britanicca mbona unaandika kama kwamba hii ni mara ya kwanza kwa mbunge/wabunge au wanachama influential wa CHADEMA kufukuzwa na chama lakini watawala wakang'ang'ana/wakakumbatia kwa mbinu hizi hizi za kimahakama hadi wakamaliza muda wao wa ubunge..?
Unajaribu kuwataka watu wamlaumu nani? Mwenyekiti Freeman Mbowe? Katibu John Mnyika?
Sikiliza bwana.
Hakuna cha wajinga ndiyo waliwao wala nini. The main issue hapa ni kuelewa tu namna ya kucheza siasa za hawa maCCM..
Kinachowabeba CHADEMA kwa miaka yote kuendelea kuishi na kuwa wapinzani wakuu na tishio la utawala wa CCM ni uongozi dhabiti wa CHADEMA chini ya mwamba Freeman Aikael Mbowe..!!
Huyu mwamba angekuwa ni mtu wa tamaa na njaa kali, kwa siasa za Bongo huu, CHADEMA ingeshakwenda iliko CUF na NCCR Mageuzi..!
Ukiweza kudhibiti michezo yao hawa maCCM, mtaenda nao sambamba tu na ndiyo maana sometimes huelemewa huishiwa mikakati halali ya kisiasa na huamua kutumia pyuuu pyuuu a.k.a bunduki kuua, kujeruhi, kuteka na kupoteza kama ilivyokuwa kwa TL...
Ndugu, hawa watu wako tayari kumtumia mwanachama yeyote wa CHADEMA na hasa akiwa mbunge na ana maslahi kwao na serikali yao kutumika kama nyundo 🔨🔨🔨 ya kuigongea CHADEMA, basi hata CHADEMA wafuate sheria na taratibu zote za kinidhamu za kichama, hawataweza kumfanya lolote...
Rejea sakata la Zito Zubeiry Ruyagwa Kabwe na wengine..
Kilichopo na kinachoweza kufanyika kwa sasa, ni CHADEMA kuendelea kucheza kimkakati zaidi kwa kuzielewa mbinu zote za adui yao...
Na kwa maoni yangu, wameweza na wameshawalemea vya kutosha na ndiyo maana wakati mwingine wana - opt kutumia nguvu kujaribu kuwadhibiti hawa CHADEMA ambayo nayo ni kama njia iliyokwisha shindwa spectacularly...