mbele. Hulka zao za dictatorship hazina manufaa yoyote kwa vyama vyao.
Haya mawazo ya ajabu sijui umeyatoa wapi.

Hao wanawake wameenda kinyume na taratibu za chama chao, wameadhibiwa, ajabu lawama zako unampelekea Mbowe!

Listen man, usitoe hukumu kwa kukariri, hii scenario yako ilitumiwa na Samia kumkandamiza Ndugai kule CCM, usiipeleke Chadema.

Suala la Chadema ni separate kabisa, halifanani na mambo ya CCM na tabia zao, na wala halina uhusiano wowote na Mbowe kukaa madarakani muda mrefu.
 
Kwa hiyo hoja yako ni nini?

Yaani wenzio wamepata walivyokuwa wameibiwa halafu wewe unalalama "kwanini wamepata!!??". You must be very stupid..!!

Na kwani wamepata vya kuhongwa au haki na mali ya jasho lako?

Wamechukua vya kwao walivyokuwa wamenyang'anywa kwa nguvu na kwa hila na huyo SUKUMA GANG mwenzetu mwendazake Jiwe..

Eewaaaaaa sasa hayo ndio maridhiano so na nyie mridhie mambo mengine ambayo ccm wamefanya ambayo maybe yaliwaumiza

Msiwe kama watoto yatima kila kitu mnataka nyie ndio msikilizwe
 
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo Jumatatu Juni 27, 2022 imetoa zuio la muda la kutofanyika chochote kwenye Ubunge wa Halima Mdee na wenzake 18 mpaka pale itakaposikiliza maombi ya rufaa yao.

Chanzo: MwanaHalisi

===========

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo Jumatatu Juni 27, 2022 imetoa zuio la muda kuhusu kutofanyika chochote kwenye Ubunge wa Halima Mdee na wenzake 18 mpaka pale Mahakama hiyo itakaposikiliza maombi ya Rufaa yao.

Hatua hiyo imekuja baada ya CHADEMA kupitia kwa mawakili wake akiwemo Peter Kibatala, kuwasilisha pingamizi la awali wakipinga maombi mapya ya akina Mdee dhidi yao ambapo wanaiomba mahakama hiyo iwape kibali cha kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama wa chama hicho.

Mdee na wenzake wamefungua maombi Mahakama Kuu dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema (iliyosajiliwa) wakiomba ridhaa ya kufungua shauri la kupinga kuvuliwa uanachama wa Chadema.

Sambamba na maombi hayo ya ridhaa namba 27 ya mwaka 2022, pia wamefungua maombi ya amri ya zuio dhidi ya NEC na Spika, kutochukua hatua dhidi ya uamuzi wa Chadema kuwavua uanachama.

Maombi hayo yaliyopangwa kusikilizwa na Jaji Mustapha Ismail yametajwa leo Jumatatu Juni 27,2022, ndipo mawakili wa Chadema wakaibua pingamizi, dhidi ya maombi hayo ya zuio.
HAYA NDIYO MAAJABU NDANI YA TAIFA HILI, HAWA WATU CHAMA CHAO KIMESHAWAVUA UBUNGE, SIFA YA KUWA MUNGU NI LAZIMA UPATE RIDHAA YA CHAMA CHAKO,.
>Mambo mengine ni ya ajabu na aibu za wazi kabisa kwa vyombo vyetu tegemewa kwa taifa.
 
Chadema ni nyumba moja na hao kina Halima kaeni pamoja na muyamalize, hichi ni kitu kidogo sana, ehh mijamaa acheni kuonyeshana ubabe uwiii [emoji3062]
 
Back
Top Bottom